DC aliyetumbuliwa atoa waraka mzito kwa Naibu Waziri mpya wa TAMISEMI

DC aliyetumbuliwa atoa waraka mzito kwa Naibu Waziri mpya wa TAMISEMI

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basilla Mwanukuzi ameandika waraka mzito kuhusu utendaji dhaifu wa watumishi wa Halmashauri ambao wanahujumu miradi huku wakiendelea kukingiwa kifua na mamlaka husika.​

Na basillamwanukuzi

Hongera sana @dndejembi kwa kuamniniwa na Rais kua Naibu Waziri TAMISEMI ninakupongeze sana ndugu nikuombe utusaidie kama Watanzania hasa kwenye miradi ya maendeleo nchi nzima umsaidie Mhe Rais @Samia_suluhu_hassan na Serikali ya awamu ya 6 inayo elekeza mabillion ya fedha kwenye miradi ya maendeleo kwa ajili ya Watanzania kwenye miundombinu ya Afya , Elimu, Maji, barabara ,miradi ya kimkakati kwa ajili ya mapato ya Halmashauri etc lakini mambo hayaendi kama ilivyopangwa​

Hali ni TETE , hali ni MBAYA wananchi wamekata tamaa. Wananchi wanateseka Fedha zinakuja kwa wingi kutoka Serikali kuu zikifika halmashauri fedha hazimalizi miradi , na fedha zingine zinakuja zinakaa tu kwenye account miradi haianzi , nikuombe katika ziara zako za mwanzo anza na KOROGWE​

HALI NI MBAYAAAA . Na hakuna mwenye ujasiri wa kusema au kuchukua hatua​

Wewe ni kijana mchapakazi na bahati nzuri umeshawahi kua DC .​

Korogwe is a special case iko ICU kwenye swala la utekelezaji wa miradi ya maendeleo ukiacha madarasa. Niko tayari kukupa ushirikiano kumsaidia Rais wangu, Chama Changu na Taifa langu na zaidi wananchi wanaodhulumiwa haki yao inayotekelezwa kwa uaminifu na Serikali yao inayoongozwa na mama mwenye kufahamu 'uchungu wa mwana' na ndio sababu anaelekeza fedha hizi zikasaidie wananchi.​

Matokeo yake hakuna manufaa kwa sababu fedha zinaisha , miradi haiishi Wananchi hawapati huduma.​

Ni bora kua na mradi mmoja ukaisha kuliko kua na miradi kumi ambayo hakuna hata mmoja umeisha. Miongozo ya TAMISEMI haifuatwi, Maelekezo hayafuatwi mamlaka husika hazichukui hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.​

TUNAKWENDA WAPI???🇹🇿​

HAIKUBALIKI DUNIANI WALA MBINGUNI​

#MbelekoYaBasilla #kiongoziWaWananchi #sautiYaWatu #MzalendoDamu

Edited · 3d
See translation
mjinga tu. Mtu unaruhusu vigogo wapige hela ya umma kwa urefu wa kamba ya malisho ya kila mmoja halafu unawamwagia mabilioni kama unarushia ndege mpunga unafikiri nini. Lazima utakua mshirika tu.
 
Watanzania wanapenda mizaha sana, Mtu alikuwa DC anajua uchafu wote unaofanyika kwenye halmashauri badala tuungane kupinga uozo huo tunamlaumu tena aliyetufumbua macho.. ukumbuke hilo eneo la Korogwe lina wabunge 2 lakini hujawahi kuwasikia wakipaza sauti juu ya matatizo hayo hadi akabaki DC peke yake na RC Mgumba ambao wote wametumbuliwa
Huyo anaemshambulia Basili kwa kuusema ukweli ni FISADI anaetaka Basili asiendelee kuibua uchafu uliopo katika halmashauri nchi nzima. Kwa Sasa wanaoifadi keki ya taifa Ni viongozi wa juu na si mwananchi wa kawaida.
 
Atoe ujinga wake kipindi yy ni dc mbona halikuwa apayuki hivyo..
Mganga njaa huyo.
Kwa mfumo wa Tanzania, watu muhimu wa kufanya nao kazi zetu za kupambana na serikali ni wale walio nje ya system!
Na huyu ni mtu muhimu

Hawa Wana umuhimu wao mkubwa wa kutufumbua macho, na si watu wa kuwabeza!

Watu tunaowasifu kwa ukosoaji wa Serikali kwa data hai, ni kwasababu ya msaada wa watu Kama hawa!

Kwa Hali zetu za kimaisha Watanzania, Ni vigumu kuiwajibisha serikali ukiwa serikalini
Ukiona mtu anamshangaa mtu kuwasema watendaji wa Serikali akiwa nje ya system, eti kwa Nini asiseme akiwa ndani, huyo ni mjinga wa mawazo! Yaani anashindwa kujua kuwa Tanzania imewafunga watumishi wake kuongea kinyume na matakwa ya Serikali, hio haiwezekani!
Kama wewe mtumishi Basi jaribu kuongea hayo yanayojiri kwenye ofisi yako!
Anayeweza kuisema serikali yake Ni Raisi peke yake!
Hata shujaa JPM hakuisema serikali akiwa waziri!

Tusiwapuuze wanaoamua kuisema serikali wakitoka nje
Bila hao tutaendelea kuwa mazuzu wa kutojua yaliyopo ndani ya serikali

Raia tuna haki ya kujua serikali inafanya Nini kizuri na Nini kibaya
Mfumo unataka yatajwe mazuri tu!
Je, tutayajua vipi Yale mabaya?

Ni mawazo yangu kuwa ingekuwa vizuri kuwa wote wanaoondoka serikalini wangetoa mrejesho wa jinsi Serikali inavyowajibika na isivyowajibika!

Raia tungezidi kuwa na upeo wa ufahamu kuhusu serikali yetu!


Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Alikuwa na kila madaraka kabla ya kutumbuliwa, alifanyaje kudhibiti hayo yote??
Huu waraka wake japo alihisi utasaidia kumfanya aonekane kiuhalisia umezidi kumuharibia na kudhihirisha kuwa hakuwa sahihi kwa nafasi aliyopewa maana alishindwa kuzuia ujinga wote huo.
 
Alikuwa na kila madaraka kabla ya kutumbuliwa, alifanyaje kudhibiti hayo yote??
Huu waraka wake japo alihisi utasaidia kumfanya aonekane kiuhalisia umezidi kumuharibia na kudhihirisha kuwa hakuwa sahihi kwa nafasi aliyopewa maana alishindwa kuzuia ujinga wote huo.
Tatizo naloliona ni DC kuamini kuwa Wana maamuzi ya fedha za miradi kumbe si kweli fedha zote za Halmashauri ziko chini ya Mkurugenzi Sasa asipohusishwa katika matumizi basi ataanza majungu na kuwapakazia wenzake Kila kitu.Akihusishwa hutamsikia hata mara moja akilalamika
 
Huyo Basilla Mwanukuzi alikuwa DC wa hapo hapo Korogwe na akashindwa kuyarekebisha yote hayo, sasa leo analalamika nini?

Alitegemea hayo mapungufu yote nani aje kuyatatua?

Kama anadhani juhudi zake katika kuyatatua hayo ndio zimepelekea yeye kutumbuliwa, kwanini asimlaumu mama Samia aliyemtumbua?
 
CHADEMA NDIO kimbilio mpo wapi kwenye hili nalo mkaliangalie mlitolee majawabu.
Hawana huo muda kwa sasa. Agenda ya ufisadi kwa sasa wameitupa. Huyo Basila hajui kuishi na watu ndo maana katumbuliwa. Ukifika sehemu soma mchezo kwanza sio unakurupuka tu na kutaka kuwavuruga watu. Hii nchi kuna watu wako kwenye vitengo kwa elimu ya kuunga unga ila hata viongozi waandamizi wanawaendea kwa adabu. Kuna mzee mmoja alikuwa ni fundi tu wizarani ila hata mkurugenzi wa idara yake alikuwa anamhanya mbaya. Basila ajifunze.
 

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basilla Mwanukuzi ameandika waraka mzito kuhusu utendaji dhaifu wa watumishi wa Halmashauri ambao wanahujumu miradi huku wakiendelea kukingiwa kifua na mamlaka husika.

Na basillamwanukuzi

Hongera sana @dndejembi kwa kuamniniwa na Rais kua Naibu Waziri TAMISEMI ninakupongeze sana ndugu nikuombe utusaidie kama Watanzania hasa kwenye miradi ya maendeleo nchi nzima umsaidie Mhe Rais @Samia_suluhu_hassan na Serikali ya awamu ya 6 inayo elekeza mabillion ya fedha kwenye miradi ya maendeleo kwa ajili ya Watanzania kwenye miundombinu ya Afya , Elimu, Maji, barabara ,miradi ya kimkakati kwa ajili ya mapato ya Halmashauri etc lakini mambo hayaendi kama ilivyopangwa

Hali ni TETE , hali ni MBAYA wananchi wamekata tamaa. Wananchi wanateseka Fedha zinakuja kwa wingi kutoka Serikali kuu zikifika halmashauri fedha hazimalizi miradi , na fedha zingine zinakuja zinakaa tu kwenye account miradi haianzi , nikuombe katika ziara zako za mwanzo anza na KOROGWE​


HALI NI MBAYAAAA . Na hakuna mwenye ujasiri wa kusema au kuchukua hatua

Wewe ni kijana mchapakazi na bahati nzuri umeshawahi kua DC .

Korogwe is a special case iko ICU kwenye swala la utekelezaji wa miradi ya maendeleo ukiacha madarasa. Niko tayari kukupa ushirikiano kumsaidia Rais wangu, Chama Changu na Taifa langu na zaidi wananchi wanaodhulumiwa haki yao inayotekelezwa kwa uaminifu na Serikali yao inayoongozwa na mama mwenye kufahamu 'uchungu wa mwana' na ndio sababu anaelekeza fedha hizi zikasaidie wananchi.​

Matokeo yake hakuna manufaa kwa sababu fedha zinaisha , miradi haiishi Wananchi hawapati huduma.​

Ni bora kua na mradi mmoja ukaisha kuliko kua na miradi kumi ambayo hakuna hata mmoja umeisha. Miongozo ya TAMISEMI haifuatwi, Maelekezo hayafuatwi mamlaka husika hazichukui hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

TUNAKWENDA WAPI???[emoji1241]
HAIKUBALIKI DUNIANI WALA MBINGUNI

#MbelekoYaBasilla #kiongoziWaWananchi #sautiYaWatu #MzalendoDamu

Edited · 3d
See translation
Basi huyu alitolewa kwa halali kabisa maana hanitambui.
Kwenye Wilaya ambapo yeye alikua DC anasema hali ni mbaya.
Pesa inakuja miradi haitekelezwi na blaa blaa kibao.
Alipokuwa DC alifanya nini la maana kuondoa hali hiyo ?
Akae pembeni apishe wenzake wafanye kazi
 
Wana CCM wamejazana halmashauri huk no wakkuu was idara wote ccm. Anaiba nani?

Mtumishi kama sio mwana CCM hupewi kitengo hata ungekuwa PhD holder
 
Korogwe is a special case iko ICU kwenye swala la utekelezaji wa miradi ya maendeleo ukiacha madarasa. Niko tayari kukupa ushirikiano kumsaidia Rais wangu, Chama Changu na Taifa langu na zaidi wananchi wanaodhulumiwa haki yao inayotekelezwa kwa uaminifu na Serikali yao inayoongozwa na mama mwenye kufahamu 'uchungu wa mwana' na ndio sababu anaelekeza fedha hizi zikasaidie wananchi.
Palizi na kijembe
 
Back
Top Bottom