DC aliyetumbuliwa atoa waraka mzito kwa Naibu Waziri mpya wa TAMISEMI

DC aliyetumbuliwa atoa waraka mzito kwa Naibu Waziri mpya wa TAMISEMI

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basilla Mwanukuzi ameandika waraka mzito kuhusu utendaji dhaifu wa watumishi wa Halmashauri ambao wanahujumu miradi huku wakiendelea kukingiwa kifua na mamlaka husika.

Na basillamwanukuzi

Hongera sana @dndejembi kwa kuamniniwa na Rais kua Naibu Waziri TAMISEMI ninakupongeze sana ndugu nikuombe utusaidie kama Watanzania hasa kwenye miradi ya maendeleo nchi nzima umsaidie Mhe Rais @Samia_suluhu_hassan na Serikali ya awamu ya 6 inayo elekeza mabillion ya fedha kwenye miradi ya maendeleo kwa ajili ya Watanzania kwenye miundombinu ya Afya , Elimu, Maji, barabara ,miradi ya kimkakati kwa ajili ya mapato ya Halmashauri etc lakini mambo hayaendi kama ilivyopangwa

Hali ni TETE , hali ni MBAYA wananchi wamekata tamaa. Wananchi wanateseka Fedha zinakuja kwa wingi kutoka Serikali kuu zikifika halmashauri fedha hazimalizi miradi , na fedha zingine zinakuja zinakaa tu kwenye account miradi haianzi , nikuombe katika ziara zako za mwanzo anza na KOROGWE​


HALI NI MBAYAAAA . Na hakuna mwenye ujasiri wa kusema au kuchukua hatua

Wewe ni kijana mchapakazi na bahati nzuri umeshawahi kua DC .

Korogwe is a special case iko ICU kwenye swala la utekelezaji wa miradi ya maendeleo ukiacha madarasa. Niko tayari kukupa ushirikiano kumsaidia Rais wangu, Chama Changu na Taifa langu na zaidi wananchi wanaodhulumiwa haki yao inayotekelezwa kwa uaminifu na Serikali yao inayoongozwa na mama mwenye kufahamu 'uchungu wa mwana' na ndio sababu anaelekeza fedha hizi zikasaidie wananchi.​

Matokeo yake hakuna manufaa kwa sababu fedha zinaisha , miradi haiishi Wananchi hawapati huduma.​

Ni bora kua na mradi mmoja ukaisha kuliko kua na miradi kumi ambayo hakuna hata mmoja umeisha. Miongozo ya TAMISEMI haifuatwi, Maelekezo hayafuatwi mamlaka husika hazichukui hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

TUNAKWENDA WAPI???🇹🇿
HAIKUBALIKI DUNIANI WALA MBINGUNI

#MbelekoYaBasilla #kiongoziWaWananchi #sautiYaWatu #MzalendoDamu

Edited · 3d
See translation

Kafulila kaharibu watu wengi Sana. Wakitumbuliwa wanaanza kuandika mambo mengi ili warudishwe Tena.
 
Ukiachwa, achika

Hivi wangekuwa wanataka ufanisi TAMISEMI wangekuwa wana wawekea mawaziri wapole.

Halafu mtu mwenyewe si alikuwa na maisha mengine kabla ya siasa, ata hao hakina Happy, Makonda na wengineo ambao maisha yao yote wanajua porojo za UVCCM tu na ndoto za uongozi washaanza kusahau. Seuse yeye aliekuwa na maisha mengine kabla ya teuzi.

Amepambana wenyewe awataki watu wanoko basi inatosha njoo JF uwakejeli kwa siri maisha mengine yaendelee. Ukitaka teuzi hadharani sifia ‘bi Tozo’ anaupiga mwingi.
 
Duh mnaonekana mmekata tamaa na maisha, yaani unaona sawa kabisa viongozi wa umma kuiba kwa sababu mishahara yao ni midogo?? hamsaidiki nyie hope hamko wengi

Duh unnaonekana hujakata tamaa na maisha, yaani unakemea wizi hivi kwasababu mshahara wako mkubwa sanaa?
Unasaidike wewe hope uko pekee yako.

ILA HILO LA MISHAHARA MIDOGO UMELIONA?

#YNWA
 
Apunguze UMBEA.

Yaani mtu amesoma miaka na miaka anaajiriwa Halmashauri mshahara 745k ukitoa makato 585k

Huku mwenzie aliyesoma nae kaajiriwa taasisi mshahara 1.8Mil

Kwanini asiibe.

Amwambie huyo waziri aanze na mishahara ya halmashauri kwanza na sio mabaya tuuu.

BILA KUANGALIA MASLAHI YA WATUMISHI WA HALMASHAURI BASI WATAIBA SANAAA.

#YNWA
Kama mshahara hautoshi si mtafute shughuli nyingine ya kufanya
 
Nampongeza sana huyu Binti ni uzalendo kusema hayo, Nia njema anayo na ni wajibu wake kama raia na ni haki yake kufichua kasoro na maovu na kuomba mamlaka ifanyie kazi. Hongera kwake

Hana uzalendo wowte, ni karma inamtafuna kwa alivyomfanyia William Mngazija wa ITV kule korogwe kwa kumsweka ndani. Hana lolote.
 
Apunguze UMBEA.

Yaani mtu amesoma miaka na miaka anaajiriwa Halmashauri mshahara 745k ukitoa makato 585k

Huku mwenzie aliyesoma nae kaajiriwa taasisi mshahara 1.8Mil

Kwanini asiibe.

Amwambie huyo waziri aanze na mishahara ya halmashauri kwanza na sio mabaya tuuu.

BILA KUANGALIA MASLAHI YA WATUMISHI WA HALMASHAURI BASI WATAIBA SANAAA.

#YNWA
Ngozi nyeusi hata umlipe bln 2 atakwiba tu !

Ova
 
Watanzania wanapenda mizaha sana, Mtu alikuwa DC anajua uchafu wote unaofanyika kwenye halmashauri badala tuungane kupinga uozo huo tunamlaumu tena aliyetufumbua macho.. ukumbuke hilo eneo la Korogwe lina wabunge 2 lakini hujawahi kuwasikia wakipaza sauti juu ya matatizo hayo hadi akabaki DC peke yake na RC Mgumba ambao wote wametumbuliwa
Watanzania wanapenda uwizi

Ova
 
Yaani Tz kaazi kweli kweli, wanashabikia wanaoiba pesa halmashauri, Kodi za wanancgi, kwa kisingizio cha mishahara midogo! Sasa kama mishahara midogo kwenye halmashauri, mbona graduates wapo wengi wamejaa mtaani ambao hawana kazi, na ambao hata wako tayari kufanya hizo kazi, kwa mishahara midogo zaidi ya hiyo badala ya kuendelea kuendekeza hai wezi serikalini.... Aiseee ni kaazi kweli kweli.
Wezi,mafisadi uraiani wanaonekana

Mashujaa

Ova
 
Watanzania wanapenda mizaha sana, Mtu alikuwa DC anajua uchafu wote unaofanyika kwenye halmashauri badala tuungane kupinga uozo huo tunamlaumu tena aliyetufumbua macho.. ukumbuke hilo eneo la Korogwe lina wabunge 2 lakini hujawahi kuwasikia wakipaza sauti juu ya matatizo hayo hadi akabaki DC peke yake na RC Mgumba ambao wote wametumbuliwa
Atoe ujinga wake kipindi yy ni dc mbona halikuwa apayuki hivyo..
Mganga njaa huyo.
 
Kwa nchi yetu bila kuboresha maslahi ya watumishi wa Halmashauri walio ICU itakuwa sawasawa na bure tu,hata ungekuwa wewe ukiiba Billion 5 kesi ikienda mahakamani unahukumiwa kwenda jela miaka 5 au faini million 5,sasa kwanini mtu asijitoe muhanga
 
Back
Top Bottom