DC Arusha ambaye aliwahi kutoa 'Singo' ya kumsifia Magufuli kuwa ni jembe adai kuwa Magufuli alikuwa ni fisadi

Nchi hii ni sahihi tu walioimba navumilia shida
Vumilia shida
Yaan Rais wetu anawavumilia hawa jamaa
Yaan hawa ni vumilia shida navumilia tu
Ningekuwa Rais Samia ningewapiga chini viongozi wote wenye element za ccm
 
Katika hali ya kustaajabisha, DC wa Arusha Kenani Kihongosi ambae aliwahi kutoa 'Singo' niliyoambatanisha hapo chini ya kumsifia Magufuli kwa kudai kuwa Magufuli alikuwa ni jembe la kila kitu aibuka na kudai kuwa Magufuli alikuwa ni fisadi.

Anadai kuwa katika awamu hiyo Serikali ilikuwa haiweki wazi kuwa imekopa nini na kwa matumizi gani.

Kilichonifanya nilete huu uzi siyo tu kumshangaa Bwana huyu bali nataka niweke wazi kuwa Tanzania hatuendelei kwa sababu ya kuwa na viongozi wanafiki.

Anachomaanisha huyu Bwana ni kwamba alikuwa anajua kabisa kuwa Magufuli alikuwa ni fisadi lakini hakusema kipindi Magufuli akiwa hai ili kulinda ugali wake.

Katika Mataifa yaliyo serious viongozi huweka misimamo yao mbele kwa maendeleo ya Taifa.Viongozi huwa wapo tayari kujiuzulu au kufukuzwa kazi kwa maslahi mapana ya Taifa.

Lakini huku kwetu ni tofauti.Viongozi wapo tayari kutetea ujinga,ufisadi,wizi,mauaji,ukandamizaji wa wananchi na kadhalika ili kulinda ugali wao.Hapa Tanzania viongozi wapo tayari kumtetea kiongozi aliebadilika kuwa kichaa au mwendawazimu ili kulinda nyadhifa zao.

Katika hali kama hii usitegemee Taifa kuendelea kamwe.Hii ni kwa sababu pale kiongozi anapoamua kubadilika kuwa fisadi,mwizi,mkandamizaji au hata kichaa basi hulindwa na chama chake pamoja na viongozi wengine waliopo madarakani ambao lengo lao ni kulinda nyadhifa zao na wala siyo kutetea maslahi mapana ya Taifa.

CCM kwa miaka mingi imekuwa ikitoa viongozi wa aina ya huyu Bwana na ndiyo maana Tanzania miaka nenda haiendelei.Ni muda muafaka sasa CCM kukaa pembeni ili kupisha vyama vingine vya siasa ambavyo vina maono pamoja na nia ya dhati ya kulikomboa Taifa hili.
View attachment 2064795View attachment 2064796View attachment 2064797
Ccm ni ukoo wa kambare, kila mtu ana mandevu, ni mwendo wa kujiropokea tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningekuwa ni mimi, kiongozi yeyote anayenisifia hata pale ninapokuwa nimechemka, NAMTUMBUA mara moja.

Au ili kuwajua wanafiki ndani ya serikali yangu naweza nikaamua kutoa wazo la kipuuzi/ kipumbavu kwa kusudi ili niwatambue wanafiki watakaosifia wazo/jambo hilo wakati wakijua ni la kipuuzi.
Hao viongozi wa hiyo ccm wana upeo mkubwa kiasi hicho sasa ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wengi iliwalazimu kukaa kimya au kusifia kwa sababu waliogopa kitachowakuta baada ya hapo kwani sote tunajua wale wachache waliothubutu kukosoa sera za marehemu nini kiliwapata.
 
Huyu kihongosi magufuli ndie aliyempa maisha baada ya kumfurahisha kwa kusema atamuua zito kesho akapewa u DC Arusha.

Yule jamaa bana ulikuwa ukimshambulia au kumuua mpinzani anakupandisha cheo, ama kuhakikisha unadumu kwenye nafasi yako. Wote waliomshambulia Lisu wanamaisha, hali kadhalika kwa waliomuua saa8, nk. Akina Kingai, Mambosasa nk wote uovu ndio umewanyanyua.
 
Nchi hii nimegundua haiendelei n awala haitokuja kuendelea sabab vijana wote wanakimbilia kwenye shugul zisizo za uzalishaj bali ni shiguli za matumizi na mipango mipango..management..

Sasa mna manage nin na hamzalish chochote..

Na ndio weng wamekua watafta nyadhifa kwa udi na uvumba..uchawa..etc..mipango mipango..yaan ni ujasiriamal mpya...kujipenyeza penyeza upate wadhifa na madaraka...kamwe tutazunguka humu humu

Na ndo wanaongoza kupiga vita vijana wachakarikaj na kuwaundia kesi za uhujumu uchumi...
 
Katika hali ya kustaajabisha, DC wa Arusha Kenani Kihongosi ambae aliwahi kutoa 'Singo' niliyoambatanisha hapo chini ya kumsifia Magufuli kwa kudai kuwa Magufuli alikuwa ni jembe la kila kitu aibuka na kudai kuwa Magufuli alikuwa ni fisadi.

Anadai kuwa katika awamu hiyo Serikali ilikuwa haiweki wazi kuwa imekopa nini na kwa matumizi gani.

Kilichonifanya nilete huu uzi siyo tu kumshangaa Bwana huyu bali nataka niweke wazi kuwa Tanzania hatuendelei kwa sababu ya kuwa na viongozi wanafiki.

Anachomaanisha huyu Bwana ni kwamba alikuwa anajua kabisa kuwa Magufuli alikuwa ni fisadi lakini hakusema kipindi Magufuli akiwa hai ili kulinda ugali wake.

Katika Mataifa yaliyo serious viongozi huweka misimamo yao mbele kwa maendeleo ya Taifa.Viongozi huwa wapo tayari kujiuzulu au kufukuzwa kazi kwa maslahi mapana ya Taifa.

Lakini huku kwetu ni tofauti.Viongozi wapo tayari kutetea ujinga,ufisadi,wizi,mauaji,ukandamizaji wa wananchi na kadhalika ili kulinda ugali wao.Hapa Tanzania viongozi wapo tayari kumtetea kiongozi aliebadilika kuwa kichaa au mwendawazimu ili kulinda nyadhifa zao.

Katika hali kama hii usitegemee Taifa kuendelea kamwe.Hii ni kwa sababu pale kiongozi anapoamua kubadilika kuwa fisadi,mwizi,mkandamizaji au hata kichaa basi hulindwa na chama chake pamoja na viongozi wengine waliopo madarakani ambao lengo lao ni kulinda nyadhifa zao na wala siyo kutetea maslahi mapana ya Taifa.

CCM kwa miaka mingi imekuwa ikitoa viongozi wa aina ya huyu Bwana na ndiyo maana Tanzania miaka nenda haiendelei.Ni muda muafaka sasa CCM kukaa pembeni ili kupisha vyama vingine vya siasa ambavyo vina maono pamoja na nia ya dhati ya kulikomboa Taifa hili.
View attachment 2064795View attachment 2064796View attachment 2064797
CCM kwa miaka mingi imekuwa ikitoa viongozi wa aina ya huyu Bwana na ndiyo maana Tanzania miaka nenda haiendelei.Ni muda muafaka sasa CCM kukaa pembeni ili kupisha vyama vingine vya siasa ambavyo vina maono pamoja na nia ya dhati ya kulikomboa Taifa hili.
 
Yule jamaa bana ulikuwa ukimshambulia au kumuua mpinzani anakupandisha cheo, ama kuhakikisha unadumu kwenye nafasi yako. Wote waliomshambulia Lisu wanamaisha, hali kadhalika kwa waliomuua saa8, nk. Akina Kingai, Mambosasa nk wote uovu ndio umewanyanyua.
Wanakula mali ya haramu
 
Back
Top Bottom