DC Arusha ambaye aliwahi kutoa 'Singo' ya kumsifia Magufuli kuwa ni jembe adai kuwa Magufuli alikuwa ni fisadi

DC Arusha ambaye aliwahi kutoa 'Singo' ya kumsifia Magufuli kuwa ni jembe adai kuwa Magufuli alikuwa ni fisadi

Nilishangaa siku Kihongosi alipopendekezwa kuwa Katibu mkuu wa UVCCM lakini kinachonishangaza zaidi ni kwa nini mpaka sasa bado yupo hapo.
Huyo naye ni zao la kokoro,ila bado yupo kwa sababu hakuna kama yeye na ndiyo maana bora liende.Hata hivyo tunawaombea mnyukano uendelee.
 
Chawa baada ya godoro kuanikwa nje juani wanatafuta kivuli
 
viongozi wanafiki.
VqbuYV0.gif
 
Ccm wanafanya ujinga lkn wananchi tunaoikubali ndiyo wajinga kabisaaaaaa...
Kiongozi anachojali ni tumbo lake na la wanaomzunguka hajali wengine kwahivyo anatetea chochote mradi aendelee kujaza mtumbo wake
 
Kukosekana uwazi hakumaanishi ni kufanya ufisadi ...! Kunaweza kukakosa uwazi na ufisadi usiwepo na pia kunaweza kukawa na uwazi lakini ufisadi pia ukawepo.
Hii ni kwa mujibu wa maoni yako?Yaani unataka niamini hiki ulichoandika hapa?Wewe ni nani hadi nikiamini?

Ulichoandika kina sifa ya kuwa facts kwa hiyo nahitaji supporting evidence kutoka official sources.
 
Kama rais Samia hawezi kujifunza kitu kutoka kwa hawa njaa kali basi itakuwa ajabu sana. Ingekuwa mimi kila anayenisifia kupita inavyostahili ningemtumbua niwaache wale wanaonikosoa tu.

..SSH naye alikuwa sehemu ya genge lililokuwa likilaghai kwamba miradi inatekelezwa kwa fedha za ndani.

..Mtu aliyesema risasi tatu zilikuwa linatosha kumuua TL kama wauwaji wangekuwa ni watu wa serikali anaweza vipi leo hii kukana kuwa hakuwa sehemu ya mauza-uza ya utawala wa Magufuli?

..Sukuma gang, kama kweli wapo, wanayo haki ya kumchukia na kumnunua SSH kwasababu amewaruka kimanga wakati alikuwa mwenzao wakati Magufuli akiwa hai.

Cc Tindo, Erythrocyte, THE BIG SHOW , Nguruvi3
 
Hii ni kwa mujibu wa maoni yako?Yaani unataka niamini hiki ulichoandika hapa?Wewe ni nani hadi nikiamini?

Ulichoandika kina sifa ya kuwa facts kwa hiyo nahitaji supporting evidence kutoka official sources.
Kwa hiyo wewe unafikiri, logically ipo sawa kumtuhumu MTU ufisadi kwa kigezo cha kukosa transparency kwenye serikali yake? Je sababu hiyo inatosha kumtia hatiani?Uwazi ni kitu kingine na ufisadi ni kitu kingine japokuwa in some cases (not all cases) kutokuwa na uwazi huambatana ufisadi lakini haimaanishi moja kwa moja kukiwa hakuna uwazi ndo kuna ufisadi.
 
Katika hali ya kustaajabisha, DC wa Arusha Kenani Kihongosi ambae aliwahi kutoa 'Singo' niliyoambatanisha hapo chini ya kumsifia Magufuli kwa kudai kuwa Magufuli alikuwa ni jembe la kila kitu aibuka na kudai kuwa Magufuli alikuwa ni fisadi.

Anadai kuwa katika awamu hiyo Serikali ilikuwa haiweki wazi kuwa imekopa nini na kwa matumizi gani.

Kilichonifanya nilete huu uzi siyo tu kumshangaa Bwana huyu bali nataka niweke wazi kuwa Tanzania hatuendelei kwa sababu ya kuwa na viongozi wanafiki.

Anachomaanisha huyu Bwana ni kwamba alikuwa anajua kabisa kuwa Magufuli alikuwa ni fisadi lakini hakusema kipindi Magufuli akiwa hai ili kulinda ugali wake.

Katika Mataifa yaliyo serious viongozi huweka misimamo yao mbele kwa maendeleo ya Taifa.Viongozi huwa wapo tayari kujiuzulu au kufukuzwa kazi kwa maslahi mapana ya Taifa.

Lakini huku kwetu ni tofauti.Viongozi wapo tayari kutetea ujinga,ufisadi,wizi,mauaji,ukandamizaji wa wananchi na kadhalika ili kulinda ugali wao.Hapa Tanzania viongozi wapo tayari kumtetea kiongozi aliebadilika kuwa kichaa au mwendawazimu ili kulinda nyadhifa zao.

Katika hali kama hii usitegemee Taifa kuendelea kamwe.Hii ni kwa sababu pale kiongozi anapoamua kubadilika kuwa fisadi,mwizi,mkandamizaji au hata kichaa basi hulindwa na chama chake pamoja na viongozi wengine waliopo madarakani ambao lengo lao ni kulinda nyadhifa zao na wala siyo kutetea maslahi mapana ya Taifa.

CCM kwa miaka mingi imekuwa ikitoa viongozi wa aina ya huyu Bwana na ndiyo maana Tanzania miaka nenda haiendelei.Ni muda muafaka sasa CCM kukaa pembeni ili kupisha vyama vingine vya siasa ambavyo vina maono pamoja na nia ya dhati ya kulikomboa Taifa hili.
View attachment 2064795View attachment 2064796View attachment 2064797
Ana kasoro gani na Nd.ug.ai? Wote waliopigia makofi na kumsifia hawapo naye tena
 
njaa na umaskini ni mbaya sana.unaweza hata kujijana jinsia yako kisa pesa.huyu njaa ya utumbo mpana inamsumbua
 
Katika hali ya kustaajabisha, DC wa Arusha Kenani Kihongosi ambae aliwahi kutoa 'Singo' niliyoambatanisha hapo chini ya kumsifia Magufuli kwa kudai kuwa Magufuli alikuwa ni jembe la kila kitu aibuka na kudai kuwa Magufuli alikuwa ni fisadi.

Anadai kuwa katika awamu hiyo Serikali ilikuwa haiweki wazi kuwa imekopa nini na kwa matumizi gani.

Kilichonifanya nilete huu uzi siyo tu kumshangaa Bwana huyu bali nataka niweke wazi kuwa Tanzania hatuendelei kwa sababu ya kuwa na viongozi wanafiki.

Anachomaanisha huyu Bwana ni kwamba alikuwa anajua kabisa kuwa Magufuli alikuwa ni fisadi lakini hakusema kipindi Magufuli akiwa hai ili kulinda ugali wake.

Katika Mataifa yaliyo serious viongozi huweka misimamo yao mbele kwa maendeleo ya Taifa.Viongozi huwa wapo tayari kujiuzulu au kufukuzwa kazi kwa maslahi mapana ya Taifa.

Lakini huku kwetu ni tofauti.Viongozi wapo tayari kutetea ujinga,ufisadi,wizi,mauaji,ukandamizaji wa wananchi na kadhalika ili kulinda ugali wao.Hapa Tanzania viongozi wapo tayari kumtetea kiongozi aliebadilika kuwa kichaa au mwendawazimu ili kulinda nyadhifa zao.

Katika hali kama hii usitegemee Taifa kuendelea kamwe.Hii ni kwa sababu pale kiongozi anapoamua kubadilika kuwa fisadi,mwizi,mkandamizaji au hata kichaa basi hulindwa na chama chake pamoja na viongozi wengine waliopo madarakani ambao lengo lao ni kulinda nyadhifa zao na wala siyo kutetea maslahi mapana ya Taifa.

CCM kwa miaka mingi imekuwa ikitoa viongozi wa aina ya huyu Bwana na ndiyo maana Tanzania miaka nenda haiendelei.Ni muda muafaka sasa CCM kukaa pembeni ili kupisha vyama vingine vya siasa ambavyo vina maono pamoja na nia ya dhati ya kulikomboa Taifa hili.
View attachment 2064795View attachment 2064796

1641051816312.png
 
..SSH naye alikuwa sehemu ya genge lililokuwa likilaghai kwamba miradi inatekelezwa kwa fedha za ndani.
Na alipita akishadidia hilo, sijui anawezaje kujitenga sasa.
..Mtu aliyesema risasi tatu zilikuwa linatosha kumuua TL kama wauwaji wangekuwa ni watu wa serikali anaweza vipi leo hii kukana kuwa hakuwa sehemu ya mauza-uza ya utawala wa Magufuli?
Ilikuwa ni mbaya sana! sana tu . Alikuwa ''accomplice'' hakuna shaka
 
Nilichogundua kwa hasa wachumia tumbo wa lumumba ni kua kwanza wanamsoma kiongozi wao ni mtu wa namna gani.

Kwa jinsi wanaojitokeza wengi kumtupia lawama mwendazake ilhali zamani walikua wanamsifia ni dhahili kua mama haukua anaelewana na mwendazake kwa namna moja au nyingine na watu wa karibu huenda walijua hicho kitu.

Ndio maana sio viongozi wa chini yake tu ila hata yeye alishwahi kukiri huko nyuma hakukua sawa kwa kutupa madongo utawala uliopita.
Siyo Mama tu, hata Kabudi hajawahi kumkubali Mwendazake, jamaa alikuwa wa hovyo kweli kweli, bora kafa
 
Huyu kihongosi magufuli ndie aliyempa maisha baada ya kumfurahisha kwa kusema atamuua zito kesho akapewa u DC Arusha.
Pamoja simkubali Magufuli, simkubali hiyo dogo na simkubali CCM lakini huyu dogo ameonyesha kuwa msaliti kwa huyo aliyempa maisha aisee.

Hakina mhehe mjinga na asiye na msimamo namna hii, hakuna mhehe snitch aisee, huyu amekosa shukrani amoja simkubli huyo Magufuli.
 
Halafu wanataka sisi ambao hatukupata hata uteuzi wa balozi nyumba kumi ndio Tumsifie.
Walipanda baiskeli ya miwa sasa kiu imewakamata wameanza kula spoke, watasema yote bila kuulizwa usicheze na njaa.

Dogo alipewa ulaji akaoa fasta sasa mke kumlisha inataka uanaume kwelikweli, ndio akaze mdhuti amkane kayafa asifie Hangaya.

Alichapa bakora wazazi wa wanafunzi waliyofanya fujo shuleni as if wazazi ndio waliwatuma hao watoto na akawalipisha faini juu.

Baniani mbaya kiatu chake dawa.
 
Back
Top Bottom