Wenye mamlaka ya kusema Fatuma alikuwa amevaa hijab ya Kiislam au vinginevyo, kisheria, kwa Tanzania, ni BAKWATA.
BAKWATA wamesema Fatuma alikuwa amevaa, na akavuliwa, hijabu. Lakini wamekosolewa kwamba mvaa hijabu alikuwa Mkatoliki. Ikawa mada yetu hapa, kwamba mvaa hijab kumbe alikuwa Mkatoliki.
Nikasema, ukimvua Mwanamke hijab, Mkatoliki au M-Sunni, umedhalilisha alama ya Uislam, Uislam wote, na Waislam, hali kadhalika umenyanyasa faragha ya Mwanamke. Hata kama aliyekuwa amevaa hijab ya Kiislam ni Mkatoliki.
BAKWATA wamesimama kutetea tamko la sheria na Katiba ya Tanzania, inayomtaka kila raia kuheshimu dini za Wananchi wenzake, zikiwemo alama na nguzo za imani za dini hizo, japo Tanzania haina dini ya Taifa, au dini ya serikali, ambayo kila Mtanzania lazima aifuate.