Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,197
- 128,160
Unazungumzia heshima ya uislamu au ya uarabu?? Bakwata wamewazalilisha nyie baadhi ya waisilamu mnaosupport Bakwata na mama Joseph Kimario.Ukimvua mwanamke hijabu umemdhalilisha na umeudhalilisha Uislam hata ikitokea sio Muislam kwa sababu umeivunjia heshima alama ya Uislam na faragha ya mwanamke. BAKWATA wametetea heshima ya Uislam mbele ya jamii, hata kama Kimario mmoja kumbe sio Muislam.
Kwa hali kama hii ndo maana nkasema BAKWATA wameingizwa choo cha kike bila kujitambua!
Umejuaje mimi Muislam?Bakwata wamewazalilisha nyie baadhi ya waisilamu mnaosupport Bakwata
hiyo ndoa ya joseph na fatuma haina uhusiano na dini yake.....mama ni muislamu tena swala tano!hiyo haihitaji evidence ninamfahamu
Umejuaje mimi Muislam?
Nimesema, ukimvua Mwanamke hijab umedhalilisha alama ya Uislam na umemnyanyasa mwanamke, hata kama itakuja kugundulika kwamba aliyevaa vazi hilo si Muislam.
Kama ambavyo, kwa mfano, ukimkuta mtu amebeba Biblia, ukampokonya ukaikanyaga, umedhalilisha nguzo na alama ya Ukristo na Wakristo, hata kama itaja gundulika baadae kwamba aliyekuwa amebeba biblia ile si Mkristo.
Una upeo wewe wa kujibu hiyo hoja rahisi bila kukimbilia kusema mimi ni Muislam?
Wenye mamlaka ya kusema Fatuma alikuwa amevaa hijab ya Kiislam au vinginevyo, kisheria, kwa Tanzania, ni BAKWATA.DC Fatuma alikua amevaa mtandio, na sio hijab....
Wajameni tuwe waangalifu kwenye jambo hili. Mwislamu kuolewa na mkristo hakummfanyi mwislamu kuwa automatically mkristo kwani hata huko kanisani zipo ndoa za mchanganyiko wa dini au madhehebu. Ili tuweze kuwa na uhakika kama kweli ni mkristo tulete vithibitisho kwamba alibatizwa (mahali, na mbatizaji wake) na jina lake la ubatizo. Kwa kifupi tutafute cheti chake cha ubatizo au watu wanaomjua fika kwamba ni mkristo na jina lake linafahamika. siyo hizi ngonjera za kusema kaolewa na mkatoliki kwa hiyo naye ni mkatoliki.
Hii wala haina tatizo.Chadema hakuna pa kutokea kuhusiana na uhasama baina yenu na waislamu.Fursa ya kuomba radhi kwa kumsikiliza yule mroho wa madaraka-Safari mumeshindwa kuitumia.
Bakwata tunaamini kama kweli Fatma si muislamu mwenzetu na sisi tulikuwa hatujui hilo,basi na wale waliomvua hijabu mama Fatuma hawakujuwa kwamba ni mkatoliki mwenzao,walidhani ni muislamu.Hivyo tatizo liko pale pale kwamba nia ya Chadema ilikuwa kudharau uislamu na kubeza alama zake.
Kuanzia sasa hatumzungumzii Fatuma bali tunazugumzia hijabu.
Kwa upande mwengine hiki kisa iwapo ni kweli kinaweza kikatoa ushahidi mzito juu ya kitu kinachoitwa mfumo kristo.
Umejuaje mimi Muislam?
Nimesema, ukimvua Mwanamke hijab umedhalilisha alama ya Uislam na umemnyanyasa mwanamke, hata kama itakuja kugundulika kwamba aliyevaa vazi hilo si Muislam.
Kama ambavyo, kwa mfano, ukimkuta mtu amebeba Biblia, ukampokonya ukaikanyaga, umedhalilisha nguzo na alama ya Ukristo na Wakristo, hata kama itaja gundulika baadae kwamba aliyekuwa amebeba biblia ile si Mkristo.
Una upeo wewe wa kujibu hiyo hoja rahisi bila kukimbilia kusema mimi ni Muislam?
Wenye mamlaka ya kusema Fatuma alikuwa amevaa hijab ya Kiislam au vinginevyo, kisheria, kwa Tanzania, ni BAKWATA.
BAKWATA wamesema Fatuma alikuwa amevaa, na akavuliwa, hijabu. Lakini wamekosolewa kwamba mvaa hijabu alikuwa Mkatoliki. Ikawa mada yetu hapa, kwamba mvaa hijab kumbe alikuwa Mkatoliki.
Nikasema, ukimvua Mwanamke hijab, Mkatoliki au M-Sunni, umedhalilisha alama ya Uislam, Uislam wote, na Waislam, hali kadhalika umenyanyasa faragha ya Mwanamke. Hata kama aliyekuwa amevaa hijab ya Kiislam ni Mkatoliki.
BAKWATA wamesimama kutetea tamko la sheria na Katiba ya Tanzania, inayomtaka kila raia kuheshimu dini za Wananchi wenzake, zikiwemo alama na nguzo za imani za dini hizo, japo Tanzania haina dini ya Taifa, au dini ya serikali, ambayo kila Mtanzania lazima aifuate.
Sasa mnazungumzia hijabu ya nani kama sio Fatuma?... Kuanzia sasa hatumzungumzii Fatuma bali tunazugumzia hijabu.
...
Si kila mwenye koti jeupe ni daktari, wengine wauza nyama buchani.