PostGE2025 DC Ilala ahimiza ujenzi upya wa Ofisi zilizoharibiwa wakati wa Vurugu Oktoba 29

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewataka watumishi wa umma katika wilaya hiyo kuendelea kutoa huduma kwa wananchi licha ya changamoto zilizojitokeza baada ya baadhi ya ofisi zao kuharibiwa.

Akizungumza wakati wa kufanya tathmini ya maeneo yaliyoharibiwa, Mpogolo alisema kuwa Serikali, kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, imeanza mchakato wa kufanya tathmini ya kina ili kuhakikisha kuwa ofisi zote zilizoharibiwa zinajengwa upya au kukarabatiwa kwa haraka.

Aidha, aliwataka wakandarasi watakaopewa kazi ya kujenga upya ofisi hizo kuwa waaminifu na kufuata masharti ya mikataba watakayowekewa, ili kuhakikisha kuwa fedha za umma zinatumika ipasavyo.

Akihitimisha, Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka watumishi wa umma wa Ilala kuendelea kuwa na moyo wa uzalendo na kujituma katika kuhudumia wananchi, akisisitiza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi bila vikwazo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndugu Elihuruma Mabelya amemhakikishia Mkuu wa Wilaya kuwa maagizo yote yaliyotolewa na serikali yatatekelezwa ipasavyo, na kwamba watumishi wako tayari kuhakikisha huduma kwa wananchi zinatolewa kwa ari kubwa sana na kufikia malengo

1762941724207.png

1762941799179.png

1762941773535.png

1762941831562.png
 
Nawashauri wasijenge kwa sasa.

Wasubiri mpka uchaguzi mpya utakapoitishwa na Rais halali atakapopatikana.
 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewataka watumishi wa umma katika wilaya hiyo kuendelea kutoa huduma kwa wananchi licha ya changamoto zilizojitokeza baada ya baadhi ya ofisi zao kuharibiwa.

Akizungumza wakati wa kufanya tathmini ya maeneo yaliyoharibiwa, Mpogolo alisema kuwa Serikali, kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, imeanza mchakato wa kufanya tathmini ya kina ili kuhakikisha kuwa ofisi zote zilizoharibiwa zinajengwa upya au kukarabatiwa kwa haraka.

Aidha, aliwataka wakandarasi watakaopewa kazi ya kujenga upya ofisi hizo kuwa waaminifu na kufuata masharti ya mikataba watakayowekewa, ili kuhakikisha kuwa fedha za umma zinatumika ipasavyo.

Akihitimisha, Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka watumishi wa umma wa Ilala kuendelea kuwa na moyo wa uzalendo na kujituma katika kuhudumia wananchi, akisisitiza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi bila vikwazo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Ndugu Elihuruma Mabelya amemhakikishia Mkuu wa Wilaya kuwa maagizo yote yaliyotolewa na serikali yatatekelezwa ipasavyo, na kwamba watumishi wako tayari kuhakikisha huduma kwa wananchi zinatolewa kwa ari kubwa sana na kufikia malengo

Duuuh! Kumbeee, nikajua ni panya road walikuwa wanaiba.. hahahaha
 
Back
Top Bottom