DC Jerry Muro amfokea DED kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 kwenye msafara

DC Jerry Muro amfokea DED kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 kwenye msafara

Wala usohangaike huyo mla rushwa Jerry kapewa wilaya kwa sababu aliyemteuwa ni kichaa na usalama wataifa wamekuwa malaya w kisiasa na kujali matumbo yao utawala mwingine jerry angekuwa ndani
 
That is not how we are supposed to serve.

Kama mwanachama mtiifu wa CCM ambayo inajukumu la kuisimamia Serikali.

Naomba mheshimiwa D.C. aonywe na mamlaka ya uteuzi.
Atleast mmoja wenu umejitambua..! Hii sio sahihi kabisa
 
Msomi kama huyu anakubali kudhalilishwa na 'msaka tonge'! aisee nami ningemjia juu tena kwa sana hadi aone cha moto! mie ni mteule wa raisi kama yeye! kama vipi nirudi zangu chuoni!
Jerry asingeshindwa kumpa 48 hours
 
Hivi ni kwa nini wananchi wasielimishwe kuwakataa hawa wanyapara wa rais. Kama tulipinga utwana na utumwa wa mkoloni mweupe tunashindwa je huyu mkoloni mweusi?
Cha msingi hapa katika hawa ma Dc na ma Rc ni raia kujiunga na kutotambua mamlaka zao. Asiyethamini utu nae automatically amejiondoa kutambulika kisheria. Ma Dc wa mfano wa Jerry ni wapuuzi tu waliojipuuza tayari. Wasipewe ushirikiano wowote
 
Huyu DC anapata wapi nguvu na mamlaka ya kumdharau DED tena mbele ya public ..Jerry kielimu na kiumri hawalingani na mahola ..

Angeshimu hata umri wake kama anadharau mamlaka yake. Nasema hivi Jerry huku hakumfai bora arudi yanga kupambana na Haji Manara
 
Natumaini Mhe. Rais ameona hiyo clip. Katika dhana ya Utawala Bora kitendo kama hicho hakivumiliki hata kidogo. Tena DED ni mtu mwenye PhD ni mtu wa kuheshimiwa.
 
Ndugu wanajamvi nadhani ninalo lisema inawezekana lisieleweke vyema ila kwa ufupi nimezunguka mikoa mingi kidgo tangu uongozi huu uingie madarakani na Mh rais chini ya ushauri wa watu wake afanye uteuzi wa wakuu wa mikoa na wilaya na wakurugenzi aise ndgu zangu kama una ndgu ni mkuu wa mkoa kidgo afadhali ila kuna vita kubwa sanaaa inaendelea uko maofisini yani

VITA KATI YA WAKURUGENZI NA WAKUU WA WILAYA NI KUBWA WOTE YANI HAWAPENDANI WANAWINDANA KILA MMOJA ANAMWOFIA MWENZIE KILA MTU ANAMWOFIA MWENZAKE!

MFANO mzuri ni kati ya Jerry muro na mwenzake utaona kabsaaa rais wa mkoa yupo pembenei hao wateule wanalaluana tu hapo! Hii tafsiri yake ni kuwa wanautafta ukuu wa mkoa

Binafsi sina shida na Jerry Muro maana nakumbuka aliwai tabiliwa na mwalimu Mmoja miaka mingi tukiwa chuo kikuu cha Tumaini mwalimu ambae siwezi mficha jona lake tulimtambua kwa jina la Mwendamseke tafadhali huyu mama alisema kbsaa JERRY MURO HAFAI NA HANA UWEZO WA KUWA KIONGOZI BORA.
ushauri wangu kwa jafo tafadhal watu hawa watenganishe ndo watafanya kazi vinginevyo ipo siku watazichapa ofisini!.View attachment VID-20180906-WA0005.mp4
 
Hizi takataka sijui zinaokotwa wapi halafu zinapewa wadhifa

Kitu kizuri kafanya mbele ya Gambo ambaye Ki protokali ni mkubwa wake na Gambo ni mzee wa Fitna soon habari zake zitamfikia Magufuli ,Gambo alikuwa na ugomvi gani sijui na katibu wa ccm Arusha ..Matokeo yake katibu kahamishwa Mara huko
 
Mh.Jerry Muro hebu kuwa na heshima kwa viongozi wenzako huwezi kumwita Mkurugenzi eti Mpuuzi sio busara hata kidogo
 
Inasikitisha sema Elimu ni kitu cha msingi sana kwenye nyadhifa hizi za uongozi kigezo cha upiga debe tuu na mfia chama hapana jamaa amewadharirisha vijana lakini kama TFF walimfungia hafai kuwa msemaji wa Club ya Yanga anapewa ukuu wa wilaya kweli?
 
Na Malisa GJ


Mkuu wa Wilaya Jerry Muro anamtukana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha DC, Dr.Wilson Mahela (PhD) mbele ya Mkuu wa mkoa na macamera ya waandishi wa habari yanawamulika. Uongozi wa kijinga sana huu. Kanuni za maadili ya uongozi haziruhusu kufanya huu utoto. Kama Mkurugenzi alichelewa kufika, kuna namna bora ya kumuwajibisha ambayo ingekua na tija kuliko huu ujinga uliofanya Jerry. Tatizo mnateuliwa teuliwa tu bila hata kupewa semina elekezi.

Mtu hajawahi kuwa hata CR darasani leo anakuwa DC ama RC what do u expect? Matokeo yake ndio haya ya kuja kutukanana hadharani na mnaona sifa kurekodiwa. Halafu wewe Jerry sio mamlaka ya nidhamu ya DED. Pengine huo uDC umekulevya. Mamlaka ya nidhamu ya DED ni RAS. Kwahiyo kama alichelewa ungeweza kuzungumza nae baadae na kumueleza masikitiko yako, na kama angekaidi ungemripoti kwa RAS. Sio kutukanana hadharani.

Unamtukana DED na kumuita mpuuzi na mpumbavu hadharani, halafu unategemea awasimamie watendaji wa Halmashauri. How that possible? Atawasimamiaje wakati wameona akiitwa mpuuzi na mpumbavu hadharani? Na wenyewe watampuuza tu kama ulivyompuuza wewe. Ni aibu viongozi kuzozana hadharani. Wahenga walisema wazazi wapumbavu pekee ndio wanaoweza kugombana mbele ya watoto. Kulikua na tatizo gani mngeendelea na hiyo ziara then badae mkae na kujadili?

Halafu kichekesho unamlaumu DED kwa kuchelewa dakika 10, lakini wewe umepoteza dakika nyingi zaidi kumtukana. Hivi lengo lako lilikua kuokoa muda kweli?

Huyu Dr.Wilson Mahela ni PhD holder. Amefundisha chuo kikuu UDSM muda mrefu wakati wewe ukifanya ukanjanja kwenye media. Amekuzidi umri, amekuzidi elimu, amekuzidi busara. Kama umeshindwa kumheshimu kwa nafasi yake basi ungemheshimu hata kwa umri wake tu.

Then huyo DED unayemdhalilisha ndo anayekuweka mjini. Tunajua maDC hamna budget. Mnalelewa na ofisi za DED kwa kila kitu. Hadi mafuta ya gari mnaomba kwao. Sasa how comes unamdhalilisha mtu anayekufanya usurvive? Kesho ukimuomba mafuta akikunyima utamfanya nini? Au ndo utaita tena macamera uanze kumtukana? Growup na uache sifa za kijinga. Uongozi ni kujifunza. Take time to learn from your elders kabla ya kukurupuka. Unajidhalilisha na kumdhalilisha aliyekuteua.!
UMENENA VEMA, ILA SAHIHISHO DOGO
MAMLAKA YA NIDHAMU YA DED ZAMANI ILIKUA WAZIRI WA TAMISEMI ILA SASA HIVI BAADA YA AWAMU HII NI MKUU WA KAYA MWENYEWE (PREZDA)
 
Kwa hiyo issue ni msafara naona Jamaa alidramatize usiku kucha aonje convoy ikabuma .jamaa hafai hata kuwa kiranja
 
Inasikitisha sema Elimu ni kitu cha msingi sana kwenye nyadhifa hizi za uongozi kigezo cha upiga debe tuu na mfia chama hapana jamaa amewadharirisha vijana lakini kama TFF walimfungia hafai kuwa msemaji wa Club ya Yanga anapewa ukuu wa wilaya kweli?
Hili nalo ni neno
 
Vyieo vya kisisa ni vyeo vya kijinga sana DC anafokea mkurugenzi ni only in Afrika tena Tanzania
 
DC mpya wa Arumeru, Jerry leo ameonekana kwenye video fupi akimfokea mkurugenzi wa manispaa kama mtoto mdogo kwa kuchelewa dakika 10 tu, tukio hilo limetokea mbele ya RC ( Gambo ) na baadhi ya viongozi wa Arusha, huku Gambo akionesha dhahiri kutofurahiswa na tukio lile



Huu ndio mfano wa maudhui wa kale kawimbo kanakoitwa 'Madaraka ya Kukevya'

Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo. Baada ya ile kauli ya King Kong juzi kule Ukerewe niliamini kabisa kifuatacho kinafurahisha. Hili analilifanya bwana Muro ni uhalisia wa aliyemteua maana boss kubwa (Jiwe) ni Kioo yeye (Muro &the co.) wanajitazama tu.

Kwani, malezi bora kwa mtoto yanaanza kwa mifano, watoto wanatakiwa kuelewa mifano, mtoto anakuwa mwepesi sana kufuatisha unachofanya kuliko unachomuambia. Muro na wenzake wa kaliba yake wala hawawezi kutenguliwa sanasana watapandishwa vyeo, yuko wapi Mnyeti??
 
Back
Top Bottom