Mkuu nimeona umezungumza maoni yako ambayo kiasi kikubwa uko sahihi, Ila kabla ya kumdhalilisha mtu kwenye umma lazima uwe na uhakika wa kile kilichomfanya yeye kuchelewa hapo alipo.Labda kwa kuzungumza ukweli ninaoufahamu juu ya tukio kwa sababu mimi naishi na huyu mkurugenzi kwake ila pia siwezi kuzungumza kwa kutetea upande wowote lakini nitazungumza namna stori ilivyokuwa na dr alivyofika nyumbani alivyotuambia nini kilitokea kabla ya kuenea mitandaoni.Ilikuwa ni juzi siku ya Jumanne usiku wakati mkurugenzi anarudi nyumbani alitukuta tumekaa sebuleni tunaangalia filamu ya marehemu Steven Kanumba dar 2 lagos chanel ya St swahili, alivyofika baada ya kumsalimia alikuwa tofauti na tulivyomzoea yaani hakuwa na furaha kuna simu ikawa imeingia ya kiongozi mmoja hivi wa serikali akamuuliza mkutano wenu umeendaje, akwambia haukuwa vizuri kulikuwa na tatizo baada ya kusikia hivyo ilibidi kupunguza sauti ya tv ili kusikiliza kilichotokea baada ya kuongea na simu akaanza kutuelezea ilivyokuwa.
Kwa kifupi ilikuwa hivi...... Asubuhi ya Jumanne viongozi hawa yaani Dc, Rc, Rpc, Ded na wengine walikuwa wamepanga kwenda ziara nahisi ilikuwa Arumeru hivyo wakati wanajiandaa kuondoka pale ofisini Mkurugenzi akawa amesahau baadhi ya documents ofisini hivyo akaomba kuzichukua haraka ili waondoke wakati anachukua documents hizo, akatoka nje akakuta msafara umeshaondoka ikiwepo gari ya King'ora ambayo hufanya gari na watu barabarani kupisha msafara hivyo basi akapanda kwenye gari lake na kuondoka ili kuwahi,Hivyo basi kutoka ofisini Sekei hadi kwenye mkutano Arumeru kulikuwa na foleni sana njiani pia Magari na watu hawa kupisha gari ya Mkurugenzi kwa sababu hakukuwa na gari ya king'ora kuonesha kuwa anawahi sehemu.
Baada ya purukushani hizo Mkurugenzi alifanikiwa kufika akiwa amechelewa kati ya dakika tano hadi kumi kwa hiyo kabla hajaeleza kitu chochote ndio akakutana na fedheha ya namna hii.Hivyo basi ningependa kushauri mtu yoyote kabla ya kutoa hukumu au kumuona mtu .. amekosea ni bora kwanza kusikiliza nini kimesababisha tatizo. kwa hiyo kwa tukio hili la Jumanne mheshimiwa Jerry Muro alikuwa akijua kabisa mkurugenzi amechelewa kwa sababu walimuacha bila kumpa taarifa wakati walikuwa pamoja na alikuwa anachukua documents ambazo ni mhimu kwa ajili ya mkutano wa siku ile hivyo inaweza kuwa Dc alifanya hivyo aidha kwa kupanga au bila kufikiria.