cocastic
JF-Expert Member
- Nov 30, 2019
- 96,456
- 156,324
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kuna watu wanajikuta wakereketwa sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kuna watu wanajikuta wakereketwa sana
Utalipa tu, upende usipende, ukigoma jiandae kuingia 'lindo'.Kama mmeamua kuwa wanga basi kawangeni tu
Hela sitoi na hakuna wa kunifanya chochote maana mimi siyo polisi wala sungusungu.
Tangu umezaliwa hadi umefika hapo ramli zimekusaidia nini maishani?Utalipa tu, upende usipende, ukigoma jiandae kuingia 'lindo'.
Nyie mnaopinga hili ndio wafadhili wa 'panya road' mnaogopa mtaumbuka.
Kama ni lazima itabidi walipwe mishahara kima cha chiniDC. Jokate Mwegelo: Ametoa siku saba kwa wenyeviti wa serikali za mitaa kuunda Vikundi vya Ulinzi Shirikishi katika Mitaa yao.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Temeke Mhe.Jokate Mwegelo ametoa siku saba kwa wenyeviti wa serikali za mitaa wilayani humo kuhakikisha wanaunda vikundi vya ulinzi shirikishi.
Agizo hilo amelitoa leo Aprili 29,2022 alipokuwa akizungumza na wenyeviti hao katika ukumbi wa Iddi Nyundo uliopo katika Manispaa hiyo.
Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya hiyo amewataka viongozi hao kuhakikisha suala la ulinzi na usalama linapewa kipaumbele ili kuwezesha wananchi kuishi kwa usalama.
"Ninatoa siku 7 muhakikishe kule ambapo hakuna vikundi vya ulinzi shirikishi mnaanzisha vikundi hivyo na kule ambapo vilikuwepo ila vinalegalega mviimarishe".Alisema Mhe.Jokate
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam,Muliro Jumanne Muliro amesema kuwa uhalifu unatokea pale ambapo hakuna ulinzi na kusisitiza kuwa suala la ulinzi ni jukumu la kila raia.
"Ili uhalifu utokee lazima kuwepo na fursa,na fursa ni pale ambapo hakuna ulinzi kwa kile ambacho mhalifu anachokusudia kufanya".Alisema Afande Muliro.
Kikao hicho ambacho kilihusisha kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya,wenyeviti wa serikali za mitaa pamoja na baadhi ya vikundi vya ulinzi shirikishi kilikuwa na lengo la kuweka mikakati ya jinsi ya kukabiliana na wimbi la vitendo vya uhalifu ambavyo vimeanza kujitokeza kwa siku hizi za karibuni.
View attachment 2205003
View attachment 2205004
View attachment 2205005
View attachment 2205006
View attachment 2205007
View attachment 2205008
...Ramli ndio nini ?Tangu umezaliwa hadi umefika hapo ramli zimekusaidia nini maishani?