JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Wameeleza kuwa wamefikisha malalamiko yao mara nyingi kuhusu mgogoro wa ardhi lakini hatua zinazochukuliwa ni zile ambazo zinakandamiza Wananchi.
Wakizungumza katika Mkutano wa Hadhara ulioongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Remidius Mwema wamedai kuwa hata mgogoro unaohusisha Hifadhi ya Indema WMA ambayo pia imekuwa ikijiita MAKAME WMA umetokana na baadhi ya viongozi wa Halmashauri kutotenda haki dhidi ya Wananchi wa kawaida.
Julius Tajiri, ambaye ni Mkulima amesema “Moja ya michezo inayofanywa na Viongozi wa Halmashauri ni kuwa kukitokea mgogoro wa ardhi, wanaomba Hati ya mwananchi, wakiiona wanatengeneza nyaraka nyingine za kuonesha huyo wanayemtetea alipewa nyuma ya yule aliyewaonesha Hati.
Ameongeza kuwa baadhi ya viongozi wamefanya migogoro kama njia ya kujiingizia maslahi kwao.
Joseph Michael, Mkazi wa Kijiji cha Ndaleta naye amesema Viongozi wa Halmashauri wanaelewa kinachoendelea lakini wanakwepa kutoa maelezo sahihi.
Akizungumza migogoro inayoendelea, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Remidius Mwema amesema “Nitaenda maeneo yenye changamoto ikiwemo lile lenye mgogoro wa Hifadhi ya WMA pamoja na Wanakijiji kujionea mwenyewe, nijue ninapofanya uamuzi wa kutamka tuwe na uhakika wa tunachokizungumza
Hata Rais akiniuliza kama nimefika maeneo husika niwe na majibu nisikune kichwa, tukibaini kuwa kuna makosa yalifanyika, watu wamechukuliwa maeneo yao na maeneo mengine yalikuwa mashamba ya Watu utaratibu wa kufidia utafanyika.
“Serikali haiwezi kumnyonya mtu yeyote Haki yake ya msingi, pia ispobainika tuwe tayari kuyakubali majibu hayo, naombeni mnipe nafasi, mwezi mmoja kuanzia leo tutakutana hapa, nitakuja kutoa maamuzi.”
Chanzo: EATV
Pia soma:
~ Wakulima 27 Wilayani Kiteto washikiliwa na Polisi kutokana na mgogoro wa Ardhi
~ Manyara: Wakulima Kiteto warejea kwenye mashamba waliyoondolewa, watuma ujumbe kwa Rais Samia wakidai wameporwa Ardhi yenye mashamba yao
~ Polisi Kiteto wamekamata Wakulima, wanawatesa na kuwanyima dhamana