Pre GE2025 DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
dah? Allah atuhifadhi. Mimi nashangaa sana mtu kutumia mbinu chafu kuiba kura au lolote ili ashinde ili iwe nini?nani kaishi kaishi katika dunia hii milele? hata ukiiba kura au kudhulumu nini kitasaidia? Kama utafurahi ni muda mchache sana lkn majuta yaankuwa makunbwa mbele . kikubwa Ukifa utaenda kusema nini kwa muumba wako? Allah aniepushe na mambo kama haya, nisaysikie tu kupitia media lkn nisiyakiribie kabisa ktk maisha yangu - Aaamin
 
DC mstafu wa Longido, bwana Ng'umbi kasema tayari washakamilisha na kuchakata maandalizili ya chaguzi kuanzia vijiji hadi kwenye kata kwahyo matokea wanayo teyari.

Ushauri wangu kwakua watanzania wachache wapo busy na Yanga na Simba ,ila vyama vya siasa na wapenda demokrasia wapo chagueni yafuatayo.

(1) Kufanya maandamano yasiyo na kikomo mpaka tume huru ipatikane au sheria mpya ya tume huru itumike

(II) Kupinga TAMISEM kutosimamia uchaguzi tena kwa njia ya maandamano na siyo kwenda mahakamani, kwakua mahakama zimeshapewa maelekezo sababu ata kesi mliyofungua haitakuwa na maana.

(III) Kutoshiriki uchaguzi kabisa
NB: Maandamano yawe ya amani ambapo vyama vyote vishiriki na wanaharakati siyo kuishia kutoa matamko ambayo hayana faida na hayajawahi kusikirizwa, pazeni sauti zaidi
 
Kwa wananchi. Inaonyesha hawaogopi wananchi na wako tayari kusema wanaiba kwa sababu wanajua sisi wananchi ni matutusa. Haiwezi kuwa dharau kwa serikali kwa sababu wao siku zote ni wezi na wako pale kula na kustarehe.
Siyo kweli serikali ipo kwaajili ya kula na kustarehe.
 
Mungu fundi nyie
Hakuna siri chini ya juu
Mwamba katoa siri za jandoni
 
Kikubwa ambacho WAPINZANI wanatakiwa wafahamu ni kwamba KATIBA MPYA BORA na TUME HURU YA UCHAGUZI havitopatikana kwa URAHISI..ni lazima wawe na MIKAKATI mizito na waweke pembeni MASLAHI ya muda mfupi...Gharama zake ni KUBWA ila INAWEZEKANA!
 
Swali langu ni Moja tu
Je aliongea uongo?
 
Bila DC, DED na DSO sidhani kama Kuna Diwani wa ccm anaweza kushinda. Hata DC kasema ukweli kama ulivyo.
At least kipindi Cha JK kulikua narudia at least kulikua na TRUE & FAIR ELECTION ndio maana hata wapinzani walipata nafasi
 

Amesema ukweli lakini Rais amemuonea kumtoa angelimuonya asiseme Siri za Serikali yake kuchakachukuwa kura za Wananchi. Kama Kuna usimamiz wa Kura kutoka nje CCM haiwezi kushinda hata katika Uchaguzi wa Madiwani siuze Uchaguzi Mkuu wa Rais. CCM Wanaiba kura za Wananchi na kuamuwa kumchaguwa Wanaye mtaka awe Kiongozi wao lakini sio Uchaguzi wa Wananchi wenyewe.




Your browser is not able to display this video.
 
Huyu kasema wazi alichofanya maporini , kiburi na ujinga vina gharama kubwa
 
Hilo sio kosa la kumuonya, huyu ni jela kufukuza haitoshi, Kaua maporini inawezekana
 
Hivi vijana wa siku hizi tunafanya nini kuiacha CCM madarakani!
 
Kwa nini ametenguliwa!? Kama ni kwa sababu ya kauli yake juu ya uchaguzi 2020, hapo ni wazi ameonewa, kwani aliyazungumza hayo kwenye vikao vya ndani vya makada wenziwe wa ccm. Na alikuwa anaongea ukweli. Kesho ikivuja taarifa ya kada mwingine ndani ya mikutano yao ya ndani itafanyiwa Kazi!?
 



Your browser is not able to display this video.



 
DC amesema kile ambacho huwa wanafanya na ambacho wamejiandaa kufanya. Na ukisikiliza kwa makini wote waliopo hapo ni Madiwani wa CCM hivyo alijua ni kama kikao cha ndani tu. Kuna MCCM hapo kachoma utambi.
Jamaa kaonewa pakubwa. Je, kesho ikivuja taarifa nyingine ya kiongozi mkubwa wa ccm, au hata yake yeye Samia, atachukua hatua!? Hapa ni unafiki umefanyika, ila jamaa hana kosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…