Pre GE2025 DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!

Pre GE2025 DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Alitumwa na serikali kuua Wapinzani ili wapite bila kupingwa, Iko hivi, January, Nape,Riziwani na Kasimu Majaliwa walipita bila Kupingwa huku wagombea wa upinzani wakikamatwa ama kuokotwa kwenye mapori ya Mkurunga, Kwa Mfano, Mgombea wa Chadema Mtama aliyeitwa Suleiman Mathew alikamatwa kwenye ofisi ya Ded akirejesha fomu ya kugombea Ubunge, akapewa kesi ya uongo ya Uhujumu Uchumi, Mgombea wa upinzani Jimbo la Rwangwa aliokotwa Mkuranga akiwa nusu Maiti, hili ni Jimbo la Kasimu Majaliwa.

Haya Mambo yalifanywa Mchana kabisa huku kila mtu akiona kwa macho.

Mwingine ambaye baadaye atakamatwa na kushitakiwa ni Abood wa Morogoro, huyu pia aliteka Wagombea wa Upinzani akiwemo Mgombea wa Chadema

Mnyororo ni mrefu mno na nakuhakikishia kwamba siku zijazo watakamatwa na kushitakiwa, Ushahidi umejaa tele, hakutakuwa na Mswalie Mtume, Usalama wao ni Kufa kabla ya Kukamatwa, lakini wakiwa Hai watakamatwa hata wakiwa kwenye Wheel Chair
Kisasi siyo!
 
Siamini kama haya maneno yanatoka kinywani mwa kiongozi mkubwa.

Naomba tumsikilize kwa makini anavyo wadharau wapiga kura na anavyo jimwambafai kushiriki kwenye uchaguzi wa 2020.

Kama viongozi wetu wapo hivi sioni kama uadilifu unaoimbwa na wenzake utakuja kutimia.

Asante sana CCM, idumu.

"Na mimi naomba niwahakikishie, mimi niko very tough, kama kuna mtu ambaye siyo mwoga ni mimi! Wote hapa madiwani mwaka 2020 hayuko diwani aliyepiga kampeni hapa nyumba kwa nyumba, hakuna!

"Sasa yale mazingira ya mwaka 2020 siyo kwamba yalikuja yenyewe automatically kwasababu ninyi mlikuwa wagombea bora sana, ni mazingira ambayo yalikuwa, yametengenezwa na serikali ndio iliyofanya kazi ile ya wewe kupita bila kupingwa.

"Na kuna watu mnafahamu kilichotokea kwenye mapori huko na sehemu zingine na mimi nilihusika kwenye majimbo fulani fulani, sasa mazingira yale ni serikali ndiyo iliyofanya ile kazi, diwani huna ujanja wowote kwenye kata yako ya kwamba utashinda bila serikali, HAKUNA.

"Na usije ukajidanganya ndio maana sisi sasa hivi tumeshafanya kazi huko kubwa sana, ya kuchakata huko kwenye kata, vijiji, vitongoji vyote, taarifa zile zote tunazo, hali ya mambo jinsi ilivyo, tunaendaje.."



Pia soma:

Serikali inapojivua nguo hadharani.
Kwanza Nape, pili Ng'umbi wamejitokeza kukiri uhalifu wa serikali hadharani.
This is shocking!!!!!
 
DC mstafu wa Longido, bwana NG,umbi kasema teyari washakamilisha na kuchakata maandalizili ya chaguzi kuanzia vijiji hadi kwenye kata kwahyo matokea wanayo teyari.
Ushauri wangu kwakua watanzania wachache wapo busy na Yanga na Simba ,ila vyama vya siasa na wapenda demokrasia wapo chagueni yafuatayo.
(1)Kufanya maandamano yasiyo na kikomo mpaka tume huru ipatikane au sheria mpya ya tume huru itumike
(II)Kupinga TAMISEM kutosimamia uchaguzi tena kwa njia ya maandamano na siyo kwenda mahakamani, kwakua mahakama zimeshapewa maelekezo sababu ata kesi mliyofungua haitakuwa na maana.
(III)Kutoshiriki uchaguzi kabisa
NB: Maandamano yawe ya amani ambapo vyama vyote vishiriki na wanaharakati siyo kuishia kutoa matamko ambayo hayana faida na hayajawahi kusikirizwa, pazeni sauti zaidi
Dawa ni migomo maandamano mpaka kieleweke.
 
Oooohh kumbe ndio maana Msigwa mkamnyima Uenyekiti wa Kanda sababu hana hela kumzidi Sugu 😂😂😂

Ndo maana tajiri Mbowe chama haachii kwa maskini akina Lissu na Heche!!
Msigwa si tayari anaenda kumrithi DC Longido. Mshahara wake huo.
 
Hii nchi viongozi wa kweli wako mitaaani,huko kwenye siasa wajaa wahuni tu
 
Hapo kama kawaida wagombea wa upinzani watatekwa wakati wa kurudisha form watahifadhiwa maporini hadi muda wa kurudisha form ukipita wataachiliwa huku wakiwa wameumizwa kwa vipigo.
 
Waongezewe posho , posho zao ziwe zinatoka serikali kuu, kila diwani posho yake iwe 1,000,000 per month. pia pension yao angalau iwe milioni 50. Pesa hii itokane na punguzo la posho za wabunge na mawaziri.
 
Toa full video tujiridhishe,sio tuvipande ungaunga halafu unataka tujaji
 
Wajinga bado mko wengi Huyo DC ni wa kupongezwa ni Shujaa wa kuusema Ukweli kama ulivyo
Kuna haja ya kuanzisha shule Ya kukuza uelewa Kwa viongozi wapuuzi kama huyu DC,anaongea ambayo mama hayataki,akiwemo ofisini kufikia kesho itakuwa ni doa Kwa serikali yetu.
 
Mi siamini kama Nape ametumbuliwa kwa sababu ya kauli yake aliyoitoa mjini Bukoba.
Kuna zaidi ya kauli ile.
Kauli ile ya Nape ndiyo msimamo wa kisiasa wa chama chake.
Chama chake ni Kama Mbuni kinajaribu kujificha kwenye Mchanga.
 
DC mstafu wa Longido, bwana NG,umbi kasema teyari washakamilisha na kuchakata maandalizili ya chaguzi kuanzia vijiji hadi kwenye kata kwahyo matokea wanayo teyari.
Ushauri wangu kwakua watanzania wachache wapo busy na Yanga na Simba ,ila vyama vya siasa na wapenda demokrasia wapo chagueni yafuatayo.
(1)Kufanya maandamano yasiyo na kikomo mpaka tume huru ipatikane au sheria mpya ya tume huru itumike
(II)Kupinga TAMISEM kutosimamia uchaguzi tena kwa njia ya maandamano na siyo kwenda mahakamani, kwakua mahakama zimeshapewa maelekezo sababu ata kesi mliyofungua haitakuwa na maana.
(III)Kutoshiriki uchaguzi kabisa
NB: Maandamano yawe ya amani ambapo vyama vyote vishiriki na wanaharakati siyo kuishia kutoa matamko ambayo hayana faida na hayajawahi kusikirizwa, pazeni sauti zaidi
Uchochezi!!!! mbona uchaguzi utakuwa huru wa haki na wa kuaminiwa.
 
Kikubwa ambacho WAPINZANI wanatakiwa wafahamu ni kwamba KATIBA MPYA BORA na TUME HURU YA UCHAGUZI havitopatikana kwa URAHISI..ni lazima wawe na MIKAKATI mizito na waweke pembeni MASLAHI ya muda mfupi...Gharama zake ni KUBWA ila INAWEZEKANA!
Wewe katiba mpya haikuhusu
 
Back
Top Bottom