Pre GE2025 DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!

Pre GE2025 DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwenye MAPORI alifanya nini ?!!

Awaeleze watanzania....alifanya nini huko maporini ?!!
Alitumwa na serikali kuua Wapinzani ili wapite bila kupingwa, Iko hivi, January, Nape,Riziwani na Kasimu Majaliwa walipita bila Kupingwa huku wagombea wa upinzani wakikamatwa ama kuokotwa kwenye mapori ya Mkurunga, Kwa Mfano, Mgombea wa Chadema Mtama aliyeitwa Suleiman Mathew alikamatwa kwenye ofisi ya Ded akirejesha fomu ya kugombea Ubunge, akapewa kesi ya uongo ya Uhujumu Uchumi, Mgombea wa upinzani Jimbo la Rwangwa aliokotwa Mkuranga akiwa nusu Maiti, hili ni Jimbo la Kasimu Majaliwa.

Haya Mambo yalifanywa Mchana kabisa huku kila mtu akiona kwa macho.

Mwingine ambaye baadaye atakamatwa na kushitakiwa ni Abood wa Morogoro, huyu pia aliteka Wagombea wa Upinzani akiwemo Mgombea wa Chadema

Mnyororo ni mrefu mno na nakuhakikishia kwamba siku zijazo watakamatwa na kushitakiwa, Ushahidi umejaa tele, hakutakuwa na Mswalie Mtume, Usalama wao ni Kufa kabla ya Kukamatwa, lakini wakiwa Hai watakamatwa hata wakiwa kwenye Wheel Chair
 
Siamini kama haya maneno yanatoka kinywani mwa kiongozi mkubwa.

Naomba tumsikilize kwa makini anavyo wadharau wapiga kura na anavyo jimwambafai kushiriki kwenye uchaguzi wa 2020.

Kama viongozi wetu wapo hivi sioni kama uadilifu unaoimbwa na wenzake utakuja kutimia.

Asante sana CCM, idumu.

"Na mimi naomba niwahakikishie, mimi niko very tough, kama kuna mtu ambaye siyo mwoga ni mimi! Wote hapa madiwani mwaka 2020 hayuko diwani aliyepiga kampeni hapa nyumba kwa nyumba, hakuna!

"Sasa yale mazingira ya mwaka 2020 siyo kwamba yalikuja yenyewe automatically kwasababu ninyi mlikuwa wagombea bora sana, ni mazingira ambayo yalikuwa, yametengenezwa na serikali ndio iliyofanya kazi ile ya wewe kupita bila kupingwa.

"Na kuna watu mnafahamu kilichotokea kwenye mapori huko na sehemu zingine na mimi nilihusika kwenye majimbo fulani fulani, sasa mazingira yale ni serikali ndiyo iliyofanya ile kazi, diwani huna ujanja wowote kwenye kata yako ya kwamba utashinda bila serikali, HAKUNA.

"Na usije ukajidanganya ndio maana sisi sasa hivi tumeshafanya kazi huko kubwa sana, ya kuchakata huko kwenye kata, vijiji, vitongoji vyote, taarifa zile zote tunazo, hali ya mambo jinsi ilivyo, tunaendaje.."


View attachment 3084265

Pia soma: Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!
Sasa huyu haogopi kumkuta yaliyowakuta wenzake Kwa kuzungumza uchaguzi in negative way,. Kwamba serikali inatumia njama Ili sisiem ishinde? Au ndio kama alivyosema sio mwoga
 
DC aweka mambo kweupe hadharani jinsi serikali ya chama dola kongwe kinavyovuruga chaguzi

1725201510623.png

Picha : MKUU WA WILAYA YA LONGIDO MHE. MARKO HENRY NG'UMBI
 
NITASEMA UKWELI DAIMA, FITINA KWANGU MWIKO


MKUU WA WILAYA LONGIDO AAPISHWA.

Posted on: January 31st, 2023 Mkuu wa Wilaya ya Longido nchini Tanzania, Mhe. Marko Henry Ng'umbi Leo tarehe 31/01/2023 amekula kiapo katika hafla fupi ya kuwaapisha wakuu wa Wilaya wateule wa Mkoa wa Arusha.

Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambapo wakuu wa Wilaya zote saba za Arusha, Arumeru na Longido wameapishwa na kula kiapo cha maadiili.

Mhe. Marko Henry Ng'umbi aliteuliwa kuwa DC kwa mara ya kwanza tarehe 25 January 2023 na mheshimiwa rais kama taarifa ya Ikulu :

Mkeka wa Wakuu wa Wilaya huu hapa​

Na Mwandishi Wetu January 25, 2023
raissss-780x470.jpg
Rais Samia Suluhu Hassan na mwenyekiti wa CCM Taifa.

Rais ameafanya uteuzi wa Wakuu wapya wa Wilaya 37.

Taarifa iliyotolewa leo Januari 25, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, bi. Zuhura Yunus.
 
Haya mambo ni mazito sana.

Mmoja wa wateule wa mwenyekiti wa CCM taifa aliye pia rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dr. Samia S. Hassan kiongozi wa maono ya 4R.

Huku ni kipindi cha lala salama kuelekea chaguzi za serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025 utakaoratibiwa kwa karibu na mwenyekiti wa kamati ya usalama wilaya mh. Marko Henry Ng'umbi kuhakikisha unakuwa uchaguzi wenye mchakato huru na wa haki hadi kutangazwa mshindi halali.
 
Hii kauli ya mkuu wa Wilaya ya Longido imeniogopesha sana

Niishie hapo 🐼

John the baptist kada mtiifu sasa umepewa za ndani kutoka kwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama jinsi dola inavyohusika katika kudumisha utawala kwa kutumia vitisho / terror, kupoteza watu, kujeruhi hata kuondoa haki ya uhai wa mtu nchini Tanzania.
1725203954565.png
 
Hawa Ndio watekaji wenyewe na watajisema wenyewe mmoja baada ya mwingine na hapo amesema ukweli bila kupepesa macho hiyo ndio KAZI za ma rc na madc wa miaka hii
 
Back
Top Bottom