Pre GE2025 DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!

Pre GE2025 DC Longido: Mazingira ya 2020 na yale yaliyofanyika kwenye mapori yalitengenezwa na serikali ili tupite bila kupingwa!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Siamini kama haya maneno yanatoka kinywani mwa kiongozi mkubwa.

Naomba tumsikilize kwa makini anavyo wadharau wapiga kura na anavyo jimwambafai kushiriki kwenye uchaguzi wa 2020.

Kama viongozi wetu wapo hivi sioni kama uadilifu unaoimbwa na wenzake utakuja kutimia.

Asante sana CCM, idumu.

"Na mimi naomba niwahakikishie, mimi niko very tough, kama kuna mtu ambaye siyo mwoga ni mimi! Wote hapa madiwani mwaka 2020 hayuko diwani aliyepiga kampeni hapa nyumba kwa nyumba, hakuna!

"Sasa yale mazingira ya mwaka 2020 siyo kwamba yalikuja yenyewe automatically kwasababu ninyi mlikuwa wagombea bora sana, ni mazingira ambayo yalikuwa, yametengenezwa na serikali ndio iliyofanya kazi ile ya wewe kupita bila kupingwa.

"Na kuna watu mnafahamu kilichotokea kwenye mapori huko na sehemu zingine na mimi nilihusika kwenye majimbo fulani fulani, sasa mazingira yale ni serikali ndiyo iliyofanya ile kazi, diwani huna ujanja wowote kwenye kata yako ya kwamba utashinda bila serikali, HAKUNA.

"Na usije ukajidanganya ndio maana sisi sasa hivi tumeshafanya kazi huko kubwa sana, ya kuchakata huko kwenye kata, vijiji, vitongoji vyote, taarifa zile zote tunazo, hali ya mambo jinsi ilivyo, tunaendaje.."


View attachment 3084265

Pia soma:

Kama msemaji anavyofafanua wameshachakata Taarifa zote vijiji na Kata inaonekana hali ya Mama sio nzuri😆😆
 
Ni ukweli kwa kila mtu.
Chaguzi zetu ni za ovyo sana.
Hatupati viongozi wanaopendwa na wananchi bali wanoopendwa na Tume.
Nyerere akifufuka ataweza lia.
Huyo nyerere ndio alikuwa anapenda mambk hayo. Itakuwa humjui vizuri wewe.
 
Naona watu mnakuwa wepesi sana kusahau kuwa Kuna albadiri ilisomwa mara baada ya Lissu kupigwa risasi kwa wana CCM.

Sasa mmesahau kuwa albadiri ni Sawa na criminal case huwa haina expire?
Nadhani!

Wasijulikana kujulikana by huduma ya kristo pia alitabiri hili jambo!
 
Nabik Jacob namkubali sana. Kila siku lazima nisikilize Yale ambayo Roho Wa Bwana ananena na kanisa.

Kila analosema naona likitimia siku hadi siku.

Nenda Youtube Google Huduma ya Kristo.
Ndio jamaa hana makuu!anaitendea haki huduma yake!

Yupo humu!!
 
Afukuzwe na aseheme alifanya nini kwenye mapori,huenda aliuua,poor Tanzania!!
Umeandika ili uone unajibiwa au umepitiwa kuandika kitu kama hiki?

Stuff wa serikali anapozungumza kitu akiweka ishu za mapori unadhani huko porini alikuwa anaenda kuwinda swala kama siyo kuuwa?
 
Mama hayataki au laana ya kutoa siri za mama na hayati mwendazake? Kwani uongo ccm mnateka na kupoteza watu?
Ni kweli.

Ingekuwa enzi za shujaa angeongezwa cheo.
Walau kidogo mama anausikivu
 
IMG-20240901-WA0016.jpg
 
Back
Top Bottom