DC Makala, hakikisha kuwa wamachinga wote hawarejei kwenye maeneo tena

RC Makala ni mwelewa sana kuliko unavyodhani. Anafahamu kuwa hakuna dhamira mbaya kwenye hili zaidi ya kujisahau
Mh.Makala ni bonge la RC....jamaa yuko "smart" sana upstairs👊

Kongole kwake mh.Rais SSH kwa kuliletea jiji mkuu huyu wa mkoa 💪👏

Siempre JMT
 
Hao watu wanasogeza huduma karibu zaidi kwa wananchi hasa wanyonge, unavunja vipi hadi magenge ya kuuza nyanya, vitunguu, matunda. Mnataka kila mtu akanunue nyanya na vitunguu mlimani city? Wanyonge watamudu kweli? manispaa wajipange namna watakavyowasimamia hao watu kwenye maeneo wanapofanyia shughuli zao, siyo kutumia ubabe tu kuwaondoa.
Hii inaonyesha kuwa hujawahi kutoka nje ya nchi hii, unadhani hivyo ndivyo inatakiwa iwe. HAPANa kaka sio kila mahali kunatakiwa kuuzwe nyanya kwenye meza, haiko hiyo duniani. Ukifanya hivyo huwezi kuzalisha walipakodi wakubwa, mtagawana umaskini kwenye kaya. Mipango miji ni muhimu sana
 
Waliotii agizo la serikali la kuondoka bila shuruti kwenye maeneo yasioruhusiwa kwa biashara wanavunjika moyo kuona wenzao waliovunjiwa panoja bado wanaendelea na biashara zao kwenye maeneo yaleyale waliyoyahama. Hii itasababisha yafuatayo:

1. Wanunuzi wasiende kwenye maeneo mapya kutafuta na kununua bidhaa.
2. Waliohama maeneo kukosa wateja na kipato.
3. Waliohama kupata sonona.
4. Waliohama kuwaza kurudi pia kwenye maeneo Yao.
5. Serikali kudharaulika kwa kukurupuka.
6. Kuonyesha kuwa Kuna mvutano ndani ya Chama na serikali na ndani ya Chama na ndani ya serikali.
7. Wamachinga kugombana kwa kulazimisha kurudi kwenye maeneo Yao yaleyale waliyokuwa kabla ya kuvujiwa au kuondoka. Bila shaka maeneo Yao watakuta yanatumiwa na wale amabao wamegoma kuondoka na hakuna wanachofanywa.

Hii ni hatari kubwa sana kwa kiongozi yeyoye anaetoa maagizo yasiyosimamiwa. Rais Magufuli alitufundisha kusimamia maamuzi yako hata kama ulikosea kuamua.
Heading ya uzi wako haujaeleweka. DC Makalla ndio yupi na yupo Wilaya gani? Au ulikuwa unamaanisha Mkuu wa Mkoa Dsm Amosi Makala?

Edit basi ueleweke acha kukurupuka ndugu. [emoji2][emoji2]
 
viongozi wa chama huko matawini ndio vinara wa kupora maeneo ya wazi, ndio maana walikuwa wanamchukia Bashiru na mwenyekiti wake kwa kudhibiti mali za chama. kama maRC hawatakuwa macho jitihada zao za kumuunga mkono Rais kwenye zoezi hili la usafi zitagonga mwamba. Hapa wanamjaribu Mama na wala sio Makala.

Kama atatokea mtu awahoji wamachinga wote lazima utafahamu ni nani amewapa kibali cha kufanya biashara kwenye eneo lisiloruhusiwa na kwa mashariti gani.
Makaka wengi wa ccm ni wamachinga...na maeneo mengi ya wazi wanagawia makada wmwa vyama na kufanya vitega uchumi..mfano mzuri ni pale kibamba nyama..Lile ni eneo la TANROAD ambalo wazee wa chama walichukua na kuwagawia watu vizimba then wanapata mgao wao hapo.
 
Hii inaonyesha kuwa hujawahi kutoka nje ya nchi hii, unadhani hivyo ndivyo inatakiwa iwe. HAPANa kaka sio kila mahali kunatakiwa kuuzwe nyanya kwenye meza, haiko hiyo duniani. Ukifanya hivyo huwezi kuzalisha walipakodi wakubwa, mtagawana umaskini kwenye kaya. Mipango miji ni muhimu sana
😍
 
Hee hata kule mikocheni regent njia ya kwenda Kairuki kutokea Victoria, pale napo makada wamefanya Yao, watu wamekodishwa kuuza bia na mishikaki eneo la wazi, pesa yaenda mifukoni
 
Waliotii agizo la serikali la kuondoka bila shuruti kwenye maeneo yasioruhusiwa kwa biashara wanavunjika moyo kuona wenzao waliovunjiwa panoja bado wanaendelea na biashara zao kwenye maeneo yaleyale waliyoyahama. Hii itasababisha yafuatayo:

1. Wanunuzi wasiende kwenye maeneo mapya kutafuta na kununua bidhaa.
2. Waliohama maeneo kukosa wateja na kipato.
3. Waliohama kupata sonona.
4. Waliohama kuwaza kurudi pia kwenye maeneo Yao.
5. Serikali kudharaulika kwa kukurupuka.
6. Kuonyesha kuwa Kuna mvutano ndani ya Chama na serikali na ndani ya Chama na ndani ya serikali.
7. Wamachinga kugombana kwa kulazimisha kurudi kwenye maeneo Yao yaleyale waliyokuwa kabla ya kuvujiwa au kuondoka. Bila shaka maeneo Yao watakuta yanatumiwa na wale amabao wamegoma kuondoka na hakuna wanachofanywa.

Hii ni hatari kubwa sana kwa kiongozi yeyoye anaetoa maagizo yasiyosimamiwa. Rais Magufuli alitufundisha kusimamia maamuzi yako hata kama ulikosea kuamua.

Mmachinga akikamatwa kwenye maeneo yaliyokatazwa sheria ni zile zile makala amesisitiza ,faini Tsh 300,000/= au Jela Mwaka m1 au vyote kwa pamoja.
 
Arusha mji umeanza kua msafi sasa
Wamejitambua, unajua huwezi kupenda kwenda Ulaya na Marekani kusafi na kurudi kwako kukuta kuchafu sana. unashindwa hata kufagia na kuzoa taka.

Wakati ule uwanja wetu haujajengwa Ile terminal 3 ulikuwa ukitoka zako Nairobi, au Addis Ababa (bore airport), au Oliver Tambo airport, au Entebbe, au Amsterdam airport na kutua uwanja wetu wa Julius Nyerere international airport ulikuwa unashikwa na kwikwi, homa na sonona ya ghafla kwa uchafu, harufu na kijiuwanja.

Jamani sio kwamba tunawasagia kunguni wamachinga ila jamani siasa zimetuzidi. Sasa hivi wanamtisha mama na akina Makala ,ooo tutakosa kura, sio kweli tunaochukizwa na uchafu wa miji tuko wengi sana, kwanza machinga hawapigi kura wengi wao.
 
Hii inaonyesha kuwa hujawahi kutoka nje ya nchi hii, unadhani hivyo ndivyo inatakiwa iwe. HAPANa kaka sio kila mahali kunatakiwa kuuzwe nyanya kwenye meza, haiko hiyo duniani. Ukifanya hivyo huwezi kuzalisha walipakodi wakubwa, mtagawana umaskini kwenye kaya. Mipango miji ni muhimu sana
Kwa hiyo mazingira ya london ndo unataka ku apply hapa bongo, hivi akili za hivi huwa mnazitoa wapi!?.....unajua disparity iliyopo ya kiuchumi na standard ya maisha ya nchi zilizoendelea na hizi za ulimwengu wa tatu? walipa kodi wakubwa wapi hao unaowalenga ambao hawawezi kulipa kodi kisa wamachinga wapo mjini? unataka kuua watu wa kipato cha chini kwa kujenga uchumi wa matajiri? eti sijawahi kutoka nje ya nchi..........akili za kilaza kabisa hizi.​
 
Waliotii agizo la serikali la kuondoka bila shuruti kwenye maeneo yasioruhusiwa kwa biashara wanavunjika moyo kuona wenzao waliovunjiwa panoja bado wanaendelea na biashara zao kwenye maeneo yaleyale waliyoyahama. Hii itasababisha yafuatayo:

1. Wanunuzi wasiende kwenye maeneo mapya kutafuta na kununua bidhaa.
2. Waliohama maeneo kukosa wateja na kipato.
3. Waliohama kupata sonona.
4. Waliohama kuwaza kurudi pia kwenye maeneo Yao.
5. Serikali kudharaulika kwa kukurupuka.
6. Kuonyesha kuwa Kuna mvutano ndani ya Chama na serikali na ndani ya Chama na ndani ya serikali.
7. Wamachinga kugombana kwa kulazimisha kurudi kwenye maeneo Yao yaleyale waliyokuwa kabla ya kuvujiwa au kuondoka. Bila shaka maeneo Yao watakuta yanatumiwa na wale amabao wamegoma kuondoka na hakuna wanachofanywa.

Hii ni hatari kubwa sana kwa kiongozi yeyoye anaetoa maagizo yasiyosimamiwa. Rais Magufuli alitufundisha kusimamia maamuzi yako hata kama ulikosea kuamua.
Kashushwa cheo lini tena?
 
Kwa hiyo mazingira ya london ndo unataka ku apply hapa bongo, hivi akili za hivi huwa mnazitoa wapi!?.....unajua disparity iliyopo ya kiuchumi na standard ya maisha ya nchi zilizoendelea na hizi za ulimwengu wa tatu? walipa kodi wakubwa wapi hao unaowalenga ambao hawawezi kulipa kodi kisa wamachinga wapo mjini? unataka kuua watu wa kipato cha chini kwa kujenga uchumi wa matajiri? eti sijawahi kutoka nje ya nchi..........akili za kilaza kabisa hizi.​
Wewe unaamini kijana kupanga chini fungu 4 za ngogwe kutamtoa kuliko kwenda kulima korosho, alizeti, mkonge, au michikichi? Mbona unawapotosha vijana kizembe? Unadhani kuwa umaskini wao utaondoka kwa kupanga dawa za mbu na mende kwenye njia za waenda kwa miguu? Kufikiria hivyo ni kukosa maarifa. Haiwezekani kila nyumba kwenye makazi Kuna genge la nyanya na vitunguu. Vitu hivyo lazima vikanunuliwe sokoni ambako ukaguzi unafanyika na ushuru unakusanywa.
 
Mkuu hakuna nchi inayofanikiwa bila utaratibu...tunashindwa ata na Burundi kwenye milango miji..ukiacha Rwanda.. tukientatain uholela tutatengeneza Jakarta au Mumbai ingine ndani ya Africa
 
Makalla naona kariakoo pamemshinda..mitaa ya katikati zile meza za mbele ya maduka na barabarani alizosema yeye mwenyewe watu wanauziana mamilioni zipo Kama kawaida...serikali imewashindwa au? Hii inaleta taswira tofauti hasa waliovunja kuona wenzao hawajarudi hata hatua moja nyuma kuvunja

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wewe unaamini kijana kupanga chini fungu 4 za ngogwe kutamtoa kuliko kwenda kulima korosho, alizeti, mkonge, au michikichi? Mbona unawapotosha vijana kizembe? Unadhani kuwa umaskini wao utaondoka kwa kupanga dawa za mbu na mende kwenye njia za waenda kwa miguu? Kufikiria hivyo ni kukosa maarifa. Haiwezekani kila nyumba kwenye makazi Kuna genge la nyanya na vitunguu. Vitu hivyo lazima vikanunuliwe sokoni ambako ukaguzi unafanyika na ushuru unakusanywa.
Kuongezeka machinga ni tatizo la kisera, hasa sera mbovu zinazo address maswala ya kiuchumi, uwekezaji na elimu, uongozi usiowajibika kwa dhati kutatua changamoto za wananchi, wengi wapo kwa maslahi ya matumbo yao na familia zao, siasa za majitaka za kutafuta uungwaji mkono, so play your steps carefully.
 
Kwa hiyo mazingira ya london ndo unataka ku apply hapa bongo, hivi akili za hivi huwa mnazitoa wapi!?.....unajua disparity iliyopo ya kiuchumi na standard ya maisha ya nchi zilizoendelea na hizi za ulimwengu wa tatu? walipa kodi wakubwa wapi hao unaowalenga ambao hawawezi kulipa kodi kisa wamachinga wapo mjini? unataka kuua watu wa kipato cha chini kwa kujenga uchumi wa matajiri? eti sijawahi kutoka nje ya nchi..........akili za kilaza kabisa hizi.​
Ni hatari sana kuona kila nyumba Kuna biashara na kila mtaa na uchochoro Kuna biashara. Biashara za hivi hazina udhibiti wa ubora
Kuongezeka machinga ni tatizo la kisera, hasa sera mbovu zinazo address maswala ya kiuchumi, uwekezaji na elimu, uongozi usiowajibika kwa dhati kutatua changamoto za wananchi, wengi wapo kwa maslahi ya matumbo yao na familia zao, siasa za majitaka za kutafuta uungwaji mkono, so play your steps carefully.
Wamachinga haikupaswa kuwa tatizo ya tanzania ambayo inafursa nyingi bado za kulima, kufuga, kuvua, kuchimba na biashara, tatizo liko kwa viongozi ambao waliachia vijana wajazane mitaani kufanya biashara kwenye maeneo ambayo yana matumizi mengine bila kuchukua hatua mapema. Lakini tunajua sababu hasa ya kutokuchukua hatua kumechagizwa na :
1. Kuimarika kwa vyama vya upinzani nchini. Vyama vilikuwa vinaokiteza kura kutoka kwa kila mtu.
2. Viongozi wa CCM binafsi kujinufaisha na wamachinga.
3. Serikali kuchelea kuchukua hatua kabla tatizo halijawa kubwa.
4. Ukosefu wa mikopo ya bei nafuu, pembejeo na masoko kwenye kilimo, mifugo uvuvi, biashara na uchimbaji.
5. Ukosefu wa sera kwa vijana wasiokuwa na ajira.
 
Makalla naona kariakoo pamemshinda..mitaa ya katikati zile meza za mbele ya maduka na barabarani alizosema yeye mwenyewe watu wanauziana mamilioni zipo Kama kawaida...serikali imewashindwa au? Hii inaleta taswira tofauti hasa waliovunja kuona wenzao hawajarudi hata hatua moja nyuma kuvunja

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Makala peke yake hawezi bila support kutoka juu na chini yake, Lushoto na kulia kwake. Kila mtaa una balozi wa nyumba 10, serikali za mtaa, kata, tarafa, na wilaya. Kwanini hawasaidi kudumisha usafi kwenye mtaa na maeneo Yao Hadi Rais na mkuu wa mkoa aende akaondoe wanaochafua mitaa Yao?

Shida ya Nchi hii ni kwamba wale wenye uchungu kabisa na nchi yao wako nje ya mfumo,
 
Kwa hiyo mazingira ya london ndo unataka ku apply hapa bongo, hivi akili za hivi huwa mnazitoa wapi!?.....unajua disparity iliyopo ya kiuchumi na standard ya maisha ya nchi zilizoendelea na hizi za ulimwengu wa tatu? walipa kodi wakubwa wapi hao unaowalenga ambao hawawezi kulipa kodi kisa wamachinga wapo mjini? unataka kuua watu wa kipato cha chini kwa kujenga uchumi wa matajiri? eti sijawahi kutoka nje ya nchi..........akili za kilaza kabisa hizi.​
Mazingira yanatofautiana lakini mahitaji (needs) yanafanana. Nchi zote zinahitaji kodi kutoka kwa wananchi wake kuendesha nchi, uchafu ni chanzo Cha magonjwa kote duniani, watu wanahitaji afya, usalama na uhuru bila kujali nchi Iko bara gani.

Barabara za waenda kwa miguu na mitaro ya majitaka ni haki ya kila raia bila kujali taifa gani. Bidhaa za chakula kuuzwa kwa kuzipanga chini ya mavumbi na tope ni chanzo Cha magonjwa, Kuuza chakula (mamalishe) na kufanya biashara mahali ambako hakuna choo, maji ya kutawaza na kuosha mikono, matunda na vyombo vya kulia chakula sio sawa kiafya bila kujali taifa. Sasa vitu hivyo huwezi kuvikuta huko kwa wenzetu, ndiyo maana nikasema wewe ni WA hapahapa TU kwetu kwakuwa umezaliwa umekuta uchafu huu ukafhani ndio kawaida. Ndiyo maana hata watu wa madaladala ukiwaambia level seat hawakuelewi maana wamezaliwa na kukulia kwenye mazingira haya ya kukanyagana kwenye daladala.
 
Tayari inasemekana wameanza kurejea katika baadhi ya maeneo kama mtaa wa msimbazi kariakoo na mbagala.
 
Back
Top Bottom