kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
- Thread starter
- #41
Kuna ukweli fulani,jana nilipita Ile barabara ya kutoka goba kwenda kinyerezi kukatisha Morogoro road eneo la mbezi luis. Kuanzia pale kwenye round about kuelekea stand ya chini ya daladala hali sio nzuri kabisa. Machinga wamepisha baadhi ya sehemu za njia za waenda kwa miguu lakini wameweka meza na mikokoteni Yao kwenye njia ya magari hivyo kusababisha njia kuwa nyembamba na hatari zaidi kwa machinga na magari kugonga meza na mikokoteni.Tayari inasemekana wameanza kurejea katika baadhi ya maeneo kama mtaa wa msimbazi kariakoo na mbagala.