DC Makala, hakikisha kuwa wamachinga wote hawarejei kwenye maeneo tena

Tayari inasemekana wameanza kurejea katika baadhi ya maeneo kama mtaa wa msimbazi kariakoo na mbagala.
Kuna ukweli fulani,jana nilipita Ile barabara ya kutoka goba kwenda kinyerezi kukatisha Morogoro road eneo la mbezi luis. Kuanzia pale kwenye round about kuelekea stand ya chini ya daladala hali sio nzuri kabisa. Machinga wamepisha baadhi ya sehemu za njia za waenda kwa miguu lakini wameweka meza na mikokoteni Yao kwenye njia ya magari hivyo kusababisha njia kuwa nyembamba na hatari zaidi kwa machinga na magari kugonga meza na mikokoteni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…