DC Moshi awatolea uvivu Kilimanjaro Express, acheni wizi


1. Hivi hawa serikali wana ubora kwenye biashara ipi? Atcl, TRC, ttcl, tanesco, mwendokasi, nk?

2. Kwani ilikuwa je na Uda, kamata, moretco, kauma, kaudo nk?

3. Au weledi wao ni kwenye unyapara tu?

4. LATRA, polisi, DC hawa washauriwe kuweka mabasi yao ya mfano tuone vinginevyo huu ni usanii ule ule kama wa bongo movie tu.
 
Dc anapiga kelele wakati Rc Dsm Viongozi wa polisi na viongozi wa Latra leo wamemuita tajiri Mzee sawaya wafanye nae kikao cha amani bus zote 35 keshokutwa zinarudi barabarani
 
Noana kufungiwa sio solution,unaweza kufungia mabasi kwa miezi sita kesho akayabadilisha jina huoni kifungo sio muhimu sana kwake,hapo ni kumpiga faini tu
Akibadilisha, si atapiga rangi na kufanya maboresho mengine. Hii ndio inayotakiwa. Kuna kampuni itakayopokea basi bovu?
Jana nilitoka Moshi kwa nauli ya 44,000 niotozwa pale ofisini kwao. Nikapata siti mkanda mbovu na gari haina kiyoyozi chapo sikujali sana kwa kuwa nilisafiri usiku. hiyk ndii semi luxury
 
Unafiki tu na ushenzy, mimi nimelipa 55,000 BM tena kwenye mfumo
 
Kwani abilia wote wanaopanda wanaenda sehemu moja?!
 
Tatizo ni CCM
 
Kuhusu nauli waangalie mabasi karibu kampuni zote yana kawaida ya kumtoza abiria nauli kubwa ambae anashukia njiani.
Mfano:
1.Abiria anae kwenda na kushukia lindi uwa anatozwa nauli ya mtwara kampuni zote zinazoenda kusini.

2.Abiria anaetoka songea kuja Dar akiwa anashukia morogoro atatozwa nauli ya Dar.

3.Abiria wa kushukia Gairo anatozwa nauli ya Dodoma
4.Abiria anaetoka mbeya na anashikia moro atatozwa nauli ya Dar.
hizo ni sehemu chache tu bado sijawaeka gari za kanda ya ziwa zinazoanzia Dar zote zina mtindo huu.
Mamlaka husika wajibu kuakikisha mnawahoji abiria na kuangalia tiketi zao msiwe mnauliza mwendo wa dereva tu.
 
Hilo sio tatizo la Mumiliki wa basi ni la wafanyakazi

Mabasi yabatakiwa kuendelea ila wafanyakazi wapewe adhabu

Sioni kosa la Mumiliki Wala mabasi yake
Wewe una akili timamu kweli?
Nani amewaajiri hao wafanyakazi?
Nani anawasimamia hao wafanyakazi?
Nani anawawajibisha hao wafanyakazi?

Iliyofungiwa kutoa huduma ni kampuni, sasa mmiliki na wafanyakazi wake wavune matunda ya kampuni yao.
 
Mkuu umeelewa lakini?
Tiketi ya mtandaoni inaeleza unapotoka (mfano Kilimanjaro) na unapokwenda (Dar) na kiasi cha pesa unachotakiwa kulipa. Kulipishwa tofauti na hivyo ni wizi na utapeli, haupaswi kuhalalishwa.

Anachofanya Kilimanjaro ni hiki:
1. Hataki kukatishia tiketi mtandaoni (maana anajua ndipo mahali pa kupigia cha juu).

2. Ana nauli zake tofauti na muongozo.
3. Anakukatia tiketi ya gharama ya juu (VIP) lakini anakusafirisha kwa ngala ngala la kubebea mkaa.
 
Hatua hiyo itokana na wamiliki wa mabasi hayo kuendelea kuwakatia tiketi abiria huku wakijua kuna katazo na baada ya abiria kuona hakuna kinachoendelea wakamtwangia simu naye chap akatia timu na ODC wake.
Hao wananchi nao hamnazo, je hawakusikia tangazo mpaka waende kukata tiketi kwenye kampuni iliyofungiwa? Kama wana Moshi tunaowajua wameadvance kimaisha wanakuwa wagumu kuelewa je hali ipoje Ruangwa, Matombo, Muyama na kunakofanana na huko?
 
Mbona hii ni common kila sehemu, ukikata ticket Njombe kwenda Morogoro au Dodoma kwenda Morogoro au Singida kwenda Morogoro unatozwa nauli za Dar hilo halina ubishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…