DC Moshi awatolea uvivu Kilimanjaro Express, acheni wizi

MKUU wa wilaya ya Moshi,Kisare Makori leo alikuwa kwenye ofisi za makampuni ya mabasi ya Kilimanjaro express baada ya abria kusota kwa saa sita bila usafiri kufuatia katazo la Mamlaka ya udhibiti usafiri Ardhini(LATRA) kwa mabasi hayo kusafrisha abiria kuanzia leo kwa kukiuka masharti ya leseni ya usafrishaji.

Hatua hiyo itokana na wamiliki wa mabasi hayo kuendelea kuwakatia tiketi abiria huku wakijua kuna katazo na baada ya abiria kuona hakuna kinachoendelea wakamtwangia simu naye chap akatia timu na ODC wake.

View attachment 2865457

Baada ya kufika na kukuta watu wa kutosha, akazungumza na abiria na hakusita kusema wazi kuwa kinachofanywa na wenye mabasi hayo ni wizi kama wizi mwingine.

Ilikuwa hivi;

Saa nne asubuhi mkuu huyo wa wilaya alifika kwenye ofisi za mabasi hayo na kuweka wazi kuwa wenye mabasi hayo wamekuwa wakikiuka taratibu za usafrishaji ikiwamo kuwatoza nauli kubwa abiria wanaoanzia safari zao Moshi Mjini kwenda Dar es salaam(44,000) ambayo ni nauli ya abiria anayeanzia safari zake Arusha badala ya Tsh. 37,000 kwa mabasi ya daraja la kawaida.

Utapeli mwingine ambao DC ameutaja ni abiria kupewa tiketi zisizo na namba za mabasi na hivyo kupandishwa kwenye mabasi ambayo hayaendani ya nauli waliyotozwa huku wakilipishwa nauli kubwa ambayo kwenye tiketi inaandikwa pungufu.

View attachment 2865458

“Kuna sheria ilipitishwa na Bunge kwa watoa huduma ya usafrishaji kutoa tiketi za mtandaoni,hawa Kilimanjaro wamegoma, wamedinda, wao wana sharia zao hawataki kufuata sheria,”

“Ulanguzi wa tiketi ni wizi kama wizi mwingine, haiwezekani mtu anasafiri kutoka Moshi kwenda Dar es salaam anatozwa nauli sawa na mtu anayeanzia safari yake Arusha. Kama serikali hatuwezi kuruhusu mambo ya kitapeli namna hiyo”

Wakati mkuu huyo wa wilaya akiingia kwenye jengo la Hotel ya Kilimanjaro ambako ndipo ofisi za mabasi hayo zilipo, wafanyakazi wa kampuni hiyo waliokuwa wakiendelea na zoezi la kurejesha nauli za abiria, ghafla walitoweka na wengine kujificha chooni na wengine kwenye baadhi ya vyumba vya kulala wageni na mkuu huyo wa wilaya kumwagiza OCD kuwatia mbaroni wachache waliobaki.

Kuanzia asubuhi ya leo maofisa wa LATRA wakiongozwa na Ofisa mfawidhi mkoa wa Kilimanjaro,Pual Nyello walikuwa wamepiga kambi kwenye ofisi za mabasi hayo kuhakikisha hakuna basi linapakia abiria.

Nyello alisema kuwa mabasi hayo yamekuwa yakifanya makossa ya mara kwa mara na licha ya wamiliki wake kuandikiwa barua mara kwa mara za onyo na hata kuitwa na kupewa elimu wamekuwa wakikaidi maelekezo yao.

Akasema makosa yamekuwa yakijirudia mara kwa mara ikiwamo kuzidisha nauli tofauti na nauli elekezi ambako baadhi ya abiria hutozwa nauli kubwa isiyoendana na kiwango halisi huku pia mabasi wanayopakizwa si madaraja husika pamoja na kutotoa tiketi za mtandaoni.

“Kama mnavyojua mabasi 35 ya kampuni hii ya Kilimanjaro wamezuiwa kutoa huduma kutokana na makossa mbali mbali na tumekuwa tukiwaita kwa maana ya ofisi zetu za makao makuu na sisi huku mikoani na kuandikiwa barua mara kwa mara na kupewa onyo lakini hawakuwa tayari kubadiliki.”

Jumamosi ya Januari 6 mwaka huuLATRA imeyasimamisha mabasi yote ya Kampuni ya Kilimanjaro Express kutoa huduma ya usafirishaji kuanzia leo jumatatu kutokana na kukiuka masharti ya leseni ikiwamo kutotoa tiketi ya kielektroniki na kuzidisha nauli kwa abiria.

Zuio hilo lilitangazwa na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Habibu Suluo baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika stendi ya mabasi ya Magufuli pamoja na ofisi za mabasi ya kampuni hiyo ya Kilimanjaro Shekilango Dar es Salaam.

Suluo alisema baada ya kufanya ukaguzi huo, ilibainika kuwa mabasi hayo pekee ndio bado yanatoa tiketi zisizo za kielektroniki na kwamba yamebainika kukiuka masharti mengi ya leseni licha ya kuonywa mara kwa mara na kutozwa faini.

"Na leo (Jumamosi)tumelikamata gari jingine la kampuni hii ya Kilimanjaro inayofanya safari zake Dar es Salaam kwenda Moshi na Arusha likiwa limezidisha nauli kwa abiria, kila abiria alilipishwa nauli tofauti, tukawataka wawarejeshee nauli zao, wakakubali, lakini muda mfupi tumetoka kwenye ofisi zao wakakataa tena kurejesha eti mpaka bosi wao aseme,"amesema Suluo.

"Na hii siyo mara moja, wamekuwa wakifanya hivi mara nyingi na tumewaonya mara kwa mara na anaona kulipa faini ni kawaida kwake. Sasa sisi lengo letu ni kutaka wafuate sheria na masharti ya leseni, watoe huduma bora na siyo kutoa faini.

“Na kama anaona kulipa faini ni kawaida kwake sisi hatuwezi kuvumilia, tumetoa maagizo asitoe huduma kuanzia jumatatu (leo) mpaka atakapofanya maboresho na kufuata masharti ya leseni yake."

Hii ya ticket sio kweli, ma bus mengi tu hawatoi ticket za kielectronic na ukiwaukiza wanasema utapewa kwenye bus na ndio imetoka hiyo.

Juzi kuna dogo amekata ticket Bus la Capricon Arusha Mbeya kwa tshs 69,000/- na hawakutoa eletronic receipt.

Kilimanjaro katolewa kafara tu.
 
Kwani abilia wote wanaopanda wanaenda sehemu moja?!
"Abiria" siyo "abilia" hivyo inaonyesha wewe ni mpogoro na kwenda kwenu Kidatu unapanda ma Coaster ya kuunga unga.

Kilimanjaro Express ukikata ticket hata kama unashuka Chalinze, au Mombo au Moshi wanakupiga naauli moja ya Arusha yaani 55,000/- .

Ukienda kukata hawakuulizi unaposhukia, maana ukisema unashuka Same wanakuacha kuna atakayekuja wa kushuka ARusha..
 
MKUU wa wilaya ya Moshi,Kisare Makori leo alikuwa kwenye ofisi za makampuni ya mabasi ya Kilimanjaro express baada ya abria kusota kwa saa sita bila usafiri kufuatia katazo la Mamlaka ya udhibiti usafiri Ardhini(LATRA) kwa mabasi hayo kusafrisha abiria kuanzia leo kwa kukiuka masharti ya leseni ya usafrishaji.

Hatua hiyo itokana na wamiliki wa mabasi hayo kuendelea kuwakatia tiketi abiria huku wakijua kuna katazo na baada ya abiria kuona hakuna kinachoendelea wakamtwangia simu naye chap akatia timu na ODC wake.

View attachment 2865457

Baada ya kufika na kukuta watu wa kutosha, akazungumza na abiria na hakusita kusema wazi kuwa kinachofanywa na wenye mabasi hayo ni wizi kama wizi mwingine.

Ilikuwa hivi;

Saa nne asubuhi mkuu huyo wa wilaya alifika kwenye ofisi za mabasi hayo na kuweka wazi kuwa wenye mabasi hayo wamekuwa wakikiuka taratibu za usafrishaji ikiwamo kuwatoza nauli kubwa abiria wanaoanzia safari zao Moshi Mjini kwenda Dar es salaam(44,000) ambayo ni nauli ya abiria anayeanzia safari zake Arusha badala ya Tsh. 37,000 kwa mabasi ya daraja la kawaida.

Utapeli mwingine ambao DC ameutaja ni abiria kupewa tiketi zisizo na namba za mabasi na hivyo kupandishwa kwenye mabasi ambayo hayaendani ya nauli waliyotozwa huku wakilipishwa nauli kubwa ambayo kwenye tiketi inaandikwa pungufu.

View attachment 2865458

“Kuna sheria ilipitishwa na Bunge kwa watoa huduma ya usafrishaji kutoa tiketi za mtandaoni,hawa Kilimanjaro wamegoma, wamedinda, wao wana sharia zao hawataki kufuata sheria,”

“Ulanguzi wa tiketi ni wizi kama wizi mwingine, haiwezekani mtu anasafiri kutoka Moshi kwenda Dar es salaam anatozwa nauli sawa na mtu anayeanzia safari yake Arusha. Kama serikali hatuwezi kuruhusu mambo ya kitapeli namna hiyo”

Wakati mkuu huyo wa wilaya akiingia kwenye jengo la Hotel ya Kilimanjaro ambako ndipo ofisi za mabasi hayo zilipo, wafanyakazi wa kampuni hiyo waliokuwa wakiendelea na zoezi la kurejesha nauli za abiria, ghafla walitoweka na wengine kujificha chooni na wengine kwenye baadhi ya vyumba vya kulala wageni na mkuu huyo wa wilaya kumwagiza OCD kuwatia mbaroni wachache waliobaki.

Kuanzia asubuhi ya leo maofisa wa LATRA wakiongozwa na Ofisa mfawidhi mkoa wa Kilimanjaro,Pual Nyello walikuwa wamepiga kambi kwenye ofisi za mabasi hayo kuhakikisha hakuna basi linapakia abiria.

Nyello alisema kuwa mabasi hayo yamekuwa yakifanya makossa ya mara kwa mara na licha ya wamiliki wake kuandikiwa barua mara kwa mara za onyo na hata kuitwa na kupewa elimu wamekuwa wakikaidi maelekezo yao.

Akasema makosa yamekuwa yakijirudia mara kwa mara ikiwamo kuzidisha nauli tofauti na nauli elekezi ambako baadhi ya abiria hutozwa nauli kubwa isiyoendana na kiwango halisi huku pia mabasi wanayopakizwa si madaraja husika pamoja na kutotoa tiketi za mtandaoni.

“Kama mnavyojua mabasi 35 ya kampuni hii ya Kilimanjaro wamezuiwa kutoa huduma kutokana na makossa mbali mbali na tumekuwa tukiwaita kwa maana ya ofisi zetu za makao makuu na sisi huku mikoani na kuandikiwa barua mara kwa mara na kupewa onyo lakini hawakuwa tayari kubadiliki.”

Jumamosi ya Januari 6 mwaka huuLATRA imeyasimamisha mabasi yote ya Kampuni ya Kilimanjaro Express kutoa huduma ya usafirishaji kuanzia leo jumatatu kutokana na kukiuka masharti ya leseni ikiwamo kutotoa tiketi ya kielektroniki na kuzidisha nauli kwa abiria.

Zuio hilo lilitangazwa na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Habibu Suluo baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika stendi ya mabasi ya Magufuli pamoja na ofisi za mabasi ya kampuni hiyo ya Kilimanjaro Shekilango Dar es Salaam.

Suluo alisema baada ya kufanya ukaguzi huo, ilibainika kuwa mabasi hayo pekee ndio bado yanatoa tiketi zisizo za kielektroniki na kwamba yamebainika kukiuka masharti mengi ya leseni licha ya kuonywa mara kwa mara na kutozwa faini.

"Na leo (Jumamosi)tumelikamata gari jingine la kampuni hii ya Kilimanjaro inayofanya safari zake Dar es Salaam kwenda Moshi na Arusha likiwa limezidisha nauli kwa abiria, kila abiria alilipishwa nauli tofauti, tukawataka wawarejeshee nauli zao, wakakubali, lakini muda mfupi tumetoka kwenye ofisi zao wakakataa tena kurejesha eti mpaka bosi wao aseme,"amesema Suluo.

"Na hii siyo mara moja, wamekuwa wakifanya hivi mara nyingi na tumewaonya mara kwa mara na anaona kulipa faini ni kawaida kwake. Sasa sisi lengo letu ni kutaka wafuate sheria na masharti ya leseni, watoe huduma bora na siyo kutoa faini.

“Na kama anaona kulipa faini ni kawaida kwake sisi hatuwezi kuvumilia, tumetoa maagizo asitoe huduma kuanzia jumatatu (leo) mpaka atakapofanya maboresho na kufuata masharti ya leseni yake."
NO ONE IS ABOVE THE LAW
 
Wapumbavu kabisa kufungia
Basi anaumia abiria bora upige faini tuuu

Soma vizuri. LATRA wamempiga faini mara nyingi na kumwita ofisini kumpa elimu, yeye akaendelea na ujinga wameamua kumfungia.
 
Hilo sio tatizo la Mumiliki wa basi ni la wafanyakazi

Mabasi yabatakiwa kuendelea ila wafanyakazi wapewe adhabu

Sioni kosa la Mumiliki Wala mabasi yake

Waendelee kufanya ujinga?. Mabasi ni mabovu yana zidisha nauli, yaendelee na huyo ujinga kisa wanelipa fine?
 
Noana kufungiwa sio solution,unaweza kufungia mabasi kwa miezi sita kesho akayabadilisha jina huoni kifungo sio muhimu sana kwake,hapo ni kumpiga faini tu

Hata akibadilisha jina na akaendelea na ujinga watamfungia. Issue kubwa ni kwamba abadilike.
 
Dc anapiga kelele wakati Rc Dsm Viongozi wa polisi na viongozi wa Latra leo wamemuita tajiri Mzee sawaya wafanye nae kikao cha amani bus zote 35 keshokutwa zinarudi barabarani

Ila abadilike
 
Hilo gar nilipanda mara moja dar arusha.sipand tena. Now nakula chuma abood luxury. Kwanza kilimanjaro wana mahotel yao bei mbaya sana na migari yao sio mzizur
Na bado huduma zao za Hotel ni mbaya.. Wahudumu wana lugha mbaya..

Hayo Magari hapana aiseee..

Extra luxury Coach for life.
 
Watu hawaelewi tu..Bwana Sawaya apunguze kukaza fuvu..Dunia imebadilila sana.
Kilimanjaro ana Bus 4 tu nzuri kwa sasa..na hazina mwaka zimeanza kuwa za hovyo ndani.

VIP bongo bado sana aisee...
Eti VIP! Ila bongo tuna vituko. Eti kuna mabasi yana madaraja ya luxury, semi-luxury. Luxury my foot!! Hivi walioweka haya madaraja wanaelewa maana ya luxury?! Kwanini isingekuwa tu daraja la kwanza, la pili, la tatu..?
 
Suala la nauli za juu ni mabasi yote, mabasi yoote tanzania hii wanatoza nauli ya juu kuliko ile imewekwa na serikali, tizama nauli ya dar dom ni sh ngapi kisha njoo utizame wanavyotoza kwenye mabus.
 
Lilikuwa gari langu la miaka yote ila siku nmekata ticker ya VIP kwa elfu arobaini halafu nikakaa kwenye gari baya ndyo ilikuwa mwisho.
Gari Lina siti fupi ukikaa kama upo jikoni
Choo kichafu kinanukaa njia nzima
Nilikerekaa na siwezi panda tenaa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuhusu nauli waangalie mabasi karibu kampuni zote yana kawaida ya kumtoza abiria nauli kubwa ambae anashukia njiani.
Mfano:
1.Abiria anae kwenda na kushukia lindi uwa anatozwa nauli ya mtwara kampuni zote zinazoenda kusini.

2.Abiria anaetoka songea kuja Dar akiwa anashukia morogoro atatozwa nauli ya Dar.

3.Abiria wa kushukia Gairo anatozwa nauli ya Dodoma
4.Abiria anaetoka mbeya na anashikia moro atatozwa nauli ya Dar.
hizo ni sehemu chache tu bado sijawaeka gari za kanda ya ziwa zinazoanzia Dar zote zina mtindo huu.
Mamlaka husika wajibu kuakikisha mnawahoji abiria na kuangalia tiketi zao msiwe mnauliza mwendo wa dereva tu.
Tena hapo kwa Songea to Dar wa kushuka Moro ndo imeanza zamani sana.
 
Kosa la wafanyakazi anasukumiwa tajiri na mabasi haiko sahihi
Tajiri na mabasi yake hawana shida tatizo wafanyakazi unaadhibuje mabasi na Tajiri? Sheria zizingatiwe

Kila mmoja abebe mzigo wake Tajiri wa Kilimanjaro na mabasi yake kaonewa
Bro mbona unapambana na shida wafanyakazi? Kwani wafanyakazi wanamiliki kampuni? Ndio waliandikiwa mabarua ya onyo?
 
Back
Top Bottom