DC Moshi awatolea uvivu Kilimanjaro Express, acheni wizi

DC Moshi awatolea uvivu Kilimanjaro Express, acheni wizi

“Ulanguzi wa tiketi ni wizi kama wizi mwingine, haiwezekani mtu anasafiri kutoka Moshi kwenda Dar es salaam anatozwa nauli sawa na mtu anayeanzia safari yake Arusha. Kama serikali hatuwezi kuruhusu mambo ya kitapeli namna hiyo”
Huyu jama si ndiyo Sawaya aliwahi kufungwa kwa ujambazi miaka ya huko nyuma? Halafu amejificha chini ya mwavuli wa mstari wa biblia "Bwana ndiye mchungaji wangu"
 
LATRA tupo pamoja, Sheria zifuatwe, Wizi mkubwa hu wa elfu 8,000 * abiria 52 =461,000/= kwa basi moja.
Sasa mabasi 35 * 461,000= 14,560,000/

Kwa siku Mzee Sawaya Mawalla anapata faida ya zuluma milioni kumi na nne na nusu.
Hapo anatoa laki tano ya kugawa jamaa wa brush viatu huko barabarani.
😅😅😅😅 hizi hesabu utafikiri kweli kumbe za kizushi.
 
Pumbafu, abiria,pumbafu, dc na wengine wote mnaopanda kwenye hizo bus.... Muda mwingine watanzania muwe na akili kidogo yaani kichwa kinakuwa kama kopo la dawa ya kuulia wadudu... Simnayajua yale? Eeh sawa haiwezekan wengine mnalalamika hapo hapo mengine yanaenda kupanda
 
Hilo sio tatizo la Mumiliki wa basi ni la wafanyakazi

Mabasi yabatakiwa kuendelea ila wafanyakazi wapewe adhabu

Sioni kosa la Mumiliki Wala mabasi yake
Ukiwa unapewa adhabu mara Kwa mara lakin makosa yanajirudia unashauri nini kinatakiwa kifanyike?

Alieenda kuomba leseni ni mmiliki, sio wafanyakazi. Hao watajuana wenyewe na boss wao.
 
Dc anapiga kelele wakati Rc Dsm Viongozi wa polisi na viongozi wa Latra leo wamemuita tajiri Mzee sawaya wafanye nae kikao cha amani bus zote 35 keshokutwa zinarudi barabarani
Umesikiliza kile kikao? Hajakatazwa kurudi barabarani Bali atimize masharti kwanza aliyopewa na latra, Moja wapo ni kutoza nauli husika na kulipa faini za serikali
 
Huyu jama si ndiyo Sawaya aliwahi kufungwa kwa ujambazi miaka ya huko nyuma? Halafu amejificha chini ya mwavuli wa mstari wa biblia "Bwana ndiye mchungaji wangu"
Bwana ndiye mchungaji wangu sio Dar express? Au yule ni In God we trust. Alifungwa kwa kuiba matairi
 
Bwana ndiye mchungaji wangu sio Dar express?
IMG-20160821-WA0087.jpg
Ef7os4KXYAArK4h.jpg
 
“Ulanguzi wa tiketi ni wizi kama wizi mwingine, haiwezekani mtu anasafiri kutoka Moshi kwenda Dar es salaam anatozwa nauli sawa na mtu anayeanzia safari yake Arusha. Kama serikali hatuwezi kuruhusu mambo ya kitapeli namna hiyo”

Si ajabu baada ya tamko hili, mkuu wa wilaya na OCD wake waliondoka pasipo kutia pingu watu kadhaa, pamoja na kukiri kwamba kuna wizi kosa ambalo ni jinai kwa mujibu wa sheria zetu...

Na pengine wakaishia kukamata watu wasiohusika wakati kuna wamiliki na wanajulikana walipo...
 
MKUU wa wilaya ya Moshi,Kisare Makori leo alikuwa kwenye ofisi za makampuni ya mabasi ya Kilimanjaro express baada ya abria kusota kwa saa sita bila usafiri kufuatia katazo la Mamlaka ya udhibiti usafiri Ardhini(LATRA) kwa mabasi hayo kusafrisha abiria kuanzia leo kwa kukiuka masharti ya leseni ya usafrishaji.

Hatua hiyo itokana na wamiliki wa mabasi hayo kuendelea kuwakatia tiketi abiria huku wakijua kuna katazo na baada ya abiria kuona hakuna kinachoendelea wakamtwangia simu naye chap akatia timu na ODC wake.

View attachment 2865457

Baada ya kufika na kukuta watu wa kutosha, akazungumza na abiria na hakusita kusema wazi kuwa kinachofanywa na wenye mabasi hayo ni wizi kama wizi mwingine.

Ilikuwa hivi;

Saa nne asubuhi mkuu huyo wa wilaya alifika kwenye ofisi za mabasi hayo na kuweka wazi kuwa wenye mabasi hayo wamekuwa wakikiuka taratibu za usafrishaji ikiwamo kuwatoza nauli kubwa abiria wanaoanzia safari zao Moshi Mjini kwenda Dar es salaam(44,000) ambayo ni nauli ya abiria anayeanzia safari zake Arusha badala ya Tsh. 37,000 kwa mabasi ya daraja la kawaida.

Utapeli mwingine ambao DC ameutaja ni abiria kupewa tiketi zisizo na namba za mabasi na hivyo kupandishwa kwenye mabasi ambayo hayaendani ya nauli waliyotozwa huku wakilipishwa nauli kubwa ambayo kwenye tiketi inaandikwa pungufu.

View attachment 2865458

“Kuna sheria ilipitishwa na Bunge kwa watoa huduma ya usafrishaji kutoa tiketi za mtandaoni,hawa Kilimanjaro wamegoma, wamedinda, wao wana sharia zao hawataki kufuata sheria,”

“Ulanguzi wa tiketi ni wizi kama wizi mwingine, haiwezekani mtu anasafiri kutoka Moshi kwenda Dar es salaam anatozwa nauli sawa na mtu anayeanzia safari yake Arusha. Kama serikali hatuwezi kuruhusu mambo ya kitapeli namna hiyo”

Wakati mkuu huyo wa wilaya akiingia kwenye jengo la Hotel ya Kilimanjaro ambako ndipo ofisi za mabasi hayo zilipo, wafanyakazi wa kampuni hiyo waliokuwa wakiendelea na zoezi la kurejesha nauli za abiria, ghafla walitoweka na wengine kujificha chooni na wengine kwenye baadhi ya vyumba vya kulala wageni na mkuu huyo wa wilaya kumwagiza OCD kuwatia mbaroni wachache waliobaki.

Kuanzia asubuhi ya leo maofisa wa LATRA wakiongozwa na Ofisa mfawidhi mkoa wa Kilimanjaro,Pual Nyello walikuwa wamepiga kambi kwenye ofisi za mabasi hayo kuhakikisha hakuna basi linapakia abiria.

Nyello alisema kuwa mabasi hayo yamekuwa yakifanya makossa ya mara kwa mara na licha ya wamiliki wake kuandikiwa barua mara kwa mara za onyo na hata kuitwa na kupewa elimu wamekuwa wakikaidi maelekezo yao.

Akasema makosa yamekuwa yakijirudia mara kwa mara ikiwamo kuzidisha nauli tofauti na nauli elekezi ambako baadhi ya abiria hutozwa nauli kubwa isiyoendana na kiwango halisi huku pia mabasi wanayopakizwa si madaraja husika pamoja na kutotoa tiketi za mtandaoni.

“Kama mnavyojua mabasi 35 ya kampuni hii ya Kilimanjaro wamezuiwa kutoa huduma kutokana na makossa mbali mbali na tumekuwa tukiwaita kwa maana ya ofisi zetu za makao makuu na sisi huku mikoani na kuandikiwa barua mara kwa mara na kupewa onyo lakini hawakuwa tayari kubadiliki.”

Jumamosi ya Januari 6 mwaka huuLATRA imeyasimamisha mabasi yote ya Kampuni ya Kilimanjaro Express kutoa huduma ya usafirishaji kuanzia leo jumatatu kutokana na kukiuka masharti ya leseni ikiwamo kutotoa tiketi ya kielektroniki na kuzidisha nauli kwa abiria.

Zuio hilo lilitangazwa na Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Habibu Suluo baada ya kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika stendi ya mabasi ya Magufuli pamoja na ofisi za mabasi ya kampuni hiyo ya Kilimanjaro Shekilango Dar es Salaam.

Suluo alisema baada ya kufanya ukaguzi huo, ilibainika kuwa mabasi hayo pekee ndio bado yanatoa tiketi zisizo za kielektroniki na kwamba yamebainika kukiuka masharti mengi ya leseni licha ya kuonywa mara kwa mara na kutozwa faini.

"Na leo (Jumamosi)tumelikamata gari jingine la kampuni hii ya Kilimanjaro inayofanya safari zake Dar es Salaam kwenda Moshi na Arusha likiwa limezidisha nauli kwa abiria, kila abiria alilipishwa nauli tofauti, tukawataka wawarejeshee nauli zao, wakakubali, lakini muda mfupi tumetoka kwenye ofisi zao wakakataa tena kurejesha eti mpaka bosi wao aseme,"amesema Suluo.

"Na hii siyo mara moja, wamekuwa wakifanya hivi mara nyingi na tumewaonya mara kwa mara na anaona kulipa faini ni kawaida kwake. Sasa sisi lengo letu ni kutaka wafuate sheria na masharti ya leseni, watoe huduma bora na siyo kutoa faini.

“Na kama anaona kulipa faini ni kawaida kwake sisi hatuwezi kuvumilia, tumetoa maagizo asitoe huduma kuanzia jumatatu (leo) mpaka atakapofanya maboresho na kufuata masharti ya leseni yake."
Hawa Walitakiwa kuwa ndani Kwa uhujumu uchumi na akaunti zao kushikiliwa.

Jiwe alikuwa hawachekei kabisa ,wanakwepa Kodi na wanabambikia watu nauli.
 
Back
Top Bottom