DC Moshi awatolea uvivu Kilimanjaro Express, acheni wizi

“Ulanguzi wa tiketi ni wizi kama wizi mwingine, haiwezekani mtu anasafiri kutoka Moshi kwenda Dar es salaam anatozwa nauli sawa na mtu anayeanzia safari yake Arusha. Kama serikali hatuwezi kuruhusu mambo ya kitapeli namna hiyo”
Huyu jama si ndiyo Sawaya aliwahi kufungwa kwa ujambazi miaka ya huko nyuma? Halafu amejificha chini ya mwavuli wa mstari wa biblia "Bwana ndiye mchungaji wangu"
 
😅😅😅😅 hizi hesabu utafikiri kweli kumbe za kizushi.
 
Pumbafu, abiria,pumbafu, dc na wengine wote mnaopanda kwenye hizo bus.... Muda mwingine watanzania muwe na akili kidogo yaani kichwa kinakuwa kama kopo la dawa ya kuulia wadudu... Simnayajua yale? Eeh sawa haiwezekan wengine mnalalamika hapo hapo mengine yanaenda kupanda
 
Hilo sio tatizo la Mumiliki wa basi ni la wafanyakazi

Mabasi yabatakiwa kuendelea ila wafanyakazi wapewe adhabu

Sioni kosa la Mumiliki Wala mabasi yake
Ukiwa unapewa adhabu mara Kwa mara lakin makosa yanajirudia unashauri nini kinatakiwa kifanyike?

Alieenda kuomba leseni ni mmiliki, sio wafanyakazi. Hao watajuana wenyewe na boss wao.
 
Dc anapiga kelele wakati Rc Dsm Viongozi wa polisi na viongozi wa Latra leo wamemuita tajiri Mzee sawaya wafanye nae kikao cha amani bus zote 35 keshokutwa zinarudi barabarani
Umesikiliza kile kikao? Hajakatazwa kurudi barabarani Bali atimize masharti kwanza aliyopewa na latra, Moja wapo ni kutoza nauli husika na kulipa faini za serikali
 
Huyu jama si ndiyo Sawaya aliwahi kufungwa kwa ujambazi miaka ya huko nyuma? Halafu amejificha chini ya mwavuli wa mstari wa biblia "Bwana ndiye mchungaji wangu"
Bwana ndiye mchungaji wangu sio Dar express? Au yule ni In God we trust. Alifungwa kwa kuiba matairi
 
“Ulanguzi wa tiketi ni wizi kama wizi mwingine, haiwezekani mtu anasafiri kutoka Moshi kwenda Dar es salaam anatozwa nauli sawa na mtu anayeanzia safari yake Arusha. Kama serikali hatuwezi kuruhusu mambo ya kitapeli namna hiyo”

Si ajabu baada ya tamko hili, mkuu wa wilaya na OCD wake waliondoka pasipo kutia pingu watu kadhaa, pamoja na kukiri kwamba kuna wizi kosa ambalo ni jinai kwa mujibu wa sheria zetu...

Na pengine wakaishia kukamata watu wasiohusika wakati kuna wamiliki na wanajulikana walipo...
 
Hawa Walitakiwa kuwa ndani Kwa uhujumu uchumi na akaunti zao kushikiliwa.

Jiwe alikuwa hawachekei kabisa ,wanakwepa Kodi na wanabambikia watu nauli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…