DC Tarime akumbusha katazo la kuendeleza maeneo yanayoguswa na mradi wa ujenzi wa bwawa la TSF – North Mara

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165

Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhe. Meja Edward Gowele, amewakumbusha wananchi wa Kijiji cha Nyangoto, Kata za Mangoto na Nyangoto, kuzingatia katazo la Serikali la kutofanya maendeleo mapya katika maeneo yanayoguswa na Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la TSF wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaomilikiwa na Barrick, wakati Serikali ikiendelea na hatua za uthamini.

Mhe. Gowele amewataka wananchi ambao bado wanaendelea kufanya maendelezo katika maeneo hayo, licha ya kuwepo kwa zuio, kusitisha mara moja shughuli hizo na kuacha kufanya maendelezo yoyote mapya hadi taratibu za uthamini zitakapokamilika kwa mujibu wa sheria na maelekezo ya Serikali.

Aidha, amesisitiza kuwa wananchi wote wanapaswa kuheshimu na kutekeleza zuio hilo, huku akiwataka wanaokiuka maelekezo hayo kuacha mara moja, ili kuepusha usumbufu na changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa zoezi la uthamini na hatua zinazofuata za mradi.

View: https://youtu.be/GkNptfCKTNo?si=gm2rLf6rWuqMIwgf

TARIME,

Bora mfumo Humu,Kuna maeneo mnakaa kimyaa,watu wanajenga,wanauza, baadae mnajitokeza kuwa ni mradi flani unskusudiwa,mfano mzuri hapa Dodoma karibu na Kisasa,Kuna eneo linaitwa block F.Watu wameshusha nyumba za Maana kwenye Ramani inasomeka ni shule Tena ya msingi!Ila mwenyekiti na balozi wanashirikiana na baadhi ya maofisa kuhalalisha ujenzi.
 
Back
Top Bottom