DC Temeke: Mtu akipiga Picha na hela akamatwe

YAni matatizo yaliyojaa kwenye wilaya anayo tawala yamemshinda lakini bado anawapigia kelele watu wanaopiga picha na pesa zao anajua wamezipataje ๐Ÿค” na wakisha kamatwa watashitakiwa kwa kesi gani๐Ÿค” akitoka zake hapo anaenda kuimba mapambio ulaji unaendelea kuwepo ๐Ÿ˜…
 
Shughuli nyingine wanazo jitafutiaga si za msingi na hazina msaada wowote kwa raia.
 
Hiki cheo kitafutiwe kazi maalumu ya kueleweka.
Au kifutwe kabisa.

Sasa unamkamata mtu kakiuka sheria gani?

Halafu anasema eti hela inatakiwa ifichwe ,
Ndio huko CCM mnavyofundishana?
 
Kama wadau walivyopendekeza vyeo vya U DC na U RC vifutwe hawakukosea! Hawana kazi kabisa.
 
Kiuhalisia sio poa sema nae kimtindo zinamtoa udenda!
 
Kupiga picha umeshika hela ni kujitoa fotokopi uwe na hela marambili, ni kosa kutengeneza pesa.
 
Hawa watu wanapataje hizi nafasi? Level of incompetence inatisha
 
Tuna tatizo la uongozi sana kila siku vituko tu mara utasikia mwingine anakamata sijui madada poa anavamia nyumba za kulala wageni anamtoa kila mteja na kumkamata!,mara mwingine anadai kwenye wilaya yake hataki sherehe za unyago! Huyu naye kaja na yake! Ipo siku watu watakatazwa kwenda kujisaidia muda wa kazi!
Maana mtu unajiuliza pesa yako umezitafuta mwenyewe sasa ukiamua kupiga picha nazo shida ipo wapi? Yaani hawa watu ni mahasidi sana na wana roho mbaya sana kwa sababu wao wakiona mtu amepata vihela kidogo wanaumia sana wanatamani watu wote wawe masikini tu ili tuendelee kuwa watumwa wao tu.
 
Sio ustaarabu kupiga hela na picha hadharani.
Unakuwa unajihatarisha usalama wako binafsi.
Huna escort unapiga picha na maburungutu ya pesa ukitekwa serikali ilaumiwe wakati wewe ndo umewashawishi wezi wakukabe.
Mkuu wa wilaya ndo Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama laZima adhibiti huu uhuni
 
wee kiherehere mwenzio kaleta uzi nawewe unaleta๐Ÿ˜•๐Ÿ˜•
mrembo kiherehere wewe๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ