DC Temeke: Mtu akipiga Picha na hela akamatwe

Mjinga mwingine huyu hapa FIU wana mamlaka ya kuuliza.
 
DC ana gubu la kunyimwa kinyeo, akwende huko na masheria yake uchwara.

Tena ngoja nikarekodi video muda huu nione kama ataleta pua yake kuniuliza swali rorose.
 
Kuna mwingine wa mkaa. Ni marufuku kubeba mkaa kwenye pikipiki
 
Kwani ni mtumishi wa serikali hadi umuulize katoa wapi? Na Akinunua gari kwa hizo pesa asipige nalo picha pia?
 
Utii ukizidi hugeuka utumwa,wakoloni wanaona wanatuweza.
 
Hawa wanamchunguza kwanza mtu na kujiridhisha kama kuna viashiria vya uvunjwaji wa sheria. hawakurupuku kama huyo dc kilaza alivosema kwamba mtu akipost picha na fedha anakamatwa.
Huyo dc mshamba na utakuta haelewi kabisa kuna vyombo hivyo ulivyovitaja vipo kazini24/7 vikiwa na utaalamu na nyenzo za kutosha kufanya kazi hizo.
Hivyo vyombo vinachunguza watu bila hata wao wenyewe kujua wanachunguzwa hata hao wapiga picha na hela vinawachunguza
Kila benk kuna maafisa vipenyo ambao kazi zao ni kuripoti miamala yote ya kiasi kikubwa ya fedha na inachunguzwa legity yake.
Viongozi wengi sasa hivi ni wakurupukaji na wala sio waelewa wanafanya mambo au wanatoa kauli ambazo zinawafanya waonekane kama nu watu wenye uelewa mdogo sana hadi inatia wasiwasi ameteuliwaje kwenye nafasi hiyo
 
Hiyo ndio kazi kiongozi anafanya?
Huwezi kumpangia mtu mzima aishije maisha yake,pesa ni yake shida iko wapi?
Kila mtu ajali mishe zake,na kila mtu aheshimu maamuzi ya mwingine endapo hajavunja sheria.
Wamefanyia kazi pesa zao let them be.
 
Wakamatwe waekeze wamelipa kodi kiasi gani.Kama wamelipa kodi stahiki, waachiwe huru

Tena ilitakiwa sheria ziwe ngumu kweli kweli.Watu hawafanyi kazi halali,wanawaza wizi,utapeli, kuuza madawa ya kulevya na ushirikina wa kutoa kafara watu kwa sababu ya tamaa tu ya pesa wanayotamanishwa na watu wachache.
Wengine wanafanya hivyo ili DM wafatwe na vitoto vya 2000 na wanavichezea sana.
Huu uhuni ukomeshwe
 
Kuna maeneo wanapaswa kuwajibika ipasavyo ila siyo kwenye huu upuuzi.
Viongozi wapenda tension kwenye vitu visivyo na tija ila kufanya madini, mafuta na gas vitulete utajiri nchi aaaaah
 
Viongozi wetu wameshazisoma akili zetu kupenda mambo rahisi rahisi yaaiyokuwa na tija wala hata siwalaumu.

Ndio maana wanazungumza mambo ya kijinga maana hata sisi tunayapenda kuyasikia.

Ukiweka habari ya uvumbuzi wa kemikali fulani itapata wachangiaji wachache kuliko habari ya Zuchu kupata boyfriend mpya, au usajili mpya wa Yanga.
 
Kupiga picha na hela zako kunahujumu vipi uchumi?

Acheni ulofa nyie.
Wanachakaza pesa kwa kuzishikashika.
Pesa hutunzwa bank sio nyumbani maana wanahatarisha maisha yao
Pili wanasababisha sonona kwa wasio na hela kujiona masikini hivyo kupelekea kujinyonga au kufa kwa stress.
Naoendekeza adhabu kali kwa wahusika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…