DC wa Hai Ole Sabaya akiachwa, basi mjue kuna tatizo kubwa huko mbele

DC wa Hai Ole Sabaya akiachwa, basi mjue kuna tatizo kubwa huko mbele

Tatizo naloliona,ni Jiwe kuwapa nafasi Nyeti kama hizo Vijana ambao hawakuwa na maadili yo yote ya kisiasa na kiutumishi.Mimi huyu Sabaya namwona ni Kijana mdogo kupewa nafasi kubwa kama hiyo! Ndiyo mfano wa akina Ally Hapi,Makonda,Gambo,nk Kwa hiyo siyo ajabu kufanya matendo kama hayo! Kwani Mbona wakuu wa Wilaya na Mikoa hawako hivyo?
 
Mungu kapiga mchungaji kondoo hana namna atatawannyika tu.
 
H

Hutaelewa kwa kuwa wewe ni nyumbu
Majini kuna mamba lakini huoni
Muulize mama yako kama mimi ni nyumbuu. Huyo unayemuita bba yako ni wa kufikia, muulize akupe ukweli
 
Nilijiulizaga sana Imekuaja Sabaya kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ?

Kwa wanaomfaha Sabaya walijiuliza sana hilo swali.
 
Duuuh Sabaya Sabaya Sabaya
Sabaya maisha ya staili hii yana mwisho, tubu hizi dhambi Sabaya, utapata mwisho mbaya sana usipotubu
Unajikuta Mungu mtu kisa kuwa DC??
Hajui kuwa kuna laana za watu baki wanaosikitika na maovu yake ...Mungu halali wala kusinzia
 
Kumekuwa na trend za Ole Sabaya kushika kasi kwenye mutandao ya kijamii.

Mengi sana hasa mabaya juu yake yamesemwa sana na kupost video nyingi sana kuonyesha udharimu wa Ole Sabaya.

Na wapinzani wamekuwa ndio wapiga zumari kwenye hii. Kelele hizi zinaweza kuwa ndio kumtangaza sana Ole Sabaya na viongozi wakuu wakapata wasaa mkubwa wa kumaamini na kumpa madaraka makubwa zaidi kwani inaonyesha hataki mchezo anapopewa kusimamia kazi.

Tusishangae kuona Ole Sabaya anakuwa RC kwenye moja ya mikoa mikubwa kabwa Dar, Mwanza na hata Mbeya.

Unaweza shangaa kusikia Ole Sabaya amekuwa hata Katibu Mkuu wa CCM.

Kumsema sana inawezakuwa ndio promotion kwake kwenda juu zaidi
 
Kumekuwa na trend za Ole Sabaya kushika kasi kwenye mutandao ya kijamii.
Mengi sana hasa mabaya juu yake yamesemwa sana na kupost video nyingi sana kuonyesha udharimu wa Ole Sabaya.
Na wapinzani wamekuwa ndio wapiga zumari kwenye hii. Kelele hizi zinaweza kuwa ndio kumtangaza sana Ole Sabaya na viongozi wakuu wakapata wasaa mkubwa wa kumaamini na kumpa madaraka makubwa zaidi kwani inaonyesha hataki mchezo anapopewa kusimamia kazi.
Tusishangae kuona Ole Sabaya anakuwa RC kwenye moja ya mikoa mikubwa kabwa Dar, Mwanza na hata Mbeya.
Unaweza shangaa kusikia Ole Sabaya amekuwa hata Katibu Mkuu wa CCM
Kumsema sana inawezakuwa ndio promotion kwake kwenda juu zaidi
For a stupid mamlaka ya uteuzi. Kuua watu ndiko kumapandishe? kudhulumu wafnyabiashara ndiyo kumapandishe? Kumtesa Mbowe ndiyo kumpandishe?
 
VIDEO YA CCTV CAMERA IKIMUONYESHA MKUU WA WILAYA YA HAI AKITESA MTU NA WATU WAKE.

Diwani Msangi wa Sombetini afunguka juu ya kipigo alichopewa na Sabaya
Philip Kana
4th April 2021

DIWANI wa Kata ya Sombetini, Jiji la Arusha, Bakari Msangi, amefunguka namna alivyoshambuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya akiwa na walinzi binafsi.

Anadai kwamba Sabaya wakati akimshamblia, alikuwa na walinzi wake binafsi sita waliobeba silaha ikiwamo bastola mbili.

Diwani huyo ameiambia SAUTI KUBWA kwamba ameamua kuyasema hayo baada ya Sabaya na wapambe wake kusambaza taarifa kuwa Februari 9, mwaka huu, alipigwa na baaadhi ya watu baada ya kumfumania “akiwa na mke wa mtu.”

Msangi akielezea namna tukio hilo lilivyokuwa anasema, Februari 9, mwaka huu majira ya saa 11 jioni alipokea simu kutoka kwa Mohamed Asaad, akimweleza kuwa mkuu huyo wa wilaya amevamia dukani kwake, hivyo kama anafahamiana naye anaomba akamsikilize na kumsaidia. Assad ni mmiliki wa duka la mapazia la Shaahidi Storea lililopo Barabara ya Nyamwezi karibu na Soko Kuu jijini Arusha.

Msangi anasema: “Mimi nikaenda pale dukani nikakuta mlango wa chuma umefungwa nikagonga hawakufungua, nikaamua kuuvuta juu nikaingia. Kweli nikamkuta Sabaya na vijana wake sita wamewaweka chini ya ulinzi wafanyakazi na wateja waliokuwa kwenye hilo duka, wanawapiga,” anasema Msangi na kuongeza.

“Nikamuuliza Sabaya kuna shida gani? Akaniambia hawa Waarabu ni wahujumu uchumi, wanafanya biashara haramu wanauza dola feki, wanauza bidhaa hawatoi risiti, akaniorodhesha makosa kibao…

“Nikamwambia mimi kama diwani wajibu wangu ni kuwatetea wananchi wa Arusha, lakini wewe hapo ulipo siyo TRA, (Mamlaka ya Mapato Tanzania), siyo Takukuru wala Usalama wa Taifam na siyo polisi, iweje uwanyanyase hawa badala ya kutumia vyombo husika vikaja kuwakamata hawa watu?”

Msangi anasema kuwa kauli hiyo ilionekana kumuudhi Sabaya ambaye bila simile alimgeukia na kuanza kumshushia kipigo.

“Aliwaamuru vijana wake waninyang’anye simu zangu, wakachukua na fedha walizonikuta nazo kama laki tatu na elfu tisini, wakanipiga vibao wakanikalisha chini,” anasema Msangi na kuongeza.

“Walipokuwa wananikalisha, niligoma, wakaamua kunifunga pingu mikononi. Wakaanza kunipiga, nikamwambia Sabaya haki ya Mungu mtaniua, lakini sitaondoka hapa mpaka nisimamie haki ya hawa watu.

“Wakati haya yakiendelea, Sabaya alimchukua mdogo wa mwenye duka na kuingia naye chumba kingine ambako walikuwa wakizungumza. Baadaye nikagundua kuwa alikuwa akimuamuru ampigie simu kaka yake, Asaad ili aje dukani kwake…”

Diwani huyo anasema kuwa iIlipofika saa tatu usiku alimwambia Sabaya awaache, lakini aligoma na baadaye kuwapiga vibao wateja waliokuwamo ndani ya duka na wadogo wa Asaad, kisha aliwaambia waondoke.

“Sabaya akapiga simu kwa OC CID akamwambia kuna watu nimewakamata ni wahujumu uchumi nataka kuwaleta hapo polisi. Wale ndugu zake Assad wawili wakaingizwa kwenye gari la walinzi aliokuwa nao – mabaunsa, mimi nikaingizwa kwenye gari alilokuwa amepanda Sabaya…

(Sabaya)
“Msafara ukaanza kuelekea Central, tulipofika tukamkuta OC CID, Gwakisa kasimama nje anatusubiri na mimi nikataka kushuka, lakini Sabaya akanizuia.”

Diwani Msangi anasema Sabaya alimwambia hajamshusha polisi kwa sababu hajamaliza kazi naye, anataka akamuonyeshe nyumbani kwa Ally Assad Ajirin na kwa kaka yake Mohamed Assad Ajirin. Anazidi kusimulia:

“Tukaenda kwa Ally Assad Ajirin, tukafika tukagonga mlango hawakufungua. Kidogo wakati tunatoka, tukakutana na mzee mmoja anaongea na simu akajua labda ni mzee wa familia hiyo akamkamata baadaye akamuacha” anasema Msangi na kuongeza.

“Tukaondoka tukaenda kwa Mohamed Assad tulipofika akavunja mlango akaingia ndani akawaluta mke wa Mohamed na watoto. Hawakumkuta Mohamed, hivyo tukaondoka.

“Tukatoka tukazunguka mjini mimi nikiwa nimefungwa pingu. Baadaye wakaenda supermarket ya Panone pale Ngarenaro wakanunua vinywaji wakawa wanakunywa, kisha tukaondoka mpaka pale Hoteli ya Tulia, iko pale WhiteRose,”.

“Tulipofika hapo wakaingia ndani wakaniacha mimi kwenye gari wakawa kama wamenisahau. Palepale nikaona mfuko waliokuwa wameweka simu, nikavivuta nikafanikiwa kuchukua simu.

“Simu kubwa nikaiicha ndani ya chupi nyingine ndogo nikaitumia kumpigia mke wangu. Nikamwambia yote yaliyonikuta, nikamwambia anifuate ila aje na jirani yetu hapo nyumbani.

“Baadaye kidogo, Sabaya akatoka akiwa kabadili nguo, mwanzo alikuwa kavaa kaunda suti sasa ametoka kavaa koti, akaja kwenye gari akaniambia nasikia kuwa watu wanakutafuta ni nani, nikamwambia sijui…

“Sabaya akasema itakuwa ana simu huyu embu mpigeni ‘teru’ (mkagueni). Walinikagua, lakini walishindwa kuziona kwa sababu zilikuwa ndani ya suruali.

“Sabaya alimuona mke wangu eneo lile, jirani na gari lake, akahoji akisema ‘huyu malaya anayekufuatilia ni nani?’

“Akawa anawaagiza mabaunsa wake waende wakamchukue, nikawaambia mtamchukuaje mke wangu, baadaye nikaamuriwa kwenda kuzungumza naye nikiwa chini ya ulinzi…

“Sabaya akaja akamtolea mke wangu bastola akamwambia leo naenda kumuua Bakari. Mke wangu akapiga ukunga, Sabaya akaona kuna shida, lakini mimi nikamwambia mke wangu asiwe na wasiwasi kwani hapo walipofika hawezi kufanya chochote nikamwambia akanisubiri Arusha Technical …

“Mabaunsa wakaniingiza kwenye gari tukaondoka tulipofika pale Petrol Station ya Mount Meru, kabla ya taa za barabarani, wakasimamisha gari wakaniambia nishuke nikimbie. Nikagoma, wao wako na bunduki na bastola nakimbia vipi? Wangeweza kunipiga risasi nikawaambia wanipeleke mahali mke wangu yupo…

“Wakaenda wakanishusha pale Arusha Technical ambapo mke wangu alikuwa wakanipiga mkwara. Nikaondoka kufika nyumbani ndiyo nikaanza kusikia maumivu, nikawapigia viongozi wenzangu sikuwapata ….

“Nikaamua kumpigia simu Mkuu wa Mkoa, Iddi Kimanta nikamweleza kila kitu, yule mzee alilia kabisa wakati naongea naye. Akawapigia RPC na OCD akawaeleza kisha akaniambia tukutane Polisi, nilipofika nikawakuta viongozi wamejaa …

“Ilikuwa saa sita usiku, wakaniandikia PF3 nikaenda hospitali kutibiwa, hivi napokwambia naendelea na matibabu na polisi wako kwenye uchunguzi.”

Diwani huyo alisema kuwa hakuweza kutambua namba za gari alilokuwa akitumia Sabaya kwani wakati wakitoka dukani kwa Assad alikuwa ameweka namna za DFP na walipokuwa wakitoka hoteli ya tulia alikuwa amebandika namna za UN.

Kamanda wa Takukuru mkoani Arusha, James Ruge alisema endapo tukio hilo lilitokea, halina uhusiano na taasisi anayoiongoza, na kubainisha kuwa “hiyo ni jinai.”

Sabaya hakujibu simu za mwandishi wetu wala ujumbe mfupi wa simu uliomtaka azungumzir sakata hili na tuhuma hizi.

View attachment 1746414

Halafu Aloyce Nyanda Mtozi anakuja kumtetea huyu Jambazi kisa anapewa fedha za dhuluma kutoka kwake.
 
angalia kitendo alichofanya mkuu wa wilaya Ole sabayi baada ya kuambiwa na boss wake mkuu wa mkoa kwamba wapunguze vitendo vya kukamata watu ovyo, utagundua hapo kuna shida

Kavua miwani akamcheck halafu akacheka kwa dharau daaa ANDAKAVA ana matatizo.
 
Acheni kumwandama Mtumwa, tafuteni aliyekuwa anamtuma, katika mazingira ya kawaida DC wa Mkoa /wilayaY anawezaje kwenda Mkoa X na kuanza kuwa harass wafanyabiashara na kuongea na Vyombo vya usalama bila approval ya DC wa eneo husika?

Mambo haya ni mepesi sana, tutamwonea mtumwa wakati yupo master wake na imeandikwa Mtumwa na amtii bwana wake? Sisi wasahili tunasema 'Mtii kafiri ili upate mkate wako'

Nani alikuwa anamtuma kijana wa watu? Vipi uvamizi wa Clouds saa 4 usiku pamoja na polisi wenye silaha, nani alikuwa nyuma ya pazia?

Hii ndio TASK FORCE za kuwapora wafanyabiashara mali zao,mtiu sio TAKUKURU wala TRA lakini anaingia kwenye maduka kukamata anavyodai ni wakwepa KODI.
 
Huyu mbwa sijui kwanini raia wanamuacha hivi mtu anawezaje kufanya hizi vurugu kwenye duka lako?? Nashangaa saana hata IGP hawezi kufanya huu upuuzii yeye ni nani?? I swear ningekuwa mimi ni mmiliki wa hiyo ofisi sasa ningekuwa nyuma ya nondo na huko hai wameweka turubai nyumbani kwake...kmmmke zake
 
Nimejifunza kitu. Upatapo madaraka isiwe tena fimbo ya kuwachapia unaowatawala.kama hizi tuhuma zote dhidi ya huyu dc wa hai ni za kweli inabidi ajitafakari na pia mamlaka zilizomteua zijiangalie upya kwa aina ya watu wanapowapa majukumu ya kulitumikia taifa
 
Huyu mbwa sijui kwanini raia wanamuacha hivi mtu anawezaje kufanya hizi vurugu kwenye duka lako?? Nashangaa saana hata IGP hawezi kufanya huu upuuzii yeye ni nani?? I swear ningekuwa mimi ni mmiliki wa hiyo ofisi sasa ningekuwa nyuma ya nondo na huko hai wameweka turubai nyumbani kwake...kmmmke zake
Yanasikitisha sana haya mambo ... Kuna clip nimeona yupo na mkuu wa mkoa ..Dah sio kwa dharau zile aisee alizoonyesha [emoji119][emoji119]
 
Kama ilivyokwama mitano ya nyongeza.

falsafa zake ndio zitaendelea kuzaa na nyinyi mpaka mtie akili.
hujasikia monitor wenu anawakumbusha sheria zake jiwe zilizotungwa kubinya watu!!!!

unashangilia tu kifo chake hata huelewi kitu.
 
Duuuh, kazi ipo, wiki hii yote imekuwa n yakuchongeana tuu, watu tangu wajue mama anazinguana na watu baasi kila kitu nikuchongeana tu ili mama asikie , mama nae kapiga kimya Kama haoni, istoshe mama Kesha kataa kusoma jf na fb hata tweeter
 
machozi hayakuwa ya bure alijua master kaondoka mtumwa hana chake tena,mama alishasema matendo yako yatafuatana nawe

masikini wanyonge.

doto akatolewa BOT akatua madini,mkashangilia katumbuliwa.

huyu naye ataporwa UDC ili mfurahi,halafu akawe mkuu wa kitengo cha kupasua kengere za waripokaji.kama kawaida wanyonge mtashangilia oyoooooooo.
 
falsafa zake ndio zitaendelea kuzaa na nyinyi mpaka mtie akili.
hujasikia monitor wenu anawakumbusha sheria zake jiwe zilizotungwa kubinya watu!!!!

unashangilia tu kifo chake hata huelewi kitu.
Falsafa za kutumia nyonyo moja la sidiria kushona barakoa au za kubaki na vima yako?
 
Back
Top Bottom