Pre GE2025 DC wa Longido aliyesema alihusika kutengeneza mazingira ya Madiwani kushinda 2020 atenguliwa

Pre GE2025 DC wa Longido aliyesema alihusika kutengeneza mazingira ya Madiwani kushinda 2020 atenguliwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mh. Rais wetu safiiiii sanaaa, excellent, hawa viongozi wanaoongea hovyo hovyo na kujiona Miungu watu, dawa yao ndio hiyo, piga chini haraka sana, wala hakuna kelele ni kufukuza kazi tu, safi kabisa 👏👏👏
Atapiga chini wangapi?Atafukuza kazi wangapi?
 
Attachments

  • 5811523-6041f5af6e2b5c7600d07027005d6658.mp4
    3.7 MB
“na sasa tumeshafanya huko nadhani mmesikia”
Sasa kama waTanzania hawana uwezo wa kuelewa haya, na CHADEMA nao wakashindwa kuwaeleza maana ya maneno haya wananchi wayaelewe; kutakuwa na sababu zipi za kuwepo kwa vyama vya upinzani hapa nchini. Na kutakuwa na sababu zipi za watu kujihangaisha kwenda kupiga kura?
Ndiyo maana nasema, kama CHADEMA hawawezi kuwaeleza wananchi wakaelewa ujinga huu; ili wananchi hao hao waukomeshe, CHADEMA na wao watakuwa ni matapeli tu kama walivyo CCM.
 
Haikupaswa kuishia hapo ilibdi apelekwe ahojiwe kuhusu aliyoyasema maana yeye kama kiongozi anajua ukweli wa alichokisema
Sasa nani wa kumhoji?ingekuwa wnatoka upande ule mwingine muda huu ungesikia tayari yupo ndani ila kwakuwa ni wao,na wadanganyika walivyo wanaona hilo la kutenguliwa kuwa ni bonge la adhabu wakati sio kabisa haitoshi.
 
Wanahitajika waku wa Wilaya zaidi wa aina hii kujitokeza mbele. Na siyo ma-DC pekee; wajitokeze na wengine zaidi walio husika kwa njia moja au nyingine katika uchafuzi huo.

Nampa pongezi za dhati huyo mTanzania mwenzangu aliye amua kuiweka Tanzania mbele zaidi ya kitu kingine chochote.
Hakika
 
Atapiga chini wangapi?Atafukuza kazi wangapi?

Luka 12:2-4

Neno: Bibilia Takatifu

2 “Hakuna jambo lililofunikwa ambalo halitafunuliwa au siri iliyofichwa ambayo haitajulikana. 3 Kwa hiyo, yote mliyosema gizani yatasikiwa mchana: na yote mliyonong’onezana mkiwa mmeji fungia chumbani, yatatangazwa hadharani.
4 “Nawambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, na halafu basi.
 
Luka 12:2-4​

Neno: Bibilia Takatifu​

2 “Hakuna jambo lililofunikwa ambalo halitafunuliwa au siri iliyofichwa ambayo haitajulikana. 3 Kwa hiyo, yote mliyosema gizani yatasikiwa mchana: na yote mliyonong’onezana mkiwa mmeji fungia chumbani, yatatangazwa hadharani.
4 “Nawambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, na halafu basi.
Absolutely.
 
Hii ngoma imeanza leo na kuisha leo!

Ameongea ukweli umemponza lakini ujumbe umetufikia.
 
Wataanza kuchunga makanwa yao..walisahau ya Nape...
Mzee Mwanakijiji kwanza "Shumalamu". Baada ya salamu naomba nikuombe uwaambje watu wa Serikali kwamba, kabla mtu hajapewa mamlaka apewe elimu hasa ya "Public Speaking". Najua wewe una "connections" na unaaminika Itawasaidia "watoto" wetu ambao sasa hivi ndio wanakasimiwa madaraka. 🙏🙏🙏🙏
 
Luka 12:2-4

Neno: Bibilia Takatifu

2 “Hakuna jambo lililofunikwa ambalo halitafunuliwa au siri iliyofichwa ambayo haitajulikana. 3 Kwa hiyo, yote mliyosema gizani yatasikiwa mchana: na yote mliyonong’onezana mkiwa mmeji fungia chumbani, yatatangazwa hadharani.
4 “Nawambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, na halafu basi.

Ukitafakari kwa karibu zaidi kuhusu jambo hili:
Hakuna wakati mzuri sana kuliko sasa kwa watu wa aina ya huyu bwana, kujitokeza mbele na kutoa mchango wao katika kulinusuru taifa hili na hili janga walilo panga hawa watu.

Binafsi sijui kwa nini huyu DC kaamua kuyasema haya mambo wazi wazi hivi wakati huu. Sijui kama ni kuropoka tu kwa mtu aliye pungukiwa akili (kama Nape Nnauye alivyo fanya)?

Kama kasukumwa na moyo wa kukataa uovu unao fanywa na serikali na chama anavyo vitumikia, mimi nitamsifu sana; na naomba na wengine wengi wajitokeze mbele kufanya hivyo. Kwani wakati mzuri ndio huu.
 
Kwa habari nilizopata huyu kamka nazo.. nape yeye alikuwa amelewa palepale eneo la tukio.. Na kama unavyojua pombe inaleta arrogace
 
Nimekwazika Sanaa....hivi hamna uwezekano Jeshi langu Pendwa
😭😭😭Nchii imeozaaa nimegundua. Tupambane na mambo mengine yanayowezekana🙌🙌
Hawa waneshafitinika hizi sasa wanatoana macho wao kwa wao, na siye tusiowaelewa tunawataka wazidi kuparurana,ili siyee tufike kule tuendakooo.
 
Kwa habari nilizopata huyu kamka nazo.. nape yeye alikuwa amelewa palepale eneo la tukio.. Na kama unavyojua pombe inaleta arrogace
Sema hiviiii kala kavimbiwaaaa,na kwa kuwa ni suala la kurefushaaa kambaa ni rahisiii mnooo
 
Kwa nini atenguliwe kwa kuzisema zile drama hadharani? :AYOOO:
 
yaani samia, mtu akizungumza ukweli anamtengua. Ila mtu akiiba mali za umma anamwambia akajirekebishe na nafasi yake anabakia nayo. Mimi simwelewi bibi yangu jamani...yaani anataka dhambi ailee tu, Mungu anapomtaka mtu wake huwa haangalii yupo wapi..anamuokoa tu chap..mtu anatoka kwenye kundi la wanyang'anyi anakuwa huru. Akatubu kwa Mungu wake sasa...hongera DC mstaafu
 
Bado mchengerwa umeona video yake?
Kuna maswali mengi hapa.

Pamoja na mawakili kupeleka mashtaka juu ya kusimamiwa kwa uchaguzi na Wizara ya Mchengerwa; ambapo sasa ni wazi kwamba mkakati ulikuwa ni haya yaliyo elezwa na DC,... lakini maswali ni: Haya yote yanapo fanyika huko mitaani kwa wananchi, na huko huko pia wapo watu/viongozi wa CHADEMA wakiyaona yote haya!
CHADEMA wanasubiri hadi lini kuyafanya haya kuwa ni mambo muhimu ya kuwaeleza wananchi? CHADEMA wapo kimya kabisa kama muda wa kufanya hivyo bado, au tuseme kuwa siyo mambo ya muhimu kuyanyanyulia bango?
Hali hii inanishangaza sana mimi wakati huu kuhusu CHADEMA.
Kuna nini ndani ya chama hiki wakati huu 'critical' namna hii kwa nchi yetu?
 
Kuna viapo vya kambi jamaa kasahau baada ya kupiga cha Arachuga kama yule best wake aliesema huwa wanaungama baada ya kuiba kura!

Safari ya demokrasia ni ndefu sana, japo tumlaumu mtu mzima unaanzaje kuropoka siri hivyo?!!
 
Back
Top Bottom