Mkuu 'Tindo', nilipo soma tu taarifa za huyu DC, mara hiyo hiyo nikakukumbuka wewe...; unajuwa sababu. Na huyu aliyo yasema ndiyo yanayo halalisha kwa kila hali ile nadharia yako; ya kutojihangaisha kwenda kupanga mstari. Katika hali ya namna hii, hata mimi sina hamu ya kwenda kufanya hivyo.Hata Iddy Amin tunamkumbuka.
Sasa nauliza: kwa nini hawa watu wame wadharau waTanzania kiasi hiki? Hawa wanao amua kubaki nyumbani kwa vile CCM na serikali yake wamekwisha maliza kazi ya kuwachagulia viongozi kwa nini wanaikubali hali hii bila kuhoji?.