PostGE2025 DCP Misime: Hadi sasa hali kiusalama nchini kwetu iko shwari

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Leo Disemba 12, 2025 Jeshi la Polisi limetoa taarifa baada ya saa 24 kupita toka tulipotoa taarifa ya mwisho asubuhi ya tarehe 11.12.2025 juu ya hali ya usalama nchini.

Akitoa taarifa hiyo Msemaji wa Jeshi la Polisi DCP David Misime amesema "Tungependa kuwajulisha kuwa, kwa ushirikiano wa vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na nyinyi wananchi na wadau wengine katika kutimiza jukumu la pamoja la kulinda amani, utulivu na usalama nchini, hadi sasa nchi yetu kiusalama ni shwari na shughuli za kiuchumi na za kijamii ziliendelea vizuri katika mazingira ya amani kwa kipindi hicho cha masaa 24"

Misime ameongeza kuwa, tunapoelekea kwenye siku za mwisho wa wiki, Jeshi la Polisi linazidi kutoa wito kwa kila mmoja kutii sheria sambamba na kushirikiana kwa kila mmoja na nafasi yake, kulinda na kuimarisha amani.
1765530059496.png

1765530080935.png
 
​
TAARIFA KWA UMMA​
Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa baada ya saa 24 kupita toka tulipotoa taarifa ya mwisho asubuhi ya tarehe 11.12.2025 juu ya hali ya usalama nchini. Tungependa kuwajulisha kuwa, kwa ushirikiano wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na nyinyi wananchi na wadau wengine katika kutimiza jukumu la pamoja la kulinda amani, utulivu na usalama nchini, hadi sasa nchi yetu kiusalama ni shwari na shughuli za kiuchumi na za kijamii ziliendelea vizuri katika mazingira ya amani kwa kipindi hicho cha masaa 24.

Tunapoelekea kwenye siku za mwisho wa wiki, tunazidi kutoa wito kwa kila mmoja wetu, kuendelea kutii sheria sambamba na kushirikiana kwa kila mmoja na nafasi yake, kulinda na kuimarisha amani kwani kila mmoja wetu anaihitaji katika maisha na katika shughuli zetu za kila siku.

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama vinaendelea kuwaahidi tutaendelea kulinda usalama wa nchi yetu sote, maisha na mali za kila mmoja ndani ya Taifa letu la Tanzania.

Aidha, tuendelee kuelimishana na kuhimizana kuyakataa yale yote yanayohamasishwa kwa njia mbalimbali na katika maneno ya kubadilisha mbinu kila mara ili kutaka kutuchonganisha na kutujengea chuki kati yetu lengo lao likiwa ni kutuingiza katika vurugu ambazo matokeo yake siyo mazuri kama tunavyo shuhudia katika maeneo mengine duniani.​

Imetolewa na;
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania

Taarifa kutoka Jeshi la Polisi @polisi.tanzania.jpg
Taarifa kutoka Jeshi la Polisi @polisi.tanzania (1).jpg

​
 
Hawa viumbe huwa nikiwasikia na kuwaona huwa najisikia vibaya hadi najihisi kupasuka maini.
 
Police safari hii mishahara lazima muitolee jasho…gen z ndo kwanza wanasuka mipango mipya 🤣🤣🤣
 
​
TAARIFA KWA UMMA​
Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa baada ya saa 24 kupita toka tulipotoa taarifa ya mwisho asubuhi ya tarehe 11.12.2025 juu ya hali ya usalama nchini. Tungependa kuwajulisha kuwa, kwa ushirikiano wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na nyinyi wananchi na wadau wengine katika kutimiza jukumu la pamoja la kulinda amani, utulivu na usalama nchini, hadi sasa nchi yetu kiusalama ni shwari na shughuli za kiuchumi na za kijamii ziliendelea vizuri katika mazingira ya amani kwa kipindi hicho cha masaa 24.

Tunapoelekea kwenye siku za mwisho wa wiki, tunazidi kutoa wito kwa kila mmoja wetu, kuendelea kutii sheria sambamba na kushirikiana kwa kila mmoja na nafasi yake, kulinda na kuimarisha amani kwani kila mmoja wetu anaihitaji katika maisha na katika shughuli zetu za kila siku.

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama vinaendelea kuwaahidi tutaendelea kulinda usalama wa nchi yetu sote, maisha na mali za kila mmoja ndani ya Taifa letu la Tanzania.

Aidha, tuendelee kuelimishana na kuhimizana kuyakataa yale yote yanayohamasishwa kwa njia mbalimbali na katika maneno ya kubadilisha mbinu kila mara ili kutaka kutuchonganisha na kutujengea chuki kati yetu lengo lao likiwa ni kutuingiza katika vurugu ambazo matokeo yake siyo mazuri kama tunavyo shuhudia katika maeneo mengine duniani.​

Imetolewa na;
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania

A moment later
 
Leo Disemba 12, 2025 Jeshi la Polisi limetoa taarifa baada ya saa 24 kupita toka tulipotoa taarifa ya mwisho asubuhi ya tarehe 11.12.2025 juu ya hali ya usalama nchini.

Akitoa taarifa hiyo Msemaji wa Jeshi la Polisi DCP David Misime amesema "Tungependa kuwajulisha kuwa, kwa ushirikiano wa vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na nyinyi wananchi na wadau wengine katika kutimiza jukumu la pamoja la kulinda amani, utulivu na usalama nchini, hadi sasa nchi yetu kiusalama ni shwari na shughuli za kiuchumi na za kijamii ziliendelea vizuri katika mazingira ya amani kwa kipindi hicho cha masaa 24"

Misime ameongeza kuwa, tunapoelekea kwenye siku za mwisho wa wiki, Jeshi la Polisi linazidi kutoa wito kwa kila mmoja kutii sheria sambamba na kushirikiana kwa kila mmoja na nafasi yake, kulinda na kuimarisha amani.
Hakuna usalama wowote, unauua watoto wa watu kwa ukatili uliopitiliza halafu useme kina shwali, subiri wamuue mtoto wako ndipo utaona hakuna shwali yoyote
 
Back
Top Bottom