DED ashinda kesi ya fumanizi/Ugoni Dhidi ya Mfanyabiashara na kupewa Fidia ya Milioni 10

DED ashinda kesi ya fumanizi/Ugoni Dhidi ya Mfanyabiashara na kupewa Fidia ya Milioni 10

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
83,659
Reaction score
90,151
My Take
Nilikuwa sijui kama Ugoni na fumanizi unaweza peleka kesi mahakamani na kudai fidia.

===============
Mahakama ya Rufani imethibitisha hukumu ya fidia ya Sh milioni 10 kwa Mkurugenzi wa Manispaa baada ya mfanyabiashara kukutwa na hatia ya kufanya uzinzi na mke wake.

Mkurugenzi huyo, ambaye wakati huo alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya (DED), aligundua ujumbe uliodaiwa kuashiria uhusiano huo na Mei 11, 2021, alisafiri kwenda Tabora akiwa na mashahidi na polisi. Walimkuta mfanyabiashara huyo na mwanamke huyo wakiwa uchi katika chumba namba 17 cha Star Lodge. Picha na video ziliwasilishwa na kupokelewa kama ushahidi.

Mwanamke huyo baadaye alikiri kuwa na uhusiano huo, huku mfanyabiashara huyo akikana kufanya uzinzi.

Jopo la majaji watatu; Jaji Shaban Lila, Dkt. Benhajj Shaaban Masoud na Jaji Lameck Mlacha, lilithibitisha hukumu ya fidia ya Sh milioni 10 mjini Tabora, Septemba 23, 2026, likieleza kuwa fidia kwa kosa la kushawishi na uzinzi haiwezi kutolewa kwa pamoja pale ambapo uzinzi umethibitishwa.

Wanasheria ongezeni nyama tuelewe zaidi.
 
Huo ushahidi huoni ni kuingilia faragha ya watu wazima? Hiyo haiwezi kuwa kesi?
Hao ni mashahidi waliotumika kutoa ushahidi mahakamani, wewe unataka hiyo kesi isiwe na mashahidi?

Huyo ni mke wa mtu aliyeingilia faragha hapo ni huyo mfanyabiashara.

Mke wa mtu sio sawa na mwanamke anayejiuza unaweza kujibebea tu.

Mke wa mtu ni mali halali ya mume huwezi kumtumia kwa matumizi anayompa mume wake.

Na huyo businessman alijua anafanya kosa ndio maana akampeleka mbali huyo mwanamke.

NB.
I wish huyo mwanamke nae angeamriwa kufidia nusu ya hicho kiwango, kwasababu ni mtu mzima mwenye akili timamu aliyejua vizuri anachofanya ni kosa, ajabu akakubali kusafirishwa kama mbuzi.
 
Back
Top Bottom