Ded-Kilindi Tanga amnyanyasa mwalimu mpaka aache kazi?Mh.Waziri mkuu ingilia kati suala hili.

Nguva Jike

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2018
Posts
1,292
Reaction score
1,867
Habari za jioni wana jamiiforum.

Kwa mwenye ushauri na njia za kumfanya mwalimu huyu aondokane na KERO inayomtesa atoe ushauri hapa.

Kuna mwalimu mmoja pale Kilindi Tanga alikwenda kumripoti mwajiri wake Dodoma tamisemi mwaka 2024 kutokana na mwajiri kutomlipa haki zake mbalimbali.Kuna pesa za matibabu,malimbikizo na uhamisho.Mwalimu aliporudi tu Ded akamwita mwalimu na kumhoji kwanini amekwenda Dodoma na kulalamika? Mwalimu akajibu kuwa amekwenda Dodoma kudai haki.Kwa pamoja Ded na dpeo wakamuahidi kumshughulikia mwalimu ipasavyo.

Tangu siku Ile mwalimu amekuwa katika manyanyaso mfululizo mpaka Leo hii ninapoandika Uzi huu.Moja ya manyanyaso ni kuwa walimu wengine wanalipwa pesa zote za uhamisho wanazodai huku mwalimu huyo anaeteswa analipwa laki mbili ama tatu yaani kidogo kidogo.Viongozi wa CWT ambao walitakiwa kuwapigania wenzao hawafanyi hivyo lakini katika malipo ndio wanalipwa zote ubaguzi wa kiwango Gani huu wa kidini kikabila au rangi ya mtu? Mwalimu huyu amekuwa msaada mkubwa Kwa walimu Kilindi kuliko hata cwt

Toeni ushauri kwa huyu mwalimu asie na connection yoyote hapa nchini.
 
Kama anapata mshahara fresh tu asikilizie, Mimi hapo nyuma kabla ya kuacha kazi, nilikuwa sijawahi kupangiwa kusimamia mtihani wowote wala kulipwa likizo yoyote, sijawahi kuhamishwa popote nilikuwa naishi na mshahara tu na hakuna kilichobadilika, jambo lililonifanya nijiongeze na harakati nyingine
Hili la wenzie kulipwa zote yeye anapewa robo robo Kwa makusudi nalo afanyaje?
 
Halmashauri ni taasisi ya umma.Huyo DED na DPEO siyo wamiliki binafsi wa taasisi.Malipo huja kihadibu/kimahesabu kulingana na madai ya watu kadhaa.Iweje yeye tu asilipwe,alipwe kidogokodogo au kupunjwa?Kuna nini zaidi hapo?Wampe maelezo yanayoridhisha na siyo kumfanya mtu mzima na akili zake kama zezeta tu.Mwalimu huyo,anatakiwa awe anawatangulia akili kwa kuwa na "vielelezo" (kama barua za stahili kulipwa,majibu yao na jinsi alivyowakumbusha kimaandishi kila wakati)vya kuwapiga pini hao watu wazima wahuniwahuni.Baadaye arudi huko TAMISEMI.Asiumie kwa sababu ya mihuni yenye roho mbaya.
NB;Asimuachie Mungu.Naye huchoka.
 
DED NA DPEO waliandikiwa barua na katibu mkuu Tamisemi wakielekezwa kumlipa stahiki zake wakamuita mwalimu ofisini wakamkemea kwanini amekwenda Dodoma? Wakamuahidi kumshughulikia na kweli mpaka Leo hii huyu mwalimu anaishi Kwa mateso Kwa kilio Cha samaki baharini na machozi hayaonekani.Mwalimu kanunua zana za kufundishia za shilingi laki Tano Kwa pesa zake mwenyewe LKN hakuna ofisa Alie support juhudi hizo hata Kwa kumpongeza.Mwalimu ameongea na RC wa Tanga friendly RC akatoa milioni hamsini ikajengwa nyumba ya walimu 2 in 1 lakini Leo kwenye malipo wanamtenga mwalimu wanalipwa viongozi wa CWT ambao yamelala kama mateja hii ndio Tanzania ya Kilindi
 
Habari za jioni wana jamiiforum.

Kwa mwenye ushauri na njia za kumfanya mwalimu huyu aondokane na KERO inayomtesa atoe ushauri hapa.

Kuna mwalimu mmoja pale Kilindi Tanga alikwenda kumripoti mwajiri wake Dodoma tamisemi mwaka 2024 kutokana na mwajiri kutomlipa haki zake mbalimbali.Kuna pesa za matibabu,malimbikizo na uhamisho.Mwalimu aliporudi tu Ded akamwita mwalimu na kumhoji kwanini amekwenda Dodoma na kulalamika? Mwalimu akajibu kuwa amekwenda Dodoma kudai haki.Kwa pamoja Ded na dpeo wakamuahidi kumshughulikia mwalimu ipasavyo.

Tangu siku Ile mwalimu amekuwa katika manyanyaso mfululizo mpaka Leo hii ninapoandika Uzi huu.Moja ya manyanyaso ni kuwa walimu wengine wanalipwa pesa zote za uhamisho wanazodai huku mwalimu huyo anaeteswa analipwa laki mbili ama tatu yaani kidogo kidogo.Viongozi wa CWT ambao walitakiwa kuwapigania wenzao hawafanyi hivyo lakini katika malipo ndio wanalipwa zote ubaguzi wa kiwango Gani huu wa kidini kikabila au rangi ya mtu? Mwalimu huyu amekuwa msaada mkubwa Kwa walimu Kilindi kuliko hata cwt

Toeni ushauri kwa huyu mwalimu asie na connection yoyote hapa nchini.
Kama bado yuko CWT acha anyooshwe tu.
NB,huyu Mwl ni miongoni mwa wanaowabeba watesi wa Taifa hili mabegani mwao kwa nguvu zooote.
 
DED NA DPEO waliandikiwa barua na katibu mkuu Tamisemi wakielekezwa kumlipa stahiki zake wakamuita mwalimu ofisini wakamkemea kwanini amekwenda Dodoma? Wakamuahidi kumshughulikia na kweli mpaka Leo hii huyu mwalimu anaishi Kwa mateso Kwa kilio Cha samaki baharini na machozi hayaonekani.Mwalimu kanunua zana za kufundishia za shilingi laki Tano Kwa pesa zake mwenyewe LKN hakuna ofisa Alie support juhudi hizo hata Kwa kumpongeza.Mwalimu ameongea na RC wa Tanga friendly RC akatoa milioni hamsini ikajengwa nyumba ya walimu 2 in 1 lakini Leo kwenye malipo wanamtenga mwalimu wanalipwa viongozi wa CWT ambao yamelala kama mateja hii ndio Tanzania ya Kilindi
Hizo zana zilikuwa ni zipi mkuu nami nijifunze kidogo?
 
Hayo ndio mambo ya Tamisemi,ukipangiwa kufanya kazi huko uwe mvumilivu kweli kweli lasivyo unaweza kumpasua mtu ubongo.

Aendelee na majukumu yake aache kiherehere serikali haiitaji kusaidiwa Bali serikali ndio inatakiwa isaidie sasa yeye hizo Hela alizonunulia vifaa zilikosa matumizi ama?

Kwanza Bora yeye analipwa nusu nusu Kuna Halmashauri mtu ana miaka 20 kazini na hajawahi kulipwa likizo Wala uhamisho.

Alafu huyo Mwalimu nahisi ni wewe Fanya kazi kijana mengine waachie wenyewe ukiona huwez acha kazi ukafanye unayoyaweza mtaani.
 
DED NA DPEO waliandikiwa barua na katibu mkuu Tamisemi wakielekezwa kumlipa stahiki zake wakamuita mwalimu ofisini wakamkemea kwanini amekwenda Dodoma? Wakamuahidi kumshughulikia na kweli mpaka Leo hii huyu mwalimu anaishi Kwa mateso Kwa kilio Cha samaki baharini na machozi hayaonekani.Mwalimu kanunua zana za kufundishia za shilingi laki Tano Kwa pesa zake mwenyewe LKN hakuna ofisa Alie support juhudi hizo hata Kwa kumpongeza.Mwalimu ameongea na RC wa Tanga friendly RC akatoa milioni hamsini ikajengwa nyumba ya walimu 2 in 1 lakini Leo kwenye malipo wanamtenga mwalimu wanalipwa viongozi wa CWT ambao yamelala kama mateja hii ndio Tanzania ya Kilindi
Inawezekana wewe nawe ni tatizo pia. Nimesoma thread na maoni yako nimegundua hilo.
 
Bora tu walimu wanyooshwe hadi wapate akili.******* sana hawa hutumika kuiba kura kuiwezesha chama dola.nimeshuhudia chaguzi mbili wanaiba mbashara.
 
Mwalimu mwenye mgogoro na mwajiri bado anajitolea laki tano kununua zana halafu anamshawishi RC kujenga nyumba za walimu?Rc katoa wapi hela?
 
Hili la wenzie kulipwa zote yeye anapewa robo robo Kwa makusudi nalo afanyaje?
Aachane nalo tu nikwambie kitu, mwambie hakuna kitu kizuri kama kubadilisha mindset akibadilisha mindset hakuna kinachoshindikana, mwambie atenge laki 3 achukue kuku wa kienyeji hata 30 jike na madume hata watano afuge akitoka saa 8 akimbie kwenye kuku zake watakavyoanza kumutply na kufika kuku 100 awezi kuwaza tena ujinga huo.
 
Hizo zana zilikuwa ni zipi mkuu nami nijifunze kidogo?
Yule ni mwalimu wa msingi katika masomo Kuna kutumia zana za kufundishia nyingi Kila SoMo yeye katika SoMo Fulani kulihitajika zana ya kinanda yaani keyboard 🎹 guitar 🎸 nk vyote hivyo yeye Kwa kupenda SoMo lake lieleweke akanunua vifaa hivyo pale kariakoo daresalam LKN hakuna ofisa yoyote aliepongeza hilo japo wameona.Hii ni roho mbaya katika safari ya elimu kisa walilipotiwa Tamisemi basi wanamfanyia visa labda kisa yeye asili yake sio mtanzania ndio mana hawaoni juhudi zake.
 
Kazi nzuri.
Sasa hivyo vifaa ni vya Mwl au ni ni vya shule?
 
Back
Top Bottom