DED Magu angalia sana Idara ya Elimu Msingi

Hagwila,
Hizo nafasi zilizo wazi za ualimu mkuu na uratibu ni kama migodi kwa DEO Glory na hao wapambe wake wawili Johari na Prisca; ushirika wao huo mimi nauita ni "Utatu Mchafu" na haufai.

Johari na Prisca wamemshika masikio Glory, anakubaliana nao yote wanayomwambia; anashindwa kuelewa kuwa wanamharibia kwa kumfanya stepping stone ili wafanikishe mambo yao.

Nina uhakika, Johari atahakikisha kuwa mwalimu mkuu mpya atakayeteuliwa Bundilya anakuwa Ali, Juma, Rashidi, Fatuma au Hadija; tutafika tu!!
 
Andiko lako mkuu, halina mashiko limejaa chuki binafsi, hoja hapa ni IP?
 
Andiko lako mkuu, halina mashiko limejaa chuki binafsi, hoja hapa ni IP?
Vua miwani yako ya mbao uliyovaa. Mtoa mada katoa hoja na vielelezo kibao kuthibitisha upuuzi wa ofisi ya DEO. Tatzo hii thread ime make impact kubwa kitaani. Naona mb.w.a Glory na johari mmeibuka kuja tetea uozo wao coz U are dinning under their feet.
 
Andiko lako mkuu, halina mashiko limejaa chuki binafsi, hoja hapa ni IP?
Kwa hiyo wewe hujaona matatizo yoyote kwenye andiko langu na wachangiaji wengine eeh?

Kwa hiyo kwako wewe rushwa, dhuluma, mbinu chafu kwenye mitihani kama kupanga wasimamizi, fitina dhidi ya watumishi wenye uwezo, upendeleo kwa baadhi ya watumishi hata wasiomudu majukumu yao, waalimu wanaolazimishwa kutoa shukrani kwa fedha wanazolipwa kwa uhamisho (kama mratibu wa Itumbili), waalimu wakuu kuchangishwa pesa au kupokonywa posho zao ili kugharamia matumizi ya ofisi ya DEO kana kwamba ofisi hiyo haina bajeti yake siyo hoja zinazostahili kulalamikiwa eeh?

Huo ndio ukweli mchungu wa mambo yanayoendelea ofisini kwa DEO Magu, mambo ya hovyo kabisa. Kama unawapenda wanaolalamikiwa, washauri waachane na upuuzi huo maana utawagharimu kama hawajachelewa.

Najua mtu akipenda, chongo huita kengeza; lakini kumbuka mwenye macho haambiwi tazama.
 
Msalimie itumbili, Bubinza, kisamba, nyashana, mwabulenga, kisesa, Ngudu, masanza, sayaka, lubugu, Nsola nk
 
Walimu mnakuwaga watu wa majungumajungu sana sijuwi kwanini.
 
Hizi ni fitina kwakua tu hujapata!! Penye ridhiki hapakosi fitina!!

Ualimu ni kazi ya hovyo sana!
 
Hivi mtu akishakuwa afisa elimu hawezi rudishwa kula vumbi la chaki?
 
Hizi ni fitina kwakua tu hujapata!! Penye ridhiki hapakosi fitina!!

Ualimu ni kazi ya hovyo sana!
Majungu na fitna yako kila mahali mzee

Si umeona juzi kati Hapa IGP anawalalamika baadhi ya maafande wakuu wa mikoa kwa unafiki na kupigana majungu

Majungu yako kila sehemu hata Huko jeshini full majungu

Wizarani iwe ya fedha au afya majungu na fitna kama kawa

Serikalinj majungu na fitna zipo juzi kati Hapa Kuna waziri na mkuu wa mkoa wamepigana majungu bila shaka na fitna wanafanyiana

Akina nancy pelosi wanampikia majungu Trump na kufanya fitna dhidi yake sababu Trump alifanya fitna kwenye uchaguzi mkuu na anamfanyia fitna joe Biden na mwanae

Ukiwa kama binadamu kamili majungu na fitna huwezi ya kwepa hata wewe unaweza kuwa unayafanya ila hakuna wa kukuambia

Usiwaonee walimu kila kada imejaa fitna na majungu

Zahera kafangiwa fitna na majungu Hadi katimuliwa kazi [emoji1787]

Maishs hayaendi bila unafiki-Edo kumwembe
 
There you are kandukamo1; kudos!!
 
Kazi nyingi za halmashauri hasa idara za elimu na afya zimejaa manyanyaso sana.Huwezi kupanda daraja bila kutoa chochote japo hata kwa muhudumu wa ofisi ili faili lako asilipoteze.

Ukija kwa hawa wakubwa wanajua udhaifu wote ila wanalindana sana.Rushwa ya ngono haiepukiki hasa ikitokea maafisa ni wa kiume.Hawa wa kike huwa wasumbufu tu wasiojiamini wala kujali maumivu ya wengine.

Kwa Rushwa ya ngono ni hadi Mungu tu aingilie kati
 
Walimu mnakuwaga watu wa majungumajungu sana sijuwi kwanini.
Mkuu Waterloo, naheshimu sana mchango wa mawazo yako kama mkongwe katika jukwaa hili. Una hakika kwamba malalamiko yanayotolewa dhidi ya maofisa hao wa Idara ya elimu Magu ni majungu? Sijui wewe uko wapi, lakini mimi niko Kisesa wilayani Magu na wala siyo mwalimu; lakini madhira wanayoyapata waalimu hapa wilayani kwetu nayaona, maana wapo miongoni mwetu na tunaishi nao kwenye jamii na wengine ni ndugu zetu!! Hata huyo Salyankanga anaishi hapa Kisesa, namfahamu na yeye ananifahamu katika maisha yetu ya kawaida, japo naamini hanijui kwenye jukwaa hili la JF.
Unapojumuisha tu kwamba waalimu wanapenda majungu huwatendei haki ndugu Waterloo. Hawa ni watumishi wa umma ambao wana wajibu wao kwa mwajiri wao na Taifa kwa ujumla, lakini pia wana haki zao kama watumishi kwa mujibu wa taratibu za kiutumishi.
Mambo mengi yanalalamikiwa na waalimu hawa kwa maofisa niliowataja, ambayo baadhi yake nimeyataja kama rushwa, ubadhirifu, unyanyasaji wa kisaikolojia, kingono, udanganyifu katika mitihani, kudhulumiwa malipo yao ya nauli, likizo, posho mbalimbali kama za madaraka, semina n.k kwa kupunjwa kwa makusudi, kulazimishwa kugawana na maofisa hao, kupewa maagizo nusunusu na ya kujirudiarudia yanayowagharimu waalimu muda na fedha kiasi cha kuwafanya muda mwingi washinde kwenye ma-stationery na ofisini kwa DEO na kushindwa kuwa vituoni mwao n.k.
Mambo yote haya kwa ujumla wake yanashusha morali na tija, jambo ambalo lina athari kubwa kwa hatma ya watoto wetu. Labda wewe watoto wako wanasoma IST, St. Mary's, ISM,IISM, Breuban, St. Constantine n.k. Kama ndivyo, huwezi kuona athari zinazowapata watoto wanaosoma shule za umma kutokana na waalimu wao kukosa morali kwa sababu ya matatizo niliyoyaeleza kwenye andiko hili.
Bado hoja yangu iko palepale, namsihi Mkurugenzi wetu wa Magu DC, ashughulikie udhaifu uliopo katika ofisi yetu ya DEO Magu; hats kama hao maofisa wenye appointments kutoka kwa Katibu Mkuu Tamisemi hawezi kuwaondoa; atumie uwezo wake ili washughulikiwe na waliowaweka hapo. DED ni Mteule wa Rais; yeye ndiye msimamizi wa shughuli za wizara zote za nchi ukiacha chache tu katika wilaya yetu, na mwakilishi wa Rais wetu ni DC ambaye anaingia wizara zote; wote ni vijana mahiri, wasomi wabobezi na wazalendo; kwa nini waachie taswira ya elimu wilayani Magu iharibiwe Glory, Johari, Prisca na wengine wowote wanaofrustrate waalimu na watumishi wenzao mahiri kwa kutokujiamini kwao kwa sababu ya elimu ndogo? No Way!!
 
Ndio ujue sasa hali tetemaa
 
 
Kwanini hao walimu wanaonyanyaswa wasipeleke malalamiko yao kwa viongozi ili wasaidiwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…