namba force,
Ni kweli; acha na mimi nizungumze machache ninayoyajua kuhusu hiyo ofisi ya DEO Magu ambayo imekumbwa na kashfa nyingi tangu enzi za Saryankanga. Huyu DEO wa sasa ni mpiga hela tu; amekutana na mchagga mwezake Johari rushwa mtindo mmoja.
Naanza na mfano mmoja ambao hata DED Lutengano ataukumbuka. Hivi karibuni tu kuna Mratibu (mama mjane) alihamishiwa kata ya Itumbili kwa uhamisho wa malipo. Mama huyo baada ya kulipwa, DEO Glory na timu yake walimtoza yule mratibu pesa kama shukrani kwao!! Mama yule alikwenda kulalamika kwa DED Lutengano; sijui hatua zilizochukuliwa na DED kama zipo.
Wewe mwenyewe DED, siku za karibuni uliitisha kikao cha Finance ambapo wakuu wa idara walikuwepo. Uliwapongeza wajumbe kwa matokeo mazuri ya mitihani ya darasa la VII; na Katibu wa TSD alichangia kwa kuitaka ofisi ya elimu kuwa na ushirikiano miongoni mwao, badala ya kupigana majungu na kuchongeana hadi kufikia kuhamishwa baadhi ya watendaji chapa kazi kama SLO aliyehamishwa alivyopigwa jungu.
Baada ya kikao DEO Glory alimfuata Katibu huyo wa TSD na kuanza kumshambulia kwa maneno; mpaka sasa mahusiano ya watu hao wawili siyo mazuri; lakini pia mahusiano kati ya DEO na Mkaguzi Mkuu siyo mazuri vilevile kwa sababu ya ofisi ya DEO kupanga wasimamizi kwa mapatano na baadhi ya waalimu wakuu ili watahiniwa wa darasa la VII katika shule zao wasaidiwe. Kwa mahusiano haya hafifu kazi zitafanyikaje kwa ufanisi?
Palifanyika semina au kongamano la Juma la Elimu ya Watu Wazima kimkoa hivi karibuni kule Buchosa. Maofisa wanne wafuatao:- SLO aliyehamishwa, Afisa Elimu ya Watu Wazima, DEO Glory na Johari walilipwa posho kwa ajili ya kuhudhuria na kushiriki kongamano hilo la Juma la Elimu ya Watu Wazima.
Waliokwenda Buchosa ni wawilo tu; SLO aliyehamishwa na Afisa Elimu ya Watu Wazima. DEO Glory na Johari hawakwenda Buchosa licha ya kulipwa posho, wala hawakuwa ofisini Magu siku zote za kongamano hilo. Huyo ni ubadhirifu wa mali ya umma.
Uhamisho wa SLO kwenda Misungwi pia ni ubadhirifu kwa sababu umetolewa kwa majungu. Afisa huyo amekaa Magu kwa muda wa chini ya mwaka mmoja toka alipohamia Magu akitokea Ukerewe na alilipwa.
Kwa uhamisho huu amelipwa tena kumhamishia Misungwi kwa sababu tu Glory na Johari wamekwenda kulalamika kwa Afisa Elimu Mkoa Mwanza eti SLO huyo anawanyima raha!! R.E.O. Mwanza nae kwa sababu hao wawili wote ni wapenzi wake (kama hawajui wajijue sasa), akaamua kufanya alivyofanya TAMISEMI hatimae SLO amehamishwa!!
Mhe. Jaffo, Mhe. Ndalichako, Mhe. Mkuchika afande wangu, tafadhali fuatilieni mambo haya; kuna watu bado hawajamwelewa Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Dr. John Pombe Magufuli kwamba dhamira yake kwa dhati ya moyo wake amekusudia kuipeleka mbele nchi yetu.
Baadhi ya watendaji wanafanya yao tu bila kuzingatia Vision, Mission wala Spirit ya Rais wetu. Nitakwenda Magu kumweleza Rais uozo huu siku akija kuzindua mradi wa maji; tutaonana wabaya.