Degree holder nimerudi kusoma VETA, hivi vyeti ni kupiga mikasi

Samahani mkuu ulisoma kozi gani awali?
 
Hongera sana jamaa,kuwa na degree isiwe kifungo,bali Elimu ya juu itufungue vichwa kuangalia fulsa,kuna ubaya gani,Muhandisi wa umeme,nimekosa kazi,nikaamua kusogea VETA pale nikasome ufundi wa kutengeneza madirisha ya aluminium na magril,nijifunze pia ufundi CM,na upigaji picha,
Ebu fikiria nikifungua kijiwe changu,napiga umeme,natengeneza madirisha,natengeneza CM,vile vile hata tender za picha nafanya,harafu mkobani nina driving licence,VIP,utanieleza nini?
 
I wish ningekupa ushauri ila kuna vitu hujaviweka wazi.

Sijajua huko veta ada utalipa sh. ngapi na itakuchukua muda gani. Ila kila mtu sasa hivi anakimbilia huko.
 
BA Archaeology lazima utaabike
 
Kaka nakuunga mkono nenda kasome fani upate ujuzi ,kuna fani ukisoma chuo mtaan huwezi ipata

Mie nimepata degree baada ya miaka sita ndo nikapata kazi ..lakini mtaani nilitunia degree yangu kuishi kwa kufanya nilichosemea ila ni ngumu sana kwa wengi kutokana na ulichosoma kuweza kuishi mtaana kwa elimu yako ....mfano mtu kasoma sociology, procurement, wildlife, mwalimu wa arts ,n.k utasugua sana na unahitaj kupata mtaji mkubwa ilii ufanye kitu ulichosomea

Vijana chagua kitu chenye ukisoma mtaan hukosi mia mia hata kama huna mtaji wowote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…