Demokrasia inavyohujumiwa CCM. Mwenyekiti hana mshindani

CCM wanatumia dola kuikalia Tanzania kimabavu..
Marehemu wetu huyu kama kweli Mungu yupo na zile amri 10 alizompa Mussa bado zinafanya kazi zotee...aisee kama si kuni muda muda huu basi ni sufuria.
 
UNajua Katiba yao inasema nini juu ya hilo? Unawalaumu wafuate ya kwako wakati wao wana utaratibu uliopitishwa? Naona kama kuna kuwashwa washwa!
Katiba inaweza kuwa ya kidikteta!
 
Kinachojalisha ni kufanyika kwa uchaguzi huru na haki na siyo usimikaji kama wa kichifu!
 
Unataka Mwenyekiti Wa chama amfokee [emoji51]Rais wa Nchi.
Chama ni taasisi inayojitegemea ikiwa na wanachama wake na uraisi pia ni taasisi inayojitegemea pia ikiongoza taifa kwa ujumla wake kupitia chama Fulani its better mwenyekiti wa chama awe mwngne tofauti na Raisi.
 
Umetumwa?
 
Demokrasia bongo mpaka sasa ni kiini macho tu
 
Maana nzima ya ccm kufanya rais ndo awe mwenyekiti wa chama kwanza ni hulka yao ya kutaka kutumia resources za nchi vibaya au kwa manufaa ya chama Chao na pili kurahisisha wizi wa kura kupitia vyonbo vya serikali na tatu chama kutotambua wajibu wake kwa serikali basi
 
Mbona hukuyajadili hayo wakati wa mwenyekiti aliyeaga dunia?
Hiki ni kitu kipya kwa Tanzania Rais aliye madarakani kufariki dunia na kuacha ombwe la uongozi kwa muda mfupi. Lakini pia ni wakati muafaka kuwakumbusha CCM kuangalia namna bora ya kuboresha demokrasia ndani ya chama chao na kuwapa nafasi na uhuru wanachama wao kushiriki katika kupata kiongozi wao mkuu.
 
Hadithi nyingiiiii mwishoe jibu hakuna. Du, mlalamishi huyuuuu.

Ngoja nisubiri wanaoijua katiba ya CCM waje wadadafue kiutaalam wa political science.
 
Mbaya zaidi wamewalazimisha wakuu wa vyombo vya usalama kuwa wana CCM ili kurahisisha hujuma!
 
Unapotenganisha kofia kunakuwa na checks and balances vinginevyo mtaishia kuwa na madikteta!

Checks & balances ya taasisi ya Rais na Urais inafanywa na Katiba ya Nchi sio ya chama wala wanachama wenza wa Rais!
 
Kwani NJEMBA hana kadi ili awe Mwenyekiti?
 

Hayo mamlaka ya kiserikali kwa Zanzibar uko na hakika ni ya one hundred percent?

And how about Britain? How do they do it?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…