Demokrasia ni adui wa maendeleo

Tulishakaa chini tukapendeza mfumo wa utawala unaotufaa kupitia Katiba pendekezwa ya Warioba, waambie CCM watekeleze kwanza hilo.
 
Kwenye dictatorship hakuna hata uchaguzi? Kwa mfano leo CCM, CHADEMA na ACT unafikiri wakina nani wanaweza kugombea katika hivyo vyama tumchague kama benovalent dictator mwakani ili nchi itawalike katika mfumo wa benovalent dictatorship?
Ili kufahamu hilo natakiwa nijue maisha kwa undani ya wagombea husika(na sio tu chama), uwezo wao wa kufanya kazi, track record kwenye shughuli zao za siasa, na cha muhimu zaidi ni uwezo wao wa kushiriki vizuri na team. Changamoto ya benovalent dictatorship ni kwamba maamuzi yanafanywa na watu wachache. Kuna benovalent dictators wengine ambao hubadilika baada ya muda na kuacha kuwa benovalent. Kama Tanzania ingefikiria kuwa na benovalent dictatorship basi hili ndilo litakuwa na ugumu kufahamu kuliko vyote
 

..Zimbabwe.

..Mozambique.

..Liberia.

..Siera Leone.

.Na nchi nyingine nyingi ziliongia ktk matatizo makubwa kutokana na udikteta.
 
Ni benovalent dictators gani au nchi zipi waliopatikana kwa njia hii??
 
Mungu mwenyewe hakukubali uhuru alioutaka lusifa. Demokrasia huleta mambo ya hovyo yaonekane yanafaa...Demokrasia ni kama mbwa anavyopotezwa na miluzi mingi
 
Ni benovalent dictators gani au nchi zipi waliopatikana kwa njia hii??
Taarifa hizo sio public ila ni common sense. Una mapendekezo yapi kuhusu upatikanaji wa benovalent dictator?. Je Tanzania inatakiwa kuwa na demokrasia.
 
Dogo ufisadi, wizi, upendeleo, uzembe, kutokuwajibika viko katika mfumo Gani au vinastawi katika mfumo gani?
 
Hoja ya mleta uzi ni mfu. Africa hakuna democracy na hakuna maendeleo either.
Viongizi wa Africa,wakiapishwa hawana tena Cha kuwaza zaidi ya uchaguzi ujao, ayo maendeleo unayoyasema kwa mlolongo huo utayapataje?na ilo ni zao la kulazimisha mifumo isiyoendana na sisi katika nchi zetu kama iyo democrasia. Mtoa mada yupo sawa
 
Democrasia ni nzuri sana kwa nchi ambazo majority wanana elimu ya uraia na kujua nini hasa maana ya democrasia kwa nchi zetu ambazo majority ya watu ni nyumbu democrasia haileti matokea tarajiwa wala haiwezi kuleta uwajibikaji
 
Dogo inaonekana ni mwanafunzi wa mwaka wa 2 political science na unafundishwa na mwalimu aliyekata tamaa hivyo anakufundisha na kukujaza ujinga
 
Lee Kuan Yew alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Singapore kupitia chama cha PAP na katiba ya Singapore haina ukomo wa madaraka kwa waziri mkuu.
LKY alikuwa dikteta jambo ambalo hata yeye binafsi hakuwahi kupinga sifa hiyo na siku zote alikuwa proud kuonekana hivyo na hakuwahi kuipenda demokrasia katika maisha yake.

Nimeweka records sawa
 
Naunga mkono title ya mada hii. Demkkrasia inafaa kwa mataifa yaliyoendelea tayari. Lakini kwetu sisi ni upotezaji wa rasilimali muda, fedha na nguvukazi
Shida ya waafrica ni kukariri, maandiko na mafundisho ya wazungu

Fanyeni utafiti mtagundua mfumo sahihi unaofit Africa badala ya kuanza kuilaumu demokrasia

Wew kama mwanazuoni Ulishawahi
Chambua mifumo yote unayoijua

Uka chukua mazuri ya Kila mfumo ukaunda na kupendeleza mfumo wako mbadala au unnasubiri wazungu wafikirie kwa niaba
 
Wewe unajaribu kutetea nini ? Hivi unaelewa hata nilicho andika na unacho andika hapa ???
 
Democrasia ni nzuri sana kwa nchi ambazo majority wanana elimu ya uraia na kujua nini hasa maana ya democrasia kwa nchi zetu ambazo majority ya watu ni nyumbu democrasia haileti matokea tarajiwa wala haiwezi kuleta uwajibikaji
Ndiyo, uwajibishaji ni muhimu kwenye demokrasia
 
Taarifa hizo sio public ila ni common sense. Una mapendekezo yapi kuhusu upatikanaji wa benovalent dictator?. Je Tanzania inatakiwa kuwa na demokrasia.
Ukiangalia Historia madikteta wengi wamekuwa wanaingia madarakani kwa mapinduzi ,vita, kama falme, kupitia vyama vya kidikteta na wachache kama Hitler huwa wanachaguliwa kabisa kama wanademokrasia katika mifumo ya kidemokrasia kabisa halafu wanageuka kuwa madikteta wakiwa madarakani. Nyie nafikiri mchague hiyo ya mwisho ambayo ni ya bahati nasibu, tafuteni mtu mnayeoona anafaa kuwa dictator mzuri kutoka katika vyama halafu muhakikishe mnampigia kura na anashinda uchaguzi.

Ni mwendawazimu tu ndiye anayeamini Tanzania haipaswi kuwa na demokrasia, mimi sio mwendawazimu.
 
Demokrasia ni Nini ? Na hiki tulichonacho au kiliopo Sasa ndio Demokrasia yenyewe ?


That said hata hio Demokrasia iwe kwenye nini ? Je unaona ni sawa kuwepo kwa Taxation without Representation ? Ingawa Practically hakuna Demokrasia ulimwenguni lakini hata hio iliyokuwepo hapo nyuma it was serving the purpose kwa watu kudhani uamuzi ni wao hivyo kuwepo na Amani


Mwisho kabisa kwa teknolojia tuliyonayo sasa na mambo ya Block Chain na Automation we can have real Power to the People by Automating Democracy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…