Demokrasia ni adui wa maendeleo

Demokrasia ni adui wa maendeleo

Maendeleo yatakuja kutokana na maono na usimamizi wa huyo Dikteta !
Hili jina Dikteta ni jina la kuwahadaa watu ili waingie mkenge kama walivyoingia watu wa Libya !

Hakuna anayehadaika bwana. Vitu viko open.

Kwanini tuweke our destiny kwa mtu mmoja? Maana yake unataka tubahatishe?

Huyo mtu akiwa mjinga maana yake anapeleka taifa zima matopeni. Sasa ndo ujinga gani huo mkuu?

Waafrika mna reasons zenu nyingine za kutokuendelea na zinajulikana lakini msianze kusingizia demokrasia.

Mababu zenu na falme zenu za kizamani mbona hawakuwa wanafuata mfumo huu wa kidemokrasia na bado walikuwa wanajsaidia vichakani hata vyoo walishindwa kutengeneza?

Huo ni uvivu wa kufikiri
 
Kama udictator ndio unaamini unaleta maendeleo, basj africa ilapaswa kuwa mbele sana kimaendeleo maana ndio imejaza madictator..
Nchi inaweza kupata maendeleo ikitawaliwa kidikteta lakini siyo guarantee. Mfano Shelisheli, Libya ya Ghaddafi, labda Misri na Hata Morocco iliyo kifalme. Lakini chini ya demokrasia ni kama haiwezekani kupata maendeleo.
 
Watu wanaiba mali za Umma wanafanya kila aina ya Ubadhirifu lakini wakipelekwa Mahakamani eti kwa sababu ya Demokrasia na Utawala wa Sheria wanashinda kesi kwa kutumia mali hizo hizo walizozikwapua. !

Watu wanavurunda sehemu zao za Kazi kwa kufanya kila aina ya madudu lakini Kiongozi anashindwa kumuwajibisha kwa sababu atakuwa amefanya Udikiteta 🤣😳

Mwamba alijaribu jaribu kidogo tu na mambo yalishaanza kukaa kwenye msitari 😅🙌👍

Watu wanatumbuliwa juu kwa juu hata huko mikutanoni 😳
Hakuna mchezo !
Tena yeye alikuwa na afadhali lakini huko China Korea Japan Vietnam huko huwa wanakula kitanzi tu !

Alivyokufa huyo mtu uliyemtaja hapo nini kimeendelea? Watu hawaibi?

Maana yake kila kitu alichokuwa akikipigania kiliondoka nae.

Ndo udikteta ulivyo. Ukifa hata vitu ulivyovianzisha vinakufa.

Tofauti na democracy na kuwa na taasisi imara zinazowajibika kwa wananchi hata ukifa zinabaki na zitakaa hapo as long they can survive.

Na ndo maana Marekani haitakuja kuanguka sio leo wala kesho.

Meanwhile Saudi Arabia akiingia mjinga mmoja tu anaharibu kila kitu.
 
Uingereza na Netherlands zina monarchie and still ni democracies.

Kusema kuwa Afrika hatujaendelea kwa sababu ya demokrasia ni uvivu wa kufikiri na kukosa akili.

Mobutu Seseseko na Iddi Amin waliongoza kwa mkono wa chuma lakini leo Uganda na Congo ni shitholes.

Reasons on why hatuendelei kama Waafrika zipo na mnazijua acheni kuhamisha magoli.
Sheria ni dhaifu sana kwa sababu ya kufuata misingi eti ya kidemokrasia !
Hivyo watu wanafanya Ukwapuaji na ubadhirifu huku wakijua watatoboa tu !

yule Mobutu ndio maana tukasema hao madikteta wawe ni wacha Mungu Waadilifu na wenye maono yamaendeleo !
Sio mradi tu awe Dikteta !
 
Maendeleo yatakuja kutokana na maono na usimamizi wa huyo Dikteta !
Hili jina Dikteta ni jina la kuwahadaa watu ili waingie mkenge kama walivyoingia watu wa Libya !
Watu wa Uganda hawajaingia mkenge kumuondoa Museveni ambaye yuko madarakani kwa miaka 40. Uganda ina maendeleo??

Theodore Nguema ameitawala Equatorial Guinea kwa miaka 45. Guinea yenye utajiri mkubwa wa mafuta ina maendeleo yoyote zaidi ya kina Baltasar Engonga??

Omar Bongo aliitawala Gabon kwa miaka 42 akafuatiwa na mtoto wake aliyeitawala nchi hiyo kwa miaka 15. Gabon ina maendeleo?

Paul Biya ni mtawala wa Cameroon kwa miaka 43, kuna maendeleo kwenye hiyo nchi?
 
Nd

maana wanatakiwa Madikteta Wacha Mungu, na wawe ni waadilifu na wenye maono ya maendeleo na sio wapenda anasa !
 
Nchi inaweza kupata maendeleo ikitawaliwa kidikteta lakini siyo guarantee. Mfano Shelisheli, Libya ya Ghaddafi, labda Misri na Hata Morocco iliyo kifalme. Lakini chini ya demokrasia ni kama haiwezekani kupata maendeleo.

Kwa hiyo hizo nchi za kidemokrasia na ambazo zimepata maendeleo sio nchi ni vijiji au?

Gadaffi kilichomuua ni huo huo udikteta wake.

Yaani ukishakufa na kila ulichokianzisha kinaenda na wewe kaburini.

I saw it kwa Gadaffi, Jiwe, Mobutu, Assad na viongozi wengi ambao waliendesha nchi kwa mfumo wa kidikteta.

Kusema kwamba demokrasia ndio inasababisha Afrika isiendelee ni kukosa akili.

Nigeria, Uganda, Congo, Burkinafaso, Mali kulikuwa na madikteta wa kufa mtu. Wameendelea?
 
Sheria ni dhaifu sana kwa sababu ya kufuata misingi eti ya kidemokrasia !
Hivyo watu wanafanya Ukwapuaji na ubadhirifu huku wakijua watatoboa tu !

yule Mobutu ndio maana tukasema hao madikteta wawe ni wacha Mungu Waadilifu na wenye maono yamaendeleo !
Sio mradi tu awe Dikteta !

Watu kufanya ubadhirifu sio tatizo la demokrasia.

Ubadhirifu umekuwepo tangu kipindi cha Roman Empire huko na haujaisha hadi leo upo.

Au unataka kuniambia huko Saudia na Iran hamna wabadhirifu?

Ubadhirifu ni nature ya binadamu na unajidanganya sana kama unadhani kuongozwa kwa udikteta ndo utamaliza ubadhiridfu coz history haituambii hivyo.

Laumuni watu mnaowachagua mkishapewa vitenge na af kumi kumi msilaumu demokrasia
 
Alivyokufa huyo mtu uliyemtaja hapo nini kimeendelea? Watu hawaibi?

Maana yake kila kitu alichokuwa akikipigania kiliondoka nae.

Ndo udikteta ulivyo. Ukifa hata vitu ulivyovianzisha vinakufa.

Tofauti na democracy na kuwa na taasisi imara zinazowajibika kwa wananchi hata ukifa zinabaki na zitakaa hapo as long they can survive.

Na ndo maana Marekani haitakuja kuanguka sio leo wala kesho.

Meanwhile Saudi Arabia akiingia mjinga mmoja tu anaharibu kila kitu.
Hiyo ni point lakini ili tuweze kuwa na hivyo ulivyovieleza ni lazima kuwepo na Mkono wa chuma utakao waweka watu kwenye msitari ulionyooka na kisha kuziweka hizo Taasisi imara ulizozieleza !
Kwa mfano Katiba mpya ilishindikana kipindi cha Kikwete kwa sababu mdudu anayeitwa Demokrasia alitumiwa na watu waliokuwa na maslahi binafsi na wala haikuwa kwa maslahi ya Taifa !
 
Nd

maana wanatakiwa Madikteta Wacha Mungu, na wawe ni waadilifu na wenye maono ya maendeleo na sio wapenda anasa !
Endelea kuhamisaha magoli.
Stalin, Mao Zedong, Xi na madikteta wa Korea wanaabudu mungu gani??
 
Ukitaka kumwamini mtoa mada katika familia yako ewe baba tumia demokrasia kila siku tuone kama utaendelea.
 
Nd

maana wanatakiwa Madikteta Wacha Mungu, na wawe ni waadilifu na wenye maono ya maendeleo na sio wapenda anasa !

Kwa hiyo kumbe shida hapa sio demokrasia.

Shida umeshaitaja hapo nilipopa-highlight. Shida umeitaja mwenyewe!

Shida ni uadilifu, kukosa hofu kwa muumba, na kukosa maono. Shida sio demokrasia
 
Watu kufanya ubadhirifu sio tatizo la demokrasia.

Ubadhirifu umekuwepo tangu kipindi cha Roman Empire huko na haujaisha hadi leo upo.

Au unataka kuniambia huko Saudia na Iran hamna wabadhirifu?

Ubadhirifu ni nature ya binadamu na unajidanganya sana kama unadhani kuongozwa kwa udikteta ndo utamaliza ubadhiridfu coz history haituambii hivyo.

Laumuni watu mnaowachagua mkishapewa vitenge na af kumi kumi msilaumu demokrasia
Hajui madikteta wa uarabuni ni mafisadi wakubwa wanaoiba pesa za mafuta na gesi na kujilimbikizia mali huko magharibi kwenye mabenki, real estates, makampuni na timu za mpira.
 
Ukitaka kumwamini mtoa mada katika familia yako ewe baba tumia demokrasia kila siku tuone kama utaendelea.
Demokrasia kwenye familia inakuaje??
Wanafamilia wanakuwa wanalipa kodi(tax) na kuchagua viongozi?
 
Ukitaka kumwamini mtoa mada katika familia yako ewe baba tumia demokrasia kila siku tuone kama utaendelea.

Ndo maana mnachukiwa na watoto wenu mkishazeeka. Watoto hata simu hawawapigii.

Kuongoza kiudikteta sio sifa. Sifa ni kuongoza kwa hekima.

Usichanganye hekima na udikteta
 
Ukitaka kumwamini mtoa mada katika familia yako ewe baba tumia demokrasia kila siku tuone kama utaendelea.
Mbona mamilioni ya familia za Kitanzania haziongozwi kwa demokrasia na bado ni masikini/mafukara wa kutupwa??
 
Watu wa Uganda hawajaingia mkenge kumuondoa Museveni ambaye yuko madarakani kwa miaka 40. Uganda ina maendeleo??

Theodore Nguema ameitawala Equatorial Guinea kwa miaka 45. Guinea yenye utajiri mkubwa wa mafuta ina maendeleo yoyote zaidi ya kina Baltasar Engonga??

Omar Bongo aliitawala Gabon kwa miaka 42 akafuatiwa na mtoto wake aliyeitawala nchi hiyo kwa miaka 15. Gabon ina maendeleo?

Paul Biya ni mtawala wa Cameroon kwa miaka 43, kuna maendeleo kwenye hiyo nchi?

Mtoa mada njoo hapa ujibu hoja hii.
 
Sijui ni ujinga gani unaotaka kuhararisha kuhusu Tanzania.

Countries: Argentina, Australia, Brazil, Canada, China, France, Germany, India, Indonesia, Italy, Japan, Mexico, Russia, Saudi Arabia, South Africa, South Korea, Turkey, the United Kingdom, and the United States

Nchi kariba zote hapa zina historia mbaya ya udikteta na impact yake katika maendeleo yao.

Very weak point.

Kama unataka turudi nyuma kwenye miaka ya 1700 au 1800 ni sawa tu tunaweza

Hata sisi Waafrika tuna historia ya kuwa na machief na wafalme wakatili walioongoza kwa udikteta. Wapo wengi sana.

Lakini je tuliendelea? Hi dunia yote at some point ilikuwa chini ya ufalme na udikteta,

But still hata kipindi hicho cha udikteta Waafrika kimaendeleo tulikuwa bado.

So i dont understand una-argue nini? Like whats your point?
 
Kwa hiyo hizo nchi za kidemokrasia na ambazo zimepata maendeleo sio nchi ni vijiji au?

Gadaffi kilichomuua ni huo huo udikteta wake.

Yaani ukishakufa na kila ulichokianzisha kinaenda na wewe kaburini.

I saw it kwa Gadaffi, Jiwe, Mobutu, Assad na viongozi wengi ambao waliendesha nchi kwa mfumo wa kidikteta.

Kusema kwamba demokrasia ndio inasababisha Afrika isiendelee ni kukosa akili.

Nigeria, Uganda, Congo, Burkinafaso, Mali kulikuwa na madikteta wa kufa mtu. Wameendelea?
Nchi gani ya kidemokrasia imewahi toka kwenye umasikini hadi ikaendelea? Kilichomuua hasa Ghadaffi ni kutaka kuhatarisha petrodollar na si udikteta wake. Ndiyo maana nchi za magharibi zilimpiga mabomu. Kesi yake ni kama ya Venezuela. Pia kuwa na dikteta tu siyo tiketi ya maendeleo, lakini kuwa na demokrasia ni tiketi ya moja kwa moja ya kukosa maendeleo na kurudisha nyuma yale yaliyopatikana.

Misri, nchi ya pili au ya kwanza kwa uchumi barani Africa ni nchi inayoendeshwa kidikteta.
 
Ngozi nyeusi ni case nyingine..hata uje na aina gani ya utawala lazima ufeli tu mana ngozi nyeusi tuna mattizo na laana.

All in all kuna internal na external factors zinazotufanya waafrika tusiendelee,na wengi wetu humu tunazijua fika.
 
Back
Top Bottom