Demokrasia ni adui wa maendeleo

Demokrasia ni adui wa maendeleo

DEMOKRASIA NA NCHI MASIKINI

Leo nakuja tena na hii mada.

Kwanza ijulikane kuwa hakuna nchi masikini imewahi endelea ikIwa chini ya demokrasia. Ukifutilia historia utaona kuwa hakuna nchi imewahi kutoka kwenye umaskini ikiwa inaongozwa kidemokrasia. Nchi zote zilizofanikiwa kutoka kwenye umaskini zimeongozwa kidikteta au kifalme.

Demokrasia ni anasa ya matajiri. Nchi masikini ikiingia kwenye demokrasia inajichimbia kaburi. Kwanza sababu ni kuwa ni gharama kubwa sana kuendesha nchi ya kidemokrasia. Nchi ya kidemokrasia ina walaji wengi sana.

Msomi mmoja alisema kuwa tofauti kubwa ya udikteta na demokrasia ni idadi ya watu unaotakiwa kuwaridhisha ili uendelee kushika madaraka. Idadi hiyo ni kubwa sana kwenye demokrasia. Wanaridhishwa kwa kupewa vyeo vingi vilivyoundwa kwa ajili yao. Na mzigo wote wa kuwalipa na kuwagharamia unaangukia nchi ambayo ni maskini.

Serikali ya kidemokrasia haiwezi kuja na sera za maendeleo ambazo zitawataka wananchi wafunge mikanda. Kuna wakati ili nchi iendelee ni lazima watu wafunge mikanda. Mfano nchi inaweza kusema hatutaagiza ngano ila tutahakikisha tunazalisha wenyewe kiasi cha kututosha. Kwenye nchi ya kifalme au kidikteta hilo linaweza kufanyika na baada ya muda nchi ikajitosheleza kwa ngano. Kwenye nchi ya kidemokrasia ngano ikiadimika wiki tu watu watangia barabarani na kuiangusha serikali. Wapinzani watapiga kelele za ajabu. Rais mwenye maono wa Liberia aliangushwa kwa namna hii na nchi ikachukuliwa na watu wazembe kama Samuel Doe. Ukisema tukuze textile industry yetu hivyo tulinde soko letu watu watazama barabarani na kukunyofoa madarakani. Waliotuletea demokrasia walijua vema wanachokifanya.

Kwenye nchi ya kidemokrasia ajenda kuu ya mtawala ni namna ya kubaki madarakani. Maamuzi yake yote yanazingatia kutimizwa kwa ajenda hii, hata kama yapo kinyume na maslahi ya nchi. Mfalme au dikteta anakuwa yupo imara madarakani. Anaweza kuwaza namna ya kukuza uchumi na hivyo kujiongezea kipato.

Nchi kama S Korea, Singapore, Malaysia na Shelisheli zimeweza kutoka kwenye umaskini kupitia madikteta.

Nchi kama UAE, KSA na Brunei zimeweza kufanya vizuri chini ya Ufame.

Bado hakuna nchi ya kidemokrasia iliyojitoa kwenye umaskini. Kila aina ya utawala ina mapungufu yake lakini demokrasia ni mfumo wa hovyo zaidi.

Habari kubwa kwenye nchi za kidemokrasia si za maendeleo, bali habari kuhusu michakato ya kidemokrasia.

DEMOKRASIA NA NCHI ZILIZOENDELEA

Nchi iliyoendelea na inayofuata demokrasia lazima itarudi kwenye umaskini. Nchi ya kidemokrasia iliyoendelea lazima itageuka ya kisocialist. Yaani wananchi wake watakuwa wanadai huduma kutoka kwa serikali kila leo hadi serikali itashindwa kuhudumia. Wananchi watataka afya bure. Mwanasiasa atakaye waahidi hilo wanamchagua. Kesho watadai elimu bure, kesho kutwa mishahara mikubwa, ruzuku wakulima nk nk. Nchi hizi zinajikuta zina matumizi makubwa kuliko mapato. Na wakati huo huo wanachi wakiwachagua wanasiasa wanaowaahidi kodi ndogo. Mwisho zinajikuta zina madeni wasiyoyaweza na deficit(nakisi) kwenye bajeti. Kaangalie nchi zinazodaiwa madeni ya kutisha, utakuta nchi za kidemokrasia zilizoendelea hasa ndizo zinaongoza kwa madeni, wala si nchi maskini zinazotangazwa kila leo. US deni lake ni asilimia 90 ya GDP yake. UK ni kama asilimia 250 wakati China ni kama 13%.

Hili la nchi kushindwa kumudu gharama limetokea kwa Argentina na nchi nyingi zilizoendelea zinaenda muelekeo huo.

Wafanyakazi wa nchi zilizoendelea na zinazofuata demokrasia wanaunda unions, na kudai mishahara mikubwa, benefits na haki nyingi. Matokeo yake gharama za uzalishaji zinakuwa kubwa na nchi kushindwa kushindana na bidhaa za kutoka mataifa mengine kama China. Matokeo yake viwanda vinafunga.

Gharama za kujenga miundombinu kwenye nchi za kidemokrasia ni kubwa sana. China imeziacha mbali sana nchi za magharibi kwenye suala la treni ziendazo kasi. Sababu kubwa ni mchakato mgumu na gharama kubwa za kufanya hivyo kwenye nchi za kidemokrasia. Kwenye nchi za kidemokrasia ukitaka kujenga kitu utakutana na red tapes za maana. Kila kikundi kitatoa sauti zao. Wenye ardhi watagoma reli isipite kwenye mapori yao au watadai fidia za ajabu na kukupeleka mahakamani juu.

Wengi wape lakini wakati mwingine wengi hukosea vibaya sana. Suala la Brexit ni mfano wa hili. Watu wengi walipiga kura UK ijiondoe EU. Leo hii baada ya athari kubwa za Brexit waingereza wengi wanajuta na kusema kuwa suala la Brexit halikuwa sawa. Mambo ya kitaalamu hayapaswi kuendeshwa kidemokrasia.

Demokrasia haifai kwa nchi maskini. Tukae chini tutafute mfumo mwingine.
Singapore iliendeshwa kwa mfumo gani mkuu
 
Kwa hiyo wale wa LIBYA walikuwa ni vichaa?

Yaani mamilioni ya watu walirogwa to the point wakaanza kuandamana bila sababu za msingi wakijua fika wanaweza kwenda KUFA?

Nimekuuliza swali.

Before uhuru na African societies most hazikuwa na demokrasia hii ya sasa.

Ziliendelea?
Nimekujibu hapo kuwa ziliendelea kwa viwango vyao kwa wakati wao. Unataka kusema jamii za waafrika hazijawahi kuwa na maendeleo huko kale?
 
Tu stick kwenye mada. Mada inasema Demokrasia ni adui wa maendeleo. Na kuwa nchi masikini haiwezi kuendelea ikiwa inatawaliwa kidemokrasia. Una mifano kutoka sehemu mbalimbali duniani inayoonyesha nchi masikini zilizoendelea zikiwa chini ya demokrasia?
Ufaransa
Botswana
 
Sijatoa mifano ya nchi za kidikteta tu. Pale mwanzo nimeandika mifano ya nchi za kidikteta na za kifalme. Na pia kuna nchi kama China na Vietnam ambazo zinaongozwa na vyama.

Watu wa kale, kwa wakati wao waliendelea kwa viwango vyao. Miaka 2000 ijayo USA ya leo itaonekana primitive. So, wakati wa wafalme na machifu tuliendelea. Mifano ipo mingi, mfano bora kabisa ni utawala wa mafarao wa Misri. Unataka kusema enzi za machifu na wafalme tulikuwa hatujaendelea?

Acha kubadilisha hoja mkuu.

Unataka sasa tuanze ku-debate maendeleo ni nini?

Ukweli ni kwamba hata kabla ya kuja demokrasia AFRIKA ILIKUWA MASIKINI.

Katika kipindi ambacho dunia yote ilikuwa in dictatorship mode, still wa Afrika hata vijiko mlikuwa nashindwa kutengeneza.

Maana yake ni kwamba, msisingizie demokrasia.

Kuna sababu zenu za kutokuendelea lakini demokrasia is not one of them.

Nimekutolea mfano wa nchi ambazo hazikufuata demokrasia na bado ni masikini wa kutupa.

This should not be hard for you to comprehend
 
kwenye demokrasia wengi wanagubikwa na uvivu ulikithiri,...kila kitu wao ni kulalamika kwa kuwa wanahaki ya kuongea,....
 
Kidikteta na waziri mkuu mmoja kwa miaka 30, hadi mwaka 1990.
Lee Kuan Yew alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Singapore kupitia chama cha PAP na katiba ya Singapore haina ukomo wa madaraka kwa waziri mkuu.
 
Ufaransa
Botswana
Ufaransa hadi leo ina makoloni. So ni kama nchi mwizi. Botswana Imepiga hatua kulinganisha na zingine, na sifa nyingi zimuendee waziri mkuu wao wa kwanza ambaye alikuwa mwana mfalme, ambaye alitawala kwa miaka 14 hadi kifo kilipomtoa madarakani. Huyu ndiye aliweka misingi kwenye sera za madini zilizofanya Botswana iwe hapo ilipo leo. Hatuwezi sema uchumi wake ulijengwa ikiwa ya kidemokrasia.
 
kwenye demokrasia wengi wanagubikwa na uvivu ulikithiri,...kila kitu wao ni kulalamika kwa kuwa wanahaki ya kuongea,....
Kwa nini kuna nchi za kidekteta zisizo na maendeleo??
 
Lee Kuan Yew alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Singapore kupitia chama cha PAP na katiba ya Singapore haina ukomo wa madaraka kwa waziri mkuu.
Hata Museveni huchaguliwa.
 
DEMOKRASIA NA NCHI MASIKINI

Leo nakuja tena na hii mada.

Kwanza ijulikane kuwa hakuna nchi masikini imewahi endelea ikIwa chini ya demokrasia. Ukifutilia historia utaona kuwa hakuna nchi imewahi kutoka kwenye umaskini ikiwa inaongozwa kidemokrasia. Nchi zote zilizofanikiwa kutoka kwenye umaskini zimeongozwa kidikteta au kifalme.

Demokrasia ni anasa ya matajiri. Nchi masikini ikiingia kwenye demokrasia inajichimbia kaburi. Kwanza sababu ni kuwa ni gharama kubwa sana kuendesha nchi ya kidemokrasia. Nchi ya kidemokrasia ina walaji wengi sana.

Msomi mmoja alisema kuwa tofauti kubwa ya udikteta na demokrasia ni idadi ya watu unaotakiwa kuwaridhisha ili uendelee kushika madaraka. Idadi hiyo ni kubwa sana kwenye demokrasia. Wanaridhishwa kwa kupewa vyeo vingi vilivyoundwa kwa ajili yao. Na mzigo wote wa kuwalipa na kuwagharamia unaangukia nchi ambayo ni maskini.

Serikali ya kidemokrasia haiwezi kuja na sera za maendeleo ambazo zitawataka wananchi wafunge mikanda. Kuna wakati ili nchi iendelee ni lazima watu wafunge mikanda. Mfano nchi inaweza kusema hatutaagiza ngano ila tutahakikisha tunazalisha wenyewe kiasi cha kututosha. Kwenye nchi ya kifalme au kidikteta hilo linaweza kufanyika na baada ya muda nchi ikajitosheleza kwa ngano. Kwenye nchi ya kidemokrasia ngano ikiadimika wiki tu watu watangia barabarani na kuiangusha serikali. Wapinzani watapiga kelele za ajabu. Rais mwenye maono wa Liberia aliangushwa kwa namna hii na nchi ikachukuliwa na watu wazembe kama Samuel Doe. Ukisema tukuze textile industry yetu hivyo tulinde soko letu watu watazama barabarani na kukunyofoa madarakani. Waliotuletea demokrasia walijua vema wanachokifanya.

Kwenye nchi ya kidemokrasia ajenda kuu ya mtawala ni namna ya kubaki madarakani. Maamuzi yake yote yanazingatia kutimizwa kwa ajenda hii, hata kama yapo kinyume na maslahi ya nchi. Mfalme au dikteta anakuwa yupo imara madarakani. Anaweza kuwaza namna ya kukuza uchumi na hivyo kujiongezea kipato.

Nchi kama S Korea, Singapore, Malaysia na Shelisheli zimeweza kutoka kwenye umaskini kupitia madikteta.

Nchi kama UAE, KSA na Brunei zimeweza kufanya vizuri chini ya Ufame.

Bado hakuna nchi ya kidemokrasia iliyojitoa kwenye umaskini. Kila aina ya utawala ina mapungufu yake lakini demokrasia ni mfumo wa hovyo zaidi.

Habari kubwa kwenye nchi za kidemokrasia si za maendeleo, bali habari kuhusu michakato ya kidemokrasia.

DEMOKRASIA NA NCHI ZILIZOENDELEA

Nchi iliyoendelea na inayofuata demokrasia lazima itarudi kwenye umaskini. Nchi ya kidemokrasia iliyoendelea lazima itageuka ya kisocialist. Yaani wananchi wake watakuwa wanadai huduma kutoka kwa serikali kila leo hadi serikali itashindwa kuhudumia. Wananchi watataka afya bure. Mwanasiasa atakaye waahidi hilo wanamchagua. Kesho watadai elimu bure, kesho kutwa mishahara mikubwa, ruzuku wakulima nk nk. Nchi hizi zinajikuta zina matumizi makubwa kuliko mapato. Na wakati huo huo wanachi wakiwachagua wanasiasa wanaowaahidi kodi ndogo. Mwisho zinajikuta zina madeni wasiyoyaweza na deficit(nakisi) kwenye bajeti. Kaangalie nchi zinazodaiwa madeni ya kutisha, utakuta nchi za kidemokrasia zilizoendelea hasa ndizo zinaongoza kwa madeni, wala si nchi maskini zinazotangazwa kila leo. US deni lake ni asilimia 90 ya GDP yake. UK ni kama asilimia 250 wakati China ni kama 13%.

Hili la nchi kushindwa kumudu gharama limetokea kwa Argentina na nchi nyingi zilizoendelea zinaenda muelekeo huo.

Wafanyakazi wa nchi zilizoendelea na zinazofuata demokrasia wanaunda unions, na kudai mishahara mikubwa, benefits na haki nyingi. Matokeo yake gharama za uzalishaji zinakuwa kubwa na nchi kushindwa kushindana na bidhaa za kutoka mataifa mengine kama China. Matokeo yake viwanda vinafunga.

Gharama za kujenga miundombinu kwenye nchi za kidemokrasia ni kubwa sana. China imeziacha mbali sana nchi za magharibi kwenye suala la treni ziendazo kasi. Sababu kubwa ni mchakato mgumu na gharama kubwa za kufanya hivyo kwenye nchi za kidemokrasia. Kwenye nchi za kidemokrasia ukitaka kujenga kitu utakutana na red tapes za maana. Kila kikundi kitatoa sauti zao. Wenye ardhi watagoma reli isipite kwenye mapori yao au watadai fidia za ajabu na kukupeleka mahakamani juu.

Wengi wape lakini wakati mwingine wengi hukosea vibaya sana. Suala la Brexit ni mfano wa hili. Watu wengi walipiga kura UK ijiondoe EU. Leo hii baada ya athari kubwa za Brexit waingereza wengi wanajuta na kusema kuwa suala la Brexit halikuwa sawa. Mambo ya kitaalamu hayapaswi kuendeshwa kidemokrasia.

Demokrasia haifai kwa nchi maskini. Tukae chini tutafute mfumo mwingine.
Changamoto za demokrasia zina dhihirisha kwamba wananchi siku zote hawawezi kuaminiwa kufanya maamuzi sahihi Kwa taarifa walizonazo. Kwa mfano, kwenye chaguzi yoyote wananchi wanafanya maamuzi kutokana na taarifa wanazopata kutoka Kwa vyombo vya habari lakini ila kufanya maamuzi sahihi kuhusu uongozi, wananchi takiwa kufahamu zaidi ya wanacho kiona kwenye runinga. Yaani, maisha binafsi ya wanasiasa ni muhimu katika kufahamu kama wanaweza kuwa viongozi bora. Demokrasia pia huja na urasimu mkubwa katika kufanya maamuzi kwasababu ya mchakato mrefu wa maoni ya watu wengi hata katika kipindi ambacho uhakika wa maamuzi upo. Ila udikteta nao unaweza ukawa na madhara makubwa sana ambayo yanaingilia maisha ya watu ya kila siku tofauti na siasa tu. Ila akipatikana dikteta ambaye ni "benovalent" aliye zungukwa na team imara, maamuzi hufanyika haraka na uendeshaji wa nchi huwa rahisi
 
Ufaransa hadi leo ina makoloni. So ni kama nchi mwizi. Botswana Imepiga hatua kulinganisha na zingine, na sifa nyingi zimuendee waziri mkuu wao wa kwanza ambaye alikuwa mwana mfalme, ambaye alitawala kwa miaka 14 hadi kifo kilipomtoa madarakani. Huyu ndiye aliweka misingi kwenye sera za madini zilizofanya Botswana iwe hapo ilipo leo. Hatuwezi sema uchumi wake ulijengwa ikiwa ya kidemokrasia.
Demokrasia kwako ina maana gani??

Mfano wa nchi gani ambazo unafikiri zina Demokrasia?
 
Tu stick kwenye mada. Mada inasema Demokrasia ni adui wa maendeleo. Na kuwa nchi masikini haiwezi kuendelea ikiwa inatawaliwa kidemokrasia. Una mifano kutoka sehemu mbalimbali duniani inayoonyesha nchi masikini zilizoendelea zikiwa chini ya demokrasia?

Mfano mzuri ni Tanzania.

We are better off ecoomically now than 40 years ago ambapo tulikuwa hatuja-adopt huu mfumo wa demokrasia.

Anglia after the fall of the Soviet Union. Nchi zote zilizo-adopt democracy zina maendeleo makubwa sana compared na zamani wakati wa dictatorship

Baltics, Hungary, Czech, Slovakia, Chile, Estonia Costa Rica etc.

Hizi n baadhi ya nchi ukiangalia before aingie kwenye democracy na baada mambo ni tofauti sana.
 
Changamoto za demokrasia zina dhihirisha kwamba wananchi siku zote hawawezi kuaminiwa kufanya maamuzi sahihi Kwa taarifa walizonazo. Kwa mfano, kwenye chaguzi yoyote wananchi wanafanya maamuzi kutokana na taarifa wanazopata kutoka Kwa vyombo vya habari lakini ila kufanya maamuzi sahihi kuhusu uongozi, wananchi takiwa kufahamu zaidi ya wanacho kiona kwenye runinga. Yaani, maisha binafsi ya wanasiasa ni muhimu katika kufahamu kama wanaweza kuwa viongozi bora. Demokrasia pia huja na urasimu mkubwa katika kufanya maamuzi kwasababu ya mchakato mrefu wa maoni ya watu wengi hata katika kipindi ambacho uhakika wa maamuzi upo. Ila udikteta nao unaweza ukawa na madhara makubwa sana ambayo yanaingilia maisha ya watu ya kila siku tofauti na siasa tu. Ila akipatikana dikteta ambaye ni "benovalent" aliye zungukwa na team imara, maamuzi hufanyika haraka na uendeshaji wa nchi huwa rahisi
Mfano wa nchi gani ambazo kwako zimekuwa na Demokrasia zikapatwa na hizo changamoto?
 
Sheria ni dhaifu sana kwa sababu ya kufuata misingi eti ya kidemokrasia !
Hivyo watu wanafanya Ukwapuaji na ubadhirifu huku wakijua watatoboa tu !

yule Mobutu ndio maana tukasema hao madikteta wawe ni wacha Mungu Waadilifu na wenye maono yamaendeleo !
Sio mradi tu awe Dikteta !
Hivi kusema dikteta awe mwadilifu na mcha Mungu siyo contradiction?

Dikteta ni mtu ambae anachoamua yeye tu ndiyo kifanyike, hakuna kushauriwa.

Ni uadilifu gani wa kudhani wewe ndiyo una akili kuliko watu wote?

Dikteta ni lazima awaue wanaompinga na kumkosoa, ni uchamungu gani wa kuchinja wanaokukosoa?

Inawezekanaje Dikteta awe mwadilifu na mcha Mungu?
 
demokrasia kwa nchi maskini ni kaburi unajizika huku unajiona

yaani nchi kama Tanzania inataka maendeleohalafu unawapa maamuzi watu zaid ya asilimia 30 ya watu(illiterate)uwezo wa kuchagua viongozi wakati hawana uelewa wowote kuhusu uchumi,maendeleo,sayansi ,teknolojia n.k mwisho wa siku unapata viongozi bogus

haya tuchukulie mfano Kenya ameshinda ruto kwa 51 % na Odinga 49% yaani tafsir yake ni kwamba Ruto anaongoza karibu nusu ya watu ambao hawamtaki hiv hapo maendeleo yanakujaje??
🤣🤣🤣🤣 Hapo kila siku ugomvi maana mpinzani wako inaonekana kuwa nayeye ana nguvu ktk jamii so Kesho na Kesho kutwa mkienda tofauti anawaingiza wafuasi wake mitaani nchi inakuwa na chaos
 
Back
Top Bottom