Demokrasia ni kitu cha ovyo sana. Inasababisha kuwa na viongozi wenye maneno mengi, matapeli na waongo kupindukia

Demokrasia ni kitu cha ovyo sana. Inasababisha kuwa na viongozi wenye maneno mengi, matapeli na waongo kupindukia

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Kwenye demokrasia hakuna kitu cha maana huwa kinafanyika. Mnaishia tu kuwa na viongozi waongeaji sana na waongo waongo.

Wanaotatua matatizo kwa maneno na si matendo. Watu wa zamani waliona kabisa ubaya wa huu mfumo. Leo nchi yetu imejaa wapiga maneno, matapeli na waongo-waongo.

Mtu anaweza sema hatuna demokrasia ya kweli lakini kwenye demokrasia ya "kweli" hali ndiyo huwa mbaya hata zaidi.

Rais wa FIFA aliwahi sema kuwa huwa wanaorganize kombe la dunia kirahisi sana iwapo nchi ina strong man.

Mwanazuoni mmoja wa kale alipinga demokrasia kwa kusema kuwa, "Kama mnatafuta nahodha wa meli, mtapiga kura kumchagua au mtatafuta mtaalamu wa kazi hiyo?"

Demokrasia ni janga.
 
democracy is mob rule. A demagogue has higher chance of ruling than an intelligent person. Hebu fikiria asilimia 50.0001% ya watu wapumbavu watawafanya asilimia 49.9999% ya watu werevu wataabike kwa miaka 4/5/7 mbeleni..
Duh ! Hatar sana !!
 
Domokrasia ya kiafrika ni kuipamba Demokrasia ya Magharibi!
Kwamba Demokrasia ni
"Wengi wape"
hata kama wengi hao ni kundi la "Majizi"
Kwamba Demokrasia ni kuachia Magazeti na Ukosoaji,huku watu wakiwa hawana UHURU wa Tumbo zao.

Hawawezi hata kuzipangia tumbo zao milo yenye ubora.

Demokrasia kwao ni kula ili tumbo liifukuze Njaa!

Badala ya kula ili kuijenga Afya ya Miili yao!

Uhuru pekee walionao ni wa kuoa,Kuolewa au kutalikiana!

Hii Demokrasia kwa Africa ni kama imefeli,Africa bado tunastahili kupelekwa ki- Diki- Taita!
 
Mara mia Demokrasia kuliko kuwa chini ya Dictatorship.
 
Kwenye demokrasia hakuna kiti cha maana huwa kinafanyika. Mnaishia tu kuwa na viongozi waongeaji sana na waongo waongo...
Nakubaliana na wewe kuwa demokrasia ina mianya ya kutumiwa vibaya kuliko hata ufalme.

Nawaza namna tuwe na african democracy. Tuwe na madikteta wazalendo(benevolent dictator)
 
democracy is mob rule. A demagogue has higher chance of ruling than an intelligent person. Hebu fikiria asilimia 50.0001% ya watu wapumbavu watawafanya asilimia 49.9999% ya watu werevu wataabike kwa miaka 4/5/7 mbeleni..
Watu hawaelewi hili. Li mtu lenye kuongea sana kwa ushawishi ndilo linapata uongozi. Yaani kigezo ni kuchakata maneno!!? Zamani waroma mtu kuchaguliwa kuwa consular lazima awe alikuwa meonyesha uwezo na kapitia ngazi kadhaa za uongozi. Hata hao walipata viongozi kwa njia bora kuliko sisi. Tumerudi nyuma sana kwa kutumia hii demokrasia ya kiwendawazimu.
 
Domokrasia ya kiafrika ni kuipamba Demokrasia ya Magharibi!
Kwamba Demokrasia ...
Na si Africa tu. Hata huko majuu inawafelisha. Cheki kama BREXIT. Leo karibu asilimia sitini waliopiga kura wanasema Brexit ilikuwa ni makosa.
 
Sisi hatuna demokrasia, lakini mbona bado tuna tuna matatizo mengi sana tu?
Tuna demokrasia uchwara, inatuendesha sana.

Tupo tu tunapiga domo, tunadanganyana na kutapeliana. Hao wenye demokrasia kamili karibu kila jambo linakwama. USA limebaki jeshi tu, karibu kila sekta wanrudi nyuma.
 
Wazungu walijenga nchi zao kwanza ndio wakafikiria demokrasia,nchi kama Russia,German,China,walijenga nchi zao kwanza, Demokrasia ni mtego.
 
Tuna demokrasia uchwara, inatuendesha sana.
Tupo tu tunapiga domo, tunadanganyana na kutapeliana. Hao wenye demokrasia kamili karibu kila jambo linakwama. USA limebaki jeshi tu, karibu kila sekta wanrudi nyuma.

Hatuna demokrasia ya aina yoyote. Hata Kenya wametushinda.
 
Back
Top Bottom