Deni la Serikali hadi Januari 2023 ni Trilioni 76

Deni la Serikali hadi Januari 2023 ni Trilioni 76

Deni la serikali ya Tanzania limeongezeka na kufikia trilioni 76 mpaka Januari 2023 kwa mujibu wa ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania, hi ikiwa ni ongezeko la trilioni 4 toka Septemba 2022. Takribani asilimia 65.2 ya deni hili ni deni la nje huku asilimia 34.7 ikiwa ni deni la ndani ambalo ni jumla ya trilioni 26.4.

Kwa kuendesha miradi mikubwa mikubwa kwa pamoja, ambapo sehemu kubwa miradi hiyo imekuwa ikitumia mabilioni ya fedha za kigeni, Tanzania imejikuta katika shinikizo kubwa la kutafuta mikopo ili kuweza kufidia mapungufu katika bajeti yake.

Madhara ya mtikisiko katika anga ya kimataifa pia yameongeza makali, hii ni kutokana na Tanzania kuhitaji fedha nyingi za kigeni kuagiza bidhaa kuliko fedha zinazoingia kupitia mauzo ya nje.

Mijadala mikali imekua ikiendelea nchini juu ya deni la taifa, juu ya ustahimilivu wake. Kwa kutumia ripoti ya tathmini inayofanywa na Benki ya Dunia, IMF a serikali ya Tanzania, serikali ya Tanzania imekua ikieleza kuwa bado deni la serikali ni stahimilivu.

Hata hivyo wadau wa uwajibikaji wamekuwa wakitaka maboresho zaidi kwenye mfumo wa ukopaji, ikiwemo kuongeza wadau katika Kamati ya Madeni ya Taifa ambapo kwa sasa inaongozwa a Wizara ya Fedha kupitia Katibu wake. Wadau wanaopendekezwa kuongezwa ni Bunge la Tanzania, kama uwakilishi wa wananchi.

Wadau kama Muunganiko wa Azaki Katika Mikopo na Maendeleo (TCDD) wamekua wakishauri kuwepo na mfumo wa kikomo cha kukopa (debt celieng), katika mtiririko mzima wa ukopaji Tanzania.

Chanzo: The Chanzo
Kwa kuwa hakuna atakayegongewa mlango alipe deni hilo..serikali iendelee kukopa tu ..hata tukiuzwa kulipia deni hakuna shida
 
Kwa rate hii, tutakuwa tushapiga mnada Serengeti yote, lile dege kubwa litaenda Kilimanjaro kila mwezi
Naona ni kama wanakopa sana kufanikisha 2025 wapate cha kuongelea, maana wakait huo miradi yote mikubwa itakuwa imekamilika
 
Kwani deni la watu binafsi inalipa serikali? Huu uhuni tu. Wanataka sasa wakakope wahuni hawa kisha serikali ndio idaiwe. Mbona huko zamani awamu zote hatukuwahi kusikia deni la taifa kujumuisha madeni ya watu binafsi?
National Debt vs Gov Debt
 
Kwani deni la watu binafsi inalipa serikali? Huu uhuni tu. Wanataka sasa wakakope wahuni hawa kisha serikali ndio idaiwe. Mbona huko zamani awamu zote hatukuwahi kusikia deni la taifa kujumuisha madeni ya watu binafsi?
Hakuna kitu unajua wewe mbumbumbu wa uchumi, tofauti deni la serikali na deni la Nchi.
 
Kwa sababu akili za Watanzania bado ni ndogo, subiri deni lifike hadi T. 200 ndo akili itakaa sawa.
 
Deni limeongezeka kwa Tril 4 ndani ya miezi 4

Deni halijumuishi Tril 1.3 ambayo tumekopa Mwezi uliopita kutoka WB

Deni hili ni la Serikali tu, tukijumlisha na lile la Sekta Binafsi linafika Tril 98

Maelezo zaidi

View attachment 2534658
inaonekana serikali inaaminika sana kwenye kukopa.

Wangetukopea tu huko na sisi wananchi kwa niaba mm nashida na viela vichache tu..
 
Angalia ripoti ya CAG uone jinsi mikopo ya Covid ilivyopigwa na wajanja. Halafu mnajidai eti tunakopesheka TUAMKE
 
Back
Top Bottom