Deni la Serikali hadi Januari 2023 ni Trilioni 76

Deni la Serikali hadi Januari 2023 ni Trilioni 76

tafaoti ya samia na magu ni usiri tu samia anakopa mchana kweupe magu akikoea kizani lakini kukopa ni kukopa tu awenda kama angekuwepo magu angekuwa kasha kopa zaidi
Sasa kwanini walikuwa wanasema Magufuli amekopa sana?

Kina Zitto wako wapi siku hizi?
 
Ngoja na sisi tuwekwe bond ni upuuzi mtupu, SGR mpk kesho haijaanza kazi
 
Jamaa wanapiga pesa haswa sisi tunashangilia, V8 leo zimejaa Arusha (AICC) utadhani upo Toyota Japani na Rais wa Japan mwenyewe hawezi kununua hayo mashangingi
 
Hongera kwa mkopaji.

Ukiweka na hizi zilizo kopwa Juzi - trion- 78. Hadi 2025 ni zaidi ya triln 100.

Naaseemaajeeee- Wacha tukope tu.
 
Hivi Mkapa aliwezaje kuendesha Nchi Kwa miaka 10 bila kukopa hata sent Tano?

Yaani HAKUKOPA, bt alihakikisha analipa madeni ya watangulizi.

Hivi Nchi hii yenye watu zaidi ya ml 60 tukimtafuta mtu wa aina ya Mkapa tutampata?
 
Hili SGR bado watakopa tu.

Kama fidia ya kufukua makaburi tu toka mwaka jana watu hawajalipwa means hali si hali.
 
Likifikia trilioni 200 ndio kwa mbaali tutaanza kushtuka.
 
Leo litakuwa ni 77 au 78 trillion ukijumlisha na mkopo wa jana wa 1.2 trillion or something.

Halafu Bi Tozo anakwambia ana mpango kuendelea mpaka 2030.

Nimemuona na huyo katibu mkuu kiongozi leo anaonekana ata miaka 50 ya umri hana hiyo ni shida.

Kuna nafasi nyingine maarifa tu USA kazi kama vile elimu, experience, competence skills za kuifanya sio vigezo pekee. Moja ya hizo nafasi ni katibu mkuu kiongozi au majaji, old age ni kigezo muhimu kwa sababu busara pia ni sifa ya kuteuliwa.

Rejea Magufuli yeye mwenyewe alikiri hadharani mara kadhaa Kijazi alikuwa speed governor kwake alipokuwa akitaka kufanya maamuzi huku akiwa na hasira anamtuliza subiri upige; na baadae yeye mwenyewe anaona kweli hayakuwa maamuzi ya busara kwa wakati huo baada ya kutulia.

Maza kaamua kuweka watu ambao wanajua kusema hewala tu katika safari yake ya kuiharibu hii nchi, hayo madeni ni shida ndio maana mafuta duniani kote yanashuka Tanzania ndio yana panda, si ajabu kuna mitozo ya siri humo.
 
Tunadaiwa kiduchu sana, pia Hatupo hata katika nchi 30 zinazodaiwa Afrika, Nchi ya kwanza kwa deni Africa ni Cape Verde, Kenya ipo katika kumi bora za deni, Tanzania ni kama haidaiwi kitu.
 
Swali jingine; Hii wanapoenda kukopa bila idhini yetu, Huwa wanaweka BOND au DHAMANA zipi?

Maana wanatuambia hii ni nchi MASKINI bt hapo hapo wanasema TUNAKOPESHEKA.

Hivi Kuna maskini ANAEKOPESHEKA?

Mbona mtaani maskini akienda bank kukopa pesa na Hana dhamana hutimuliwa?
 
Deni limeongezeka kwa Tril 4 ndani ya miezi 4

Deni halijumuishi Tril 1.3 ambayo tumekopa Mwezi uliopita kutoka WB

Deni hili ni la Serikali tu, tukijumlisha na lile la Sekta Binafsi linafika Tril 98

Maelezo zaidi

View attachment 2534658
Tutalipa tu, si mabarabara, hospitali, standard gauge, madaraja, na mambo lukuki tunayaona yanajengwa
 
Swali jingine; Hii wanapoenda kukopa bila idhini yetu, Huwa wanaweka BOND au DHAMANA zipi?

Maana wanatuambia hii ni nchi MASKINI bt hapo hapo wanasema TUNAKOPESHEKA.

Hivi Kuna maskini ANAEKOPESHEKA?

Mbona mtaani maskini akienda bank kukopa pesa na Hana dhamana hutimuliwa?
Nyinyi wenye akili kubwa na fikra tunduizi ndiyo hamtakiwi nchi hii!
Mimi nimehoji kuhusu ukarabati wa kivuko kwenda Kenya badala ya kumpa Songolo,Msigwa ameni-block!
 
Back
Top Bottom