Deni la Taifa lafika TZS trilioni 91.03

Deni la Taifa lafika TZS trilioni 91.03

Kutokana na deni la Taifa kuwa Shilingi Trilioni 91.03. Kila M-Tanzania anadaiwa Shilingi Milioni 1 na laki 5 Haya Wa-Tanzania tuchange kila mmoja wetu ili tupate kulipa Deni la Taifa. Mwenye kuwa na Ng'ombe,Mbuzi,nyumba mashamba na Vitu vingine auze ili tupate kulipa deni la Taifa letu Serikali ya CCM imeshindwa kulipa hayo madeni kila mwezi Madeni yanazidi kuongezeka kazi kweli ipo. Serikali ya CCM inakopa kila kukicha na pesa hazijulikani zinakwenda wapi? Lohh Majangaa makubwa nchi yetu itauzwa mpaka na Wananchi wake watauzwa kwa wingi wa madeni tunayo kopa kila kukicha.
Wanakopa za safari Hawa
 
Deni la nje ni tilioni 64. Aaaaaah bado tunakopesheka. Tulitakiwa tudaiwe tilioni 160. Mama Samia kopa, ili mradi ela inakuja ndani kwenye mzunguko. Tena kakope EU, maana walitutawala, tunakula chetu hakuna jinsi, tukifilisika Umoja wa Ulaya watatuwezesha( Bailout). Case study ni Nchi ya Ugiliki, ilikopa hadi ikafilisika ikafanyiwa bailout 2, viongozi wabunifu wakaingia, kwa sasa Greece ni taifa lenye uchumi dhabiti Ulaya kiuchumi, hasa kwenye Uchumi gas na utalii. Kuna mataifa hayasongi bila madeni, ubunifu uja ukiwa unadaiwa. Achana na wanasiasa waoga. Pia misaamaa ipo.
 
Kama nchi hii kuna usalama wa Taifa basi ndo muda wao muafaka wa kuchukua hatua na kuliokoa Taifa.

Nchi inateketea mikononi mwao na wao wanaangalia Ila wakumbuke historian itawataja wao kwa kushindwa kutimiza wajibu wao mama/namba moja. Nchi imepoteza mwelekeo, wameingia majangiri na vibaka.

TISS, liokoeni hili Taifa. Msisahau zilitumika nguvu nyingi kuiunda Tanzania na sasa wahuni wanagawana rasilimali za nchi yetu, urithi wetu na urithi wa watoto wetu.

Hawa watoto kesho watakwenda kuwa wakimbizi wapi? TISS
 
Ni kawaida kijana wala usiogope,marekani wanadaiwa hela kibao kuliko sisi
 
Kama nchi hii kuna usalama wa Taifa basi ndo muda wao muafaka wa kuchukua hatua na kuliokoa Taifa.

Nchi inateketea mikononi mwao na wao wanaangalia Ila wakumbuke historian itawataja wao kwa kushindwa kutimiza wajibu wao mama/namba moja. Nchi imepoteza mwelekeo, wameingia majangiri na vibaka.

TISS, liokoeni hili Taifa. Msisahau zilitumika nguvu nyingi kuiunda Tanzania na sasa wahuni wanagawana rasilimali za nchi yetu, urithi wetu na urithi wa watoto wetu.

Hawa watoto kesho watakwenda kuwa wakimbizi wapi? TISS
Tanzania Hakuna Tiss kuna genge la wahuni wa CCM hivyo usitegemee lolote hapo

Pesa ya kuwapa wakuu wa vyombo vya usalama kipindi cha uchaguzi zinatafutwa kwa udi na uvumba kitaeleweka tu

"Taifa la wajinga huvunjika vipande vipande"
 
Kupigana nao siwezi lakini najua mtetezi wetu yupo walahi
Ehh Mwenye Enzi Mungu tuhurumie jamani jamani!
Kama ulivyosema vita vyetu si kwa mwili na nyama bali ni katika ulimwengu wa roho!
Ehh Mwenye Enzi Mungu amka ukatushindie hii vita walahi tusaidie jamani uwiii ehh [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Machozi yetu yamejaa kwenye glasi yako, tuhurumie ehhh Mwenye Enzi Mungu mkuu [emoji31][emoji31]
 
Watakuambia nchi bado inakopesheka hatuko kwenye red line, juzi kapewa heshima ya uchumi, hadi tunakuja kushtuka watakuwa wamashatuuza hadi sisi wenyewe achilia mbali madini na madeni.
Raia huuzwa kila tunapokopa! Raia ndo dhamana na sensa inawabeba zaidi

Swali : unataka kukopa trilion ngapi
Jibu : trilioni 20
Swali: za nini?
Jibu: kujenga mji wa siri kali mtumba Dodoma na soko la urojo na pweza Makunduchi na Mchambawima!

Swali : Dhamana ya mkopo wako unaweka dhahabu au raia?
Jibu : Sensa tumeyaingiza cha kike mabongo yakakaa home tukayahesabu tumeyapata yamefika majitu 60 milioni, haya ndo nayaweka dhamana, ila usiyaamshe!!
Swali : utarudishaje mkopo sasa huna umeme, huna viwanda na huna akili?
Jibu: we ndo huna akili kweli, hivi ukiyakamua tozo majitu milioni 60 mkopo haulipiki? Kweli?

Hitimisho: Nasema mnakopesheka!Haya shime shime wabongo wajinga ndio waliwao njooni mkope mhakikishe deni limefika tr 100 ila kumbuka iko siku mkishindwa kulipa tutaijia dhamana majitu hayo mlioweka rehani tutapeleka China kulima barabara najua we wajomba zako toka Qatar watakuijia!!

Katiba mpya ijayo imzuie kiongozi mkuu kukopa kabla ya kulipa madeni ya nyuma!

Wapi Ndughayii smart boy😎😃😂😁😚😉😀
 
Kama nchi hii kuna usalama wa Taifa basi ndo muda wao muafaka wa kuchukua hatua na kuliokoa Taifa.

Nchi inateketea mikononi mwao na wao wanaangalia Ila wakumbuke historian itawataja wao kwa kushindwa kutimiza wajibu wao mama/namba moja. Nchi imepoteza mwelekeo, wameingia majangiri na vibaka.

TISS, liokoeni hili Taifa. Msisahau zilitumika nguvu nyingi kuiunda Tanzania na sasa wahuni wanagawana rasilimali za nchi yetu, urithi wetu na urithi wa watoto wetu.

Hawa watoto kesho watakwenda kuwa wakimbizi wapi? TISS
Tanzania kuna tiss basi?
 
Back
Top Bottom