Deni la Tanzania sasa lapita la Kenya, ni la tatu Afrika

Tafuta hela *** wewe,Babu zake rostam walitafuta hela kwa miaka 150+,1997 nimefanya kazi kampuni ya rostam CASPIAN mgodini
Babu zako walipovuna sana waliongeza wake na ulevi
kwa hiyo kama umefanya kazi kampuni ya rostamu ndiyo inabadilisha nini? serikali inakopa inampa rostamu anakwenda kujenga kenya badala ya tanzagiza ingawaje fedha ni za tanzagiza, thats evil …
Lini rostam alipewa hela akawekeze Kenya!?..tibu bawasiri Hilo linalokuwasha
 
Sasaa hivi viongozi Hawaibi tena bali wanasonsomola
 
Sijui umechukua takwimu za mwaka gani! Tanzania iliposhindwa kulipa DENI katika kipindi cha Mkapa, DENI lilikuwa dola bilioni 7 na ilishindwa kulipa hadi kuomba clab ya Paris tusamehewe. Hivi sasa DENI ni mara mbili ya like, na wala hakuna maendeleo yoyote ya uchumi wenyewe...sijui tutalipa kwa hela zipi.
Nilishauri wakati Fulani walipopata mkupuo wa dola bilioni 2 Msaada ghafla wa nafuu kutoka Korea, kuwa watumie bilioni 1 kulipa madeni hasa Yale waliyoyakopa kwa gharama kubwa- commercial loans, wakaniona mjinga. Zile zimeliwa bila ya kujulikana zimefanya nini. Waulizeni.
Kwa kukusahihisha, nadhani hesabu zako umeziokota jaani! Eti Kenya inadaiwa bil 3! In fact, takwimu nilizokupa ni za DENI LA IMF pekee. DENI kamili la Tanzania LA nje na ndani ni dola bilioni 50. (Shilingi trilioni 112)...na linazidi kila dakika. Lile LA Kenya ni dola bilioni 92, Uganda $ bi 35, Rwanda $ B 10
Tofauti kubwa- na siye ni kwamba wengine wote wanaona wadaiwa mno, wanazungumzia wasiwasi wao. Lakini sisi tumeshikilia 'twakopesheka'. Ukiongozwa na wapumbavu hutaki dalili ya ujinga!
Ni kweli Misri, Algeria, Morocco...zinadaiwa zaidi lakini 1- nchi hizo zina uchumi mkubwa wa kuweza kulipa, zina viwanda, pia 2- Mara nyingi tunapozungumzia Africa huwa ni hii Afrika Kusini mwa jangwa LA Sahasa. Sisi hatuna uhusiano wa kiungo na nchi za Kiarabu. Zimetupita mbali na akili zao, hata kama Wana matatizo yao, ni afadhali kuliko sisi. Huo ndio ukweli. Si Mmisri ndiye aliyewajengea Bwawa LA Nyerere? Nitajie nchi nyingine ya Afrika nyeusi, Moja tu, inayoweza kufanya hivyo, NAMI nitakuonesha kuku mwenye miguu minne!
 
Mzanzibari anakopa bila woga wala hajui italipwa lini na nani akisubiri miaka yake iiishe huku Zanzibar ikineemka naye na mwanawe huenda wakaishia kwa Wajomba Oman au kwa Sultan Makhtoom Dubai.
Unakopaje kununua mashangingi ya tz shs 450 milions kila moja kwa maelfu kuwapa Rc Dc, Ded ,kila mkoa na wilaya achilia mbali kwenye mawizara huku kumuona daktari tuu kwenye hospital za serikali "unachangia" mpaka shs 35000.
 
Kwa mwendo wa Binti Kiziwi Chura tutavunja rekodi ya dunia kwa deni kupaa kwa kasi ya Artemis II.
 
Shida zinazoenda kwenye maendeleo nish ngapi vile na zinazokwibwa ni ngapi Kuna mchwa mahali
 
Mwenyewe Mh Rais alisema tulitaje kwa dola ili lisionekane kubwa
 
Bora wao waliongeza wake na ulevi kuliko hao kina Rostam kuiba kuua na kufisidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…