Denmark kufunga Ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo 2024

Denmark kufunga Ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo 2024

Wapo sahihi kabisa.Siyo kitu kirahisi kuwa na balozi kwenye nchi zenye ugaidi kama Tanzania.

Si kuna watu kadhaa wapo lockup kwa tuhuma za ugaidi?Na juzi pia gaidi Hamza si aliuweka ubalozi wa ufaransa under presha hadi mlizi wao akauawa?

Nashauri pia nchi nyingine za Ulaya na Marekani wafunge balozi zao pia kwa sababu kuna threat kubwa sana ya security Tanzania kutokana na ugaidi.
Acha kutusagia kunguni 😂😂😂
 
Wapo sahihi kabisa.Siyo kitu kirahisi kuwa na balozi kwenye nchi zenye ugaidi kama Tanzania.

Si kuna watu kadhaa wapo lockup kwa tuhuma za ugaidi?Na juzi pia gaidi Hamza si aliuweka ubalozi wa ufaransa under presha hadi mlizi wao akauawa?

Nashauri pia nchi nyingine za Ulaya na Marekani wafunge balozi zao pia kwa sababu kuna threat kubwa sana ya security Tanzania kutokana na ugaidi.
Mbona afghanistani wanao
 
Mabeberu wote wangefunga tuu balozi zao, na pesa zao wangeenda kuwasaidia maskini wa kwao huko, sisi tuko uchumi wa kati hatutaki misaada.
 
ukisoma humu kuanzia juu, watu wanalalamikia misaada na kusaidiwa tu...dah inasikitisha sana.

kumbe ni vizuri sasa waondoke, ili akili zitukae sawa tujifunze kujitegemea sasa....bila shaka watu watakuwa wabunifu sasa kujiokoa na shida..tukizoea sana kupewa mnafikiri lini tutafikiri na kuishi wenyewe.....ushaona China na Mrusi analazimisha mtu kufungua balozi huko....watu lazima wakuheshimu, heshima hapewi ombaomba...
 
Tanzania si Tanzania tena ...

wallahi nkipata permanent residence nchi ingine nasepa ..

Tushachoka mara hiki mara kile

acha kulialia mtoto wa kiume...watu wako Afghanistan tena khost huko risasi zinalia na suicide bombers everyday, ungekuwa yemeni au syria allepo, fallujah Iraq huko ungesemaje....acheni kwenda kujazia watu wingi kwenye nchi zao ilihali mnashindwa kujenga kwenu kwa kuisingizia CCM....kumbe wazembe wenyewe mnapenda mteremko mteremko vijana...

wenzenu wanatoboa maisha hapahapa kila siku, indians, arabs na somalis wamejaa na nowa nigerians, cameronians, senegalese wanamiminika hapa na wanatoboa wenyeji mnabaki mnalilia oooooh CCM kila kukicha....sasa si mkomae muitoe kwa manufaa ya vizazi vyenu...
 
acha kulialia mtoto wa kiume...watu wako Afghanistan tena khost huko risasi zinalia na suicide bombers everyday, ungekuwa yemeni au syria allepo, fallujah Iraq huko ungesemaje...
Sasa serikali ya ccm kujenga vyoo tu vya watoto mashuleni kupitia kodi za wananchi mmeshindwa,mnaweza nn nyie sasa?
 
Dar es Salaam. Baada ya kuwapo kwa takribani miongo sita, Denmark imetangaza kuufunga ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo mwaka 2024, huku sababu zikitajwa kuwa ni kuendana na mpango wa nchi hiyo katika masuala ya kimataifa.

Mbali na Tanzania, nchi hiyo pia itafunga ubalozi wake nchini Argentina, Ubalozi mdogo wa Chongqing nchini China na ujumbe wa biashara huko Barcelona (Uhispania) na inaelezwa kuwa jumla ya uwakilishi 16 na ofisi tisa katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje huko Copenhagen zitaimarishwa.

Uamuzi huo ulitangazwa leo Ijumaa Agosti 27, 2021 na Waziri wa Mambo ya nje wa Denmark, Jeppe Kofod.

Waziri huyo amesema hayo ni matokeo ya sehemu ya marekebisho ya Denmark ya uwapo wa kimataifa. Amesema marekebisho haya yanajumuisha kuongezeka kwa ujumbe wa kidiplomasia uliopo na kufungwa kwa zingine.

Amesema huduma za kigeni za Denmark zinaandaliwa upya kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali.

“Upangaji upya unamaanisha uwakilishi zaidi utaboreshwa pamoja na mambo mengine, kazi ya Denmark katika EU, NATO, UN, Arctic, Afrika na juhudi za usafirishaji,” amesema waziri huyo na kuongeza:
“Kipaumbele changu cha kwanza kama Waziri wa Mambo ya Nje ni kuhakikisha usalama na usalama wa ndani katika ulimwengu ambao demokrasia, haki za binadamu na maadili yetu yako chini ya shinikizo. Mabadiliko haya lazima yasaidie kulenga juhudi tunazofanya nyumbani na nje ya nchi, ili tuweze kufanya tofauti kubwa iwezekanavyo,”

“Uamuzi wa kufunga Ubalozi jijini Dar es Salaam ni matokeo ya marekebisho ya vipaumbele vya serikali ya Denmark kwa ushirikiano wa maendeleo kama ilivyoainishwa katika mkakati mpya wa ulimwengu, 'The World we share',” imeeleza taarifa hiyo iliyowekwa katika tovuti ya ubalozi wa nchi hiyo Tanzania.

Amesema mkakati huo mpya una msisitizo mkubwa katika kushughulikia udhaifu, nchi zilizo kwenye mizozo au changamoto za uhamaji na uhamiaji. Barani Afrika mwelekeo zaidi utakuwa Sahel na katika pembe ya Afrika.

“Kutokana na hali hii, Serikali ya Denmark imeamua kumaliza ushirikiano wa maendeleo baina ya nchi mbili nchini Tanzania na kufunga Ubalozi wa Denmark jijini Dar es Salaam mnamo 2024 na huu haukuwa uamuzi rahisi kufikiwa,” imesema taarifa ya Ubalozi huo.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa Denmark itaheshimu ahadi zilizokubaliwa za kifedha na shughuli ya kufunga ubalozi imetengewa fungu ili kuhakikisha mchakato huo unakamilika vizuri.

“Denmark bado imejitolea kuendelea kufanya kazi kwa karibu na Tanzania katika ngazi ya nchi mbili na kwa kuzingatia maswala mapana ya kikanda na kimataifa,” imeeleza taarifa hiyo.

Akizungumza leo kwa simu, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amesema bado hajapata taarifa hiyo, anaifuatilia na Msemaji wa Serikali Gerson Msingwa naye pia amesema vivyo hivyo na kuongeza kuwa Serikali ikishapata taarifa itatoa tamko.
 
Mbali na Tanzania, nchi hiyo pia itafunga ubalozi wake nchini Argentina, Ubalozi mdogo wa Chongqing nchini China na ujumbe wa biashara huko Barcelona (Uhispania) na inaelezwa kuwa jumla ya uwakilishi 16 na ofisi tisa katika makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje huko Copenhagen zitaimarishwa.
 
Angekuwepo
Akizungumza leo kwa simu, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amesema bado hajapata taarifa hiyo, anaifuatilia na Msemaji wa Serikali Gerson Msingwa naye pia amesema vivyo hivyo na kuongeza kuwa Serikali ikishapata taarifa itatoa tamko.

Tafsiri ya kutoka lugha ya Kiingereza imechakachuliwa, wanaJF someni taarifa rasmi ya wizara ya mambo ya nje ya Denmark:
 
👆👆
Maneno mazito toka kwa waziri wa mambo ya nje wa Denmark .


1630108458353.png

MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS OF DENMARK​

Kofod presents changes in the Danish Ministry of Foreign Affairs​

27.08.2021 12:05
The Danish foreign service is to be restructured in order to be able to deliver on the Government’s priorities.

The restructuring means, among other things, that more of our missions will be bolstered, for example with regard to Denmark’s work in the EU, NATO, the UN, the Arctic, Africa, as well as with regard to our export initiatives. In all, 16 missions and 9 departments in the Ministry of Foreign Affairs’ headquarters in Copenhagen will be strengthened.

- My first priority as Minister of Foreign Affairs is to ensure the security and safety of the Danish people in a world where democracy, human rights, and our values are coming under increasing pressure.

This reorganisation is to help us target the efforts we make, both here at home and out in the world, so that we can make the biggest possible difference. The grave development in Afghanistan the last couple of weeks calls for reflection, and we need time to digest and analyse this in cooperation with the Danish Parliament.

Following that process, the government will at a later stage present a new foreign and security policy strategy, said Minister of Foreign Affairs Jeppe Kofod.

Prior to the reorganisation of the foreign service, the most comprehensive analysis of the work and the structure of the Danish foreign service since the Foreign Commission in 1989/90 at the end of the Cold War was carried out. The reorganisation will contribute to the implementation of Denmark’s new strategy for development cooperation "The world we share".

In connection with the reorganisation, the embassies in Argentina and Tanzania are also being closed, along with the Consulate General in Chongqing (China) and the trade mission in Barcelona (Spain). In addition, a number of efficiency measures will be carried out, for example in the areas of energy, procurement and properties.

Source : Kofod presents changes in the Danish Ministry of Foreign Affairs
 
Haitachukua muda, tusubirie kusikia toka Finland, Sweden na Norway.

Chini ya utawala huu primitive, wa mabavumabavu wa CCM, hakika kila siku itakuwa aheri ya jana.

Tanzania haiwezi kuchangamana na Dunia ya watu wastaarabu wanajua thamani ya utu wa kila mwanadamu.
True Mkuu ndo kinachofuta...
 
Back
Top Bottom