Denmark kufunga Ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo 2024

Denmark kufunga Ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo 2024

Kushinda Kenya ambayo inasumbuliwa na Alishabab?

Mbona huko hawafungi?

Hawa mabeberu wakigundua ka nchi kenu watu wake waoga wa maisha, wanapenda kulialia, wasumbua kishenzi!

Acheni ujinga, wafunge waondoke tu, kwa nini tulielie bhana
Halafu yawezekana wewe ndiye Mshauri wa Mama Tozo.
 
Wapo sahihi kabisa.Siyo kitu kirahisi kuwa na balozi kwenye nchi zenye ugaidi kama Tanzania.

Si kuna watu kadhaa wapo lockup kwa tuhuma za ugaidi?Na juzi pia gaidi Hamza si aliuweka ubalozi wa ufaransa under presha hadi mlizi wao akauawa?

Nashauri pia nchi nyingine za Ulaya na Marekani wafunge balozi zao pia kwa sababu kuna threat kubwa sana ya security Tanzania kutokana na ugaidi.
Kweli walifanya ovyo kusema mbowee gaidi
 
My first priority as Minister of Foreign Affairs is to ensure the security and safety of the Danish people in a world where democracy, human rights, and our values are coming under increasing pressure.”

Hii hapa ndiyo sababu ya msingi ya Dernrnark, kuona kuna haja ya kufunga ubalozi wake wa Tanzania.

Tanzania chini ya CCM isiyotambua demokrasia, haki za raia wala uhuru wa vyombo vya habari, haina mwanga wowote. Giza totoro mbepe ya safari.

Dernmark, Finland, Sweden na Norway ni wadau wakubwa wa maendeleo wasio na masharti magumu na wenye ustaarabu wa hali ya juu. Ndiyo mwisho wa misaada ya DANIDA. Mambo ya chanjo za watoto itakuwaje?
 
Mwaka jana walishatuweka kwenye mpango wa kupunguziwa au kukatiwa misaada kutokana na kuzorora kwa demokrasia nchini
Haitachukua muda, tusubirie kusikia toka Finland, Sweden na Norway.

Chini ya utawala huu primitive, wa mabavumabavu wa CCM, hakika kila siku itakuwa aheri ya jana.

Tanzania haiwezi kuchangamana na Dunia ya watu wastaarabu wanajua thamani ya utu wa kila mwanadamu.
 
Si tuliwatangazia wenyewe tuna Magaidi humu kwetu?

Hawakuamini ,tukaamua kufanya show ya kweli pale salender chini ya Sterling Hamza.

Sasa vile viposho vya mashirika ya kidenish yamekauka
😂 😂 😂
 
Nchi nyingi zitafunga balozi zake huwezi kuwa na ushirikiano na nchi inayovunja haki za kiraia na wanasiasa wa upinzani.
Huu uwendawazimu tunaouendekeza wa kuona mwana-CCM ni binadamu zaidi na mwenye haki zaidi kuliko raia wengine wote, malipo yake tutayapata.

World Bank inasema kuwa mwaka 2020 uchumi wetu ulikua kwa 1.9%, sisi kwa kutumia takwimu za akina Polepole tunasema ulikuwa unakua kwa 6%!!
 
Hao wazungu na misaada yao feki ndio waliotudumaza hadi tukawa maskini namna hii. Misaada yao wanaileta na viajenda vyao vilivyojificha, mwisho wa siku unashangaa hakuna cha maana pesa imefanya zaidi ya kutengeneza watu mandondocha wanaofikiri nchi hujengwa kwa slogans za human rights, gender na freedoms of speech.
 
tuache kulialia na kutegemea watu kujenga nchi zetu.....wao walijengewa na nani...tujikaze watoto wa kiume tujenge Taifa letu nalo siku tukifunga ubalozi huko nao watetemeke.... kama wanaume wote tunaona na kukubalian CCM ndio shida tunashindwa nini kuitoa kwa kuivimbia ili tuache kulia lia kwa wazungu na kulilia passport zao ilihali mnakwetu na wenzenu wanakwao babu zao walikujenga...Jengeni kwenu watoto wenu wawe proud na passport za kwao...
Sawa tutajenga kwa Tozo
 
Pamoja na mbwembwe zote za Mula mula bado nchi moja inaamua kufunga ubalozi wake?....Tuelewe sasa kuwa vyuma vimebana hadi huko ulaya... hakuna tena "Free lunch" kama enzi zile!. Cha msingi tuelewe kuwa tuko sasa uchumi wa kati hivyo tunapaswa kujitegemea.
 
Mnaondoka,,but mutamkumbuka Mh rais SSH. Mama mwenye hekima na busara. Allah akuongoze kwenyi majukumu yako mama.
 
Back
Top Bottom