Deo Kisandu kafungwa jela?

Angalia profile yake , nyuzi zake full comedy halafu comedy serios jinsi matukio anavyopangilia na anavyojibu maswali sometimes unaweza kusema jamaa ni mzima ila anajichetua tu kama Maghayo The Mongo Barbarian.
 
Aure mkuu kama sasa hv tunatakiwa tuwasiadie Lucas Mwashambwa na Tlaatlaah nadhani na wao wanapaitia changamoto
 
Familia yake ilishindwa kujua kuwa ndugu yao hayupo sawa mentally

Mimi nilimuona tangu 2017 na nilisema Kama kuna ndugu zake waangalie njia bora za kumuweka karibu
 
Ishu sio kuuza kitanda tu nimesoma hiyo nakala ya hukumu ya rufaa yake kulikuwa pia na ishu ya jamaa kutaka kumpa talaka mke wake ila mama hataki.
Pia kuna ishu ya jamaa kutaka kuwa mbunge ila mama kazima nyota .
ila kwa ujumla jamaa hayupo sawa lakini mbona alishaonyesha vyeti vyake kwamba afya yake ya akili ipo sawa?
 
Ndiyo maana hasikiki kwa post zake humu zenye utata na ukakasi mkubwa.
Lakini kwa watani zangu wasukuma imani kama hizo zipo hata kwa wasio na changamoto ya ugonjwa wa akili.
 
Hebu wadau humu tumfanyie mpango wamchomoe huko
Humu tunajuwa kuna mawakili
Wazuri tu wanaweza wakajitolea

Ova
 
Jamii haipo informed.
Masikini mama yake, huyu mama kwa uzoefu wangu alikaa na ndugu wakaamua kumfungulia hii kesi kwa nia njema kabisa ya kumuokoa, kwa uzoefu nilio nao, itakuwa Deo alianza kuwa violent mtaani kiasi watu walishapanga kumfanya vibaya au hata kumuua kabisa.
Kitendo cha huyu mama kumfungulia hii kesi ilikuwa ni mkakati wake kumuondoa mtaani akafungwe akiamini huko atakuwa salama zaidi.
Kumuanzishia matibabu mgonjwa wa akili nchini Tanzania ni kati ya vitu vigumu sana kuwezekana. Mtu anakuwa violent mnaenda kumpeleka mnashangaa jioni au kesho yake wamemuachia na amerudi nyumbani, wakiwa wamemfungashia dawa. Labda uwe na connections otherwise ni ngumu sana mgonjwa wako kupokewa na kupewa huduma stahiki. Hivyo kwenye issue ya Kisandu ndipo wanafamilia hukutana na kujadili na ili kumuokoa na kuhakikisha ndugu yao anakuwa salama huona ni afadhali wamtungie hata kesi ili afungwe aondolewe mitaani maana huko watampoteza haraka sana.
Keako Dkt. Gwajima D tunaomba uliangalie hili pia, kuna mahala jamii inakwama. Shirikiana na Waziri wa Afya mtafute namna ya kuwasaidia watu wanaokumbea na changamoto za afya ya akili.
 
Waziri Gwajima amsaidie huyu jamaa. Mtu anaonekana kabisa mgonjwa wao wanazidi kumfunga. Kichwa chake kimepondeka sana, sijuia alipata ajali. Nadhani hiyo ndiyo imemletea matatizo ya akili.
 
Alikua serious kweli ila niliamini dish halipo sawa baada ya kufuta nyimbo na video zake zote YouTube akidai watu wanapiga mabilioni na wanahujumu muvi yake ya boombattack isitoke
mimi pia mwanzo nilihisi anatafuta umaarufu tu,ila ukimfuatilia ana shida kweli
 
Kwenye uzi vita ya Urusi na Ukraine kuna Deo Kisandu Jr anajiita Maonihuru
 
Mnaona umaskini ulivyo wa hartari? Embu ona mama mzaz anahakikisha mtoto anafungwa jela kisa kitanda..inawwezekana ni mchawi kwel huyo mama na ndie aliemharibia maisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…