Deo Mahinyila Mwenyekiti mpya wa Bavicha ameanza na mguu mbaya ndani ya Chadema mara baada ya ushindi wake.
Mahinyila aliyejipambanua kwamba anamuunga mkono Tundu Lissu kwa siku 2 alizokaa madarakani ameligeuza Baraza hilo kama mali yake binafsi.
Akizungumza katika mkutano wa Mwanaharakati Godbless Lema leo Mwenyekiti huyo wa Bavicha amesema Baraza la Vijana linamtaka Tundu Lissu kuwa Mwenyekiti na si vinginevyo.
Mahinyila ameenda mbali na kusema Baraza lake linawataka vijana kote nchini kutafuta nauli kuja jijini Dar es Salaam tarehe 21 kudhibiti alichokiita watoa rushwa na kuhakikisha Tundu Lissu anachaguliwa kuwa Mwenyekiti.
Deogratius Mahinyila pia anatuhumiwa kukusanya vijana na kwenda nao kwenye mkutano wa Bawacha jana na kufanya vurugu kulazimisha kuingia ndani ya ukumbi kabla ya kudhibitiwa na vikosi vya ulinzi vya chama hicho.
Deogratius Mahinyila anachokifanya ni kinyume kabisa na kanuni kwa sababu hana mamlaka ya kuliamulia Baraza la vijana kwamba achaguliwe nani hiyo ni kujaribu kwa makusudi kuleta vurugu na mgogoro mkubwa ndani ya Baraza na chama.
VIongozi kadhaa waandamizi wa Chadema wamemshauri Katibu Mkuu John Mnyika kumpa onyo kali kijana huyu na ajue mipaka yake kama Mwenyekiti wa vijana wote wa Chadema nchini.
Mara baada ya uchaguzi akishinda Freeman Mbowe Mwenyekti huyu wa Bavicha atapata kazi kubwa kuliongoza Baraza la vijana na kuaminika na Kamati Kuu kutokana na tabia aliyoionyesha iliyo nje kabisa na utamaduni wa Chadema.