Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
YAH: KUJIUZULU RASMI KWA RAIS WA UTPC
Husika na kichwa cha habari hapo juu
12 Novemba 2024
Napenda kuwafahamisha kuwa tumepokea rasmi barua ya kujiuzulu kwa Rais wa UTPC Bw. Deogratius Nsokolo tarehe 10 Novemba, 2024. Baada ya kupata uteuzi na kupata wadhifa ambao kuendelea na kazi yake ya urais kunge kinzana na katiba ya UTPC.
Kwa wakati huu Makamu wa Rais wa UTPC Bi. Pendo Mwakyembe atakaimu nafasi ya Rais, hivyo kwa mambo yote ambayo yalikuwa yaelekezwe kwa rais yaelekezwe kwa kaimu rais Pendo Mwakyembe.
Tunaomba pia muwafahamishe wanachama wenu wa klabu kuhusiana na taarifa hii. Tunamshukuru na kumpongeza ndugu Deogratius kwa uamuzi wake wa busara wa kuheshimu katiba ya UTPC na kuonyesha ukomavu katika uongozi. Tuungane kwa pamoja kumtakia kila la heri katika majukumu na wadhifa wake mpya
Natanguliza Shukrani