Sababu ninayoiona mimi hapa ni tofauti na hii uliyoandika, hilo lorry kutembea juu ya mchanga wa mtoni ndio sababu yake kuanguka na kuzama.
Kwasababu licha ya uzito wa lorry, lakini kawaida nature ya mchanga haiwezi kuhimili kitu kizito { mchanga unamomonyoka kirahisi} hivyo tairi za lorry zikakosa balance zilizohitaji chini ya maji ili ziendelee kujishika chini na lorry kuendelea na safari, ndio maana lorry likasogezwa mpaka kwenye kingo ya mto na hatimaye kuanguka.
■ Hapa ni sawa na wewe ukiwa unazama mahali, lazima utafute kitu chenye kuendana na uzito wako ili kikupe support usichukuliwe na maji, lakini ukijishika kwenye kitu kisicho na uzito sawa na wako, lazima utazama.
Sababu uliyoitoa wewe ningeiamini endapo hilo lorry lingekuwa linatembea juu ya barabara ya lami pamoja na huo uzito wake, kisha nione kama lingezama, au kama unao huo mfano niwekee hapa niuone.