Kuna habari inazunguka pale mtandao wa "X" ikisema dereva wa mtei kauawa na dereva wa Lori za Rwanda je kuna ukweli?
Inadaiwa Dereva huyo wakati anaendesha Bus, njiani alikutana na na Malori mawili kutoka Rwanda...
Malori hayo yalikuwa yanaendesha vibaya hivyo derva akasimamisha gari kwa kutaka kuongea nao, ambapo walimpiga na kumuua..
Your browser is not able to display this video.
=====
UPDATES KUTOKA JESHI LA POLISI
Kamanda wa polisi mkoani Manyara, Makarani Ahmed ametoa taarifa juu ya dereva wa basi la Mtei aliyeuwawa kikatili na dereva wa gari la mizigo na kwamba jeshi hilo linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za mauaji kuhusiana na tukio hilo.
Ikumbukwe kuwa kupitia video clip iliyosambaa katika mitandao ya kijamii ilikuwa ikimuonyesha dereva wa gari la abiria akiwa chini mara baada ya kupigwa na kitu kizito na muda mchache baadaye kupoteza maisha.
NImekutana na clip moja imeharibu siku yangu yote. inaonyesha dereva wa mtei anakata roho na kuna wanaume wameshika fimbo inaonekana ndio wamempiga, inasemekana ni madereva wa lorry. ni kweli?
naomba usiangalie, imeharibu siku yangu. mtu anakata roho anaruka na kutetemeka kakakamaa kama kuku yaani. mtoto wa mwanadamu mwenzio na jamaa mwanaume amesimama na rungu pembeni kama anataka kumwongeza. wakamatwe haraka wauaji hawa.
Huko barabarani kuna mambo mengi sana wakati mwengine kwenye shari na hao jamaa wa malori kama ukiweza hata kama amekugusa muache tu aende ukafanye namna nyingine.
Jamaa ni nusu vichaa zamani tulizoea kuona madereva wa malori wazee siku hizi ni vijana wadogo hekima ya kuamua ni zero.
NImekutana na clip moja imeharibu siku yangu yote. inaonyesha dereva wa mtei anakata roho na kuna wanaume wameshika fimbo inaonekana ndio wamempiga, inasemekana ni madereva wa lorry. ni kweli?
Ni hivi hivi tu kama mleta mada alivyosema,walipishana kauli jamaa wa lorry akamtandika chuma mbili za kichwa (Ile kama nondo ya kushikilia wheel spanner wakati wa kufungua tyre)
Maisha yanatuchanganya sana,huyu ni mfano mzuri wa driver aliyempiga mwenzake mpaka kumuuwa unaweza kuona namna alivyoandika hapa seems yupo very frustrated sasa ndiyo mkorofishane barabarani huyu ataacha kukupiga nondo akuuwe?